Hizi ni kona kali na milima, kwa barabara nchini, taja nyingine

Hizi ni kona kali na milima, kwa barabara nchini, taja nyingine

Kona hatari ni kona za kutoka Mbeya kwenda Chunya. Kona nyingine inaitwa Gangi tololi, kutoka Njombe kwenda Ludewa.
Kona za mkoa zinaitwa unaona bonde la Usangu lileee na gari ikianguka kule ni bye byeee na angalau sasa njia ni rami wamepunguza na milima zamani kipindi hakuna rami ukiwa ndani ya boysasa pale unasali tu.
 
Ipo Njia ya Mkato, Unatokea Mwanza, Nzega, Tabora, Ipole, Chunya, Mbeya. Masaa 8 unaiona Mwanza kama gari iko poa.
Ok, naona gari zinazungukia Dodoma nilidhani Hanna njia ya mkato
 
Magara kwenda Mbulu usha wahi pita ile njia? Hahaaa pira siku moja na hutaomba kurudi na hio njia
Ile njia ni ya kifala sana. As if hayo makona hayatoshi, mwanzoni ilikua ukimaliza izo kona tu kwa mbele kidogo kuna mto mpana nadhani unaingiza maji lake manyara na palikua hamna daraja! Kwahiyo mnapiga mbizi na magari yenu mnaibukia upande wa pili.

Kuna siku nimepambana na makona yangu mpaka nimefika pale mtoni mbupu zote zimevimba, kichwa kinauma, mgongo haufai.. lahaulaa! kumbe kuna mamvua yamenyesha milimani huko mto umefurika balaa haupitiki na imeshabebwa coaster pale! Ikabidi nigeuze aisee nikaanza kupanda tena yale mamilima kwakweli nililaani sana iyo siku. Nimekuja kufika arusha saa 9 usiku.

Screenshot_20210426-161806_Maps.jpg
 
Mkuu, njia ipo unapita mwanza tabora rungwa makongolos chunya mbeya tena ni njia fupi kuliko kuzunguka dodoma..ila tatizo ni njia mbovu sana haina lami
Mbeya-Chunya walishatandaza lami..sijajua huko kwingine.

Ila kona haziepukiki[emoji1787]hizo za Chunya ni bora akapita tu hizo za Mtera.
 
Kaweer
Kona namba moja ilipaswa kuwa nyang'oro , kutoka mtera kwenda iringa.
Na namba mbili ilipaswa kuwa lipumburu, kutoka njombe kwenda songea
Na namba 3 ilipaswa kuwa kawetere
Kawetere kona gan sas, au mlima? Na kama ukitumia mlima bhas kawetere ndio highest point trunk kwa east afrika hakuna barabara ipo juu vile. Hivyo ungeweka namba moja
 
Mi nashangaa watu wanafananisha eti na mburu kusiko hata na maporomoko,

Burdani anapitaga na mpaka 90kmph usiku, Madereva Wageni wengine wakifika Mombo wanaomba Mwenyeji awasaidie kupandisha, No chance for mistakes juu kuna jabali, chini kuna falls kati hapatoshi.

Cha kushangaza Sijawahi sikia ajali njia ilee.
Wasambaa ni madereva asee na unaweza kuta wengine hawana leseni wanatumia uzoefu tu.
 
Morogoro kuna Njia ya kutoka Mlali kwenda Mgeta Kibaoni kuna mlima hatari kuna Kona kali na miinuko mikali pia wameweka kalavati za kupitisha maji kwa juu na njia ni nyembamba. Kama dereva mgeni akipita na gari manual atapata tabu Sana.Ukienda mbele zaidi utakutana na vilima huko Nyandira.
Nlifika huko lolo mpaka nyandira
Alafu hukoo juu kuna bhang imejiotea
Balaa
Sasa njia ya kwenda mgeta wakati unapandisha ukutane na fuso sasa
Kupishana ni mtihani

Ova
 
Utakuwa ulikuwa unapanda KING CROSS/MFALME WA KONA AU URAFIKI.[emoji3]
Kabisa King cross, safari ilikuwa ndefu sana ile kwenye zile kona mnatumia saa zima bado mnahangaika na kona ikitokea gari nyingine lazima msimame ili muweze kupishana, saizi lami hata kona zimepungua na barabara imekuwa pana.
 
Kona 17 kutoka Ziwa Natron kwenda Loliondo hizi hazina mpinzani, kona 15 za Kilimamoto/punda Karatu to Mbulu, kona za Kilimatembo Mtoambu to Karatu, Kona za Rhotia Babati.
Kona za Sekenke Singida to Tabora
 
Back
Top Bottom