Hizi ni Nchi zinazotoa VISA bure, Wabongo tunafeli wapi kusongamana ughaibuni kama Wanaijeria

Hizi ni Nchi zinazotoa VISA bure, Wabongo tunafeli wapi kusongamana ughaibuni kama Wanaijeria

Wabongo nyoso ni wananchi ambao hawana desturi ya kusafiri nje ya nchi. Wote tumesongamana hapa Nchini utafikiri watoto wanaosubiria nyumba ya urithi.

Nchi zinazotoa VISA ya bure kwa Watanzania.

View: https://www.instagram.com/p/CxC5PRyuwra/?igshid=MzRlODBiNWFlZA==

Japokuwa Nchi yetu inashika orodha ya idadi kubwa ya Raia ambao ni zaidi ya milion 60, na kwa Afrika mashariki ndio vinara wa idadi kubwa ya raia, ila hatuna watu wengi wanaotoka nje ya nchi.

Moja wapo ya sababu nchi yetu sio maarufu Duniani kote kama Wanaijeria, wasauzi na Wakenya, ni kuwà Nchi yetu Raia wake sio wengi ughaibuni.

Ukienda nchi za wenzetu Wabongo unaweza kuwatafuta kwa Tochi na usiwapate. Hizo hapo juu ni nchi ambazo huitaji kibali cha Visa kuingia kwao, Yani ni wewe na nauli yako na passport yako basi.

Sasa unakuta na Nchi ni ya Free VISA ila Wabongo bado huwakuti. Hii ni shida sana, na hizi fursa za free VISA watu kama Wanaijeria uwa hawazichezei kabisa.

Ndio maana naijeria ni nchi maarufu duniani kwa sababu Raia wake wametapakaa na kuitangaza nchi hivyo hivyo kwa wasauzi na Wakenya.

Me tatimba nchini Niue inaonekana kuna magoli sanaa ya kutoboa ila ndo ivo uhai inakua roho mkononi
 
Mbona Wachina, Wahindi, Wabelgiji, waarabu na watu wamataifa mengi yasiyo ya kiingereza wanakuja bongo na wengine hawajui hata kiingereza
hao mara nyingi wanaishi kivyao vyao vya na mitaa yao, hata kuchanganyana na wabongo iwe kwenye misiba, kuoana, n.k. wapo kivyao vyao.
 
Mbona Wachina, Wahindi, Wabelgiji, waarabu na watu wamataifa mengi yasiyo ya kiingereza wanakuja bongo na wengine hawajui hata kiingereza
hao mara nyingi wanaishi kivyao vyao na mitaa yao, hata kuchanganyana na wabongo iwe kwenye misiba, kuoana, n.k. wapo kivyao vyao.
 
Moja wapo ya sababu nchi yetu sio maarufu Duniani kote kama Wanaijeria, wasauzi na Wakenya, ni kuwà Nchi yetu Raia wake sio wengi ughaibuni.

Sababu kubwa ni kwamba kupata MKOBA napo ni kipengele ,bureaucracy kama yote ,kijana ambaye nayetafuta maisha kwenda kutoa laki 3 ya passport ,halafu 1.5m ya nauli then hajui anaenda kufanya mishe gani ,anaona hiyo 2m ni bora apambane hapa hapa Bongo.
 
hao mara nyingi wanaishi kivyao vyao vya na mitaa yao, hata kuchanganyana na wabongo iwe kwenye misiba, kuoana, n.k. wapo kivyao vyao.
Hao ndo wazuri sasa kuchangamana na wapuuzi kunaleta majungu
 
Sasa si bora nibakie zangu Kipumbwiko huku kuliko kwenda Pakistan
 
Nchi zenyewe zimechoka hizo hapo yenye ahuweni ni Singapore 🇸🇬 tu hapo ila zungine bora kubaki zako Bahi chimendel huko
 
Back
Top Bottom