Hizi ni Nchi zinazotoa VISA bure, Wabongo tunafeli wapi kusongamana ughaibuni kama Wanaijeria

Kama una taaluma nchi ambayo naona upo vizuri kwa hizo hapo ni Botswana na Namibia. Ila kama hauna taaluma nakushauri baki nyumbani.
 
Tanzania yetu bado ina opportunities nyingi sana, kwenda kwenye nchi kama hizo kwa lengo la kusaka maisha ni ujinga mkubwa.
 
Passport ni 150,000.
Issue inakuja unaenda kufanya mishe gani huko. Inabidi kwanza mtu ujue sio kwenda tu
 
Huitaji kwenda uhamiaji kupata Passport,. passport unaweza kuomba online na kila kitu kufanyia online siku ya kwenda unapeleka tu Documents ambazo ukizoziweka online.
Umefungua uzi na kuanza mjadala ukiwa huna taarifa zitakazo pelekea uzi wako kuwa potential kama title inavyosomeka.
Kwa taarifa yako tu ni kwanlmba, hzo taarifa za kuomba passport online ni za kusadikika.
Ingawa ni lazima ujaze online, ukifika uhamiaji unaanza upya na utatakiwa ku dubmt upya documents zote ulizo submt online pia utaombwa documents zaidi
 
Passport ni 150,000.
Issue inakuja unaenda kufanya mishe gani huko. Inabidi kwanza mtu ujue sio kwenda tu
Si hata kutalii... Ukienda kutalii ndio unajifunza na fursa zilizopo... Sasa wewe huko Tanzania unataka kujua ukafanye mishe gani wakati hujawai kupaona... Hata wenzako wanaofata vitu nje ya nchi, mara ya kwanza wanaenda kama watalii
 
Si hata kutalii... Ukienda kutalii ndio unajifunza na fursa zilizopo... Sasa wewe huko Tanzania unataka kujua ukafanye mishe gani wakati hujawai kupaona... Hata wenzako wanaofata vitu nje ya nchi, mara ya kwanza wanaenda kama watalii
Ndugu yangu..wabongo na kutalii wapi na wapi? Utalii wa ndani tu umetushinda..ni wenye pesa zao tu ndo wanaweza kuwaza kwenda kutalii huko.

Mfano mimi hapa sina mapesa zaidi ya kuweza kujitafutia passport, nataka kwenda kutafuta maisha nje ya nchi , naanzia wapi?
Nipo serious nataka kuondoka hapa...
 
Omba Green Lotary ya Marekani kwenye mtandao wao, ukishinda unapewa Visa... sema hizi nchi zinazohitaji Visa zina complications sana na kupata mpaka uwe mtalii, mwanafunzi au uwe na kazi maalumu iliyokupeleka huko... Unless ujue jinsi ya kudili na hizi viza, Canada nasikia ndio pa kwenda
 
Hiyo bahati nasibu hapana, nataka hizi visa free countries hata burundi, sema sina pa kuanzia
 
Mimi mkenya hapa. Mjadala wako ni wa tija mno ila ukifuatilia vile wenzako wanachangia unapigwa na butwaa hadi huruma tuu. Kwa hizi akili na vile tunahamasisha biashara baina ya waafrika (intra-african trade), kuna kila sababu ya kukiri bado waafrika tuko na safari ndefu sana. Kama kuna mtu anatoka nchi kama Nigeria ama Ghana n.k na bado anaona fursa Tanzania licha ya kuwa anatoka nchi zilizoizidi Tanzania kiuchumi. Bado utaona mtanzania akidharau eti Tanzania yake bado iko bora. Haya kila la heri mandugu zetu, sisi kama wenye shida vile mnavyodai tutatinga tuu hapo bongo na tukipata fursa bila shaka tutaidandia bila kusita.
 
Hiyo bahati nasibu hapana, nataka hizi visa free countries hata burundi, sema sina pa kuanzia
Unataka kwenda kuishi moja kwa moja au kufanya nini... Tuanzie hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…