Hizi njemba(hawa ma-legend) za JF zinatufanya kizazi cha sasa tuonekane tuna upeo mdogo wa kufikiri

Hizi njemba(hawa ma-legend) za JF zinatufanya kizazi cha sasa tuonekane tuna upeo mdogo wa kufikiri

Utandawazi na mabadiliko ya kimifumo ya kimaisha pamoja kumezalisha kizazi Cha aina mbili Cha vijana......

1) kizazi Cha hovyo
Hiki ni kile kizazi kinachosukumwa na upepo wa matukio ya kijamii na mabadiliko ya kimifumo ya maisha kwenye jamii pasi na kutumia fahamu zao.......wimbi hili huzalisha kundi la vizazi jeuri, wabishi, wasio na adabu na wenye viburi.....wao hufanya kile wanachoona kinafaa nafsini mwao bila kuangalia matokeo ya matendo yao......hawana adabu na heshima hata chembe........ kuishi vyema na vijana hawa ni kukaa nao mbali na kuheshimu maamuzi hasa yakiwa hayana muingiliano na mambo yako..... kujaribu kuwashauri au kuwarekebisha kunaweza kukugharimu heshima yako, utu wako na hata usalama wako.......

2) Vijana wenye weledi
Hili ni kundi la vijana walioupokea utandawazi na mabadiliko ya kimifumo ya kimaisha kwenye jamii katika mlengo chanya na ni wanufaika wa mchakato huo kwani wao kwenye hayo huangalia yanayowafaa na kushikamana nayo kuachana na yasiyowafaa........

Vijana hawa hawaoni uzia kutaka ushauri au muongozo Kwa wale waliowatungulia na hujisikia fahari kufanya hivyo.... daima wako kwenye njia sahihi.......

Matunda yake yanaonekana Kwa ustawi wa maisha yao kwenye jamii kwenye yale waliyoshikamana nayo.........

Tumekwisha.
Yaani Vijana wa sasa Waite kwenye Ajira, wafanyie usaili Kwa lugha ya Kiswahili tuu utaona uwezo wao jinsi ulivyo.
Wengi hawajiamini, kujieleza ni shida, sijui nini kimetokea
 
Tumekwisha.
Yaani Vijana wa sasa Waite kwenye Ajira, wafanyie usaili Kwa lugha ya Kiswahili tuu utaona uwezo wao jinsi ulivyo.
Wengi hawajiamini, kujieleza ni shida, sijui nini kimetokea
Hawaamini kwenye juhudi bali Wana amini kwenye shortcuts.....jambo lolote linalohitaji juhudi kwao ni mtihani mzito ndio maana wanashindwa kutoa maelezo madogo tu ili wapate vitu vikubwa......jambo rahisi tu kama kujieleza kupitia kitu ulichosomea chuoni ili kumshawishi mtu mwenye ajira kukupa ajira ni jambo zito kwake vipi kuhusu mengine ambayo hayajui na hakusomea lakini yapo kwenye jamii.......??
 
Kadiri unavyosoma Sana ndivyo ubongo wako unavyozidi kutumika na kuwa Bora zaidi.[emoji1752][emoji1545]

Mkuu nimekufuatilia Kwa miaka Sasa.
Ingawaje wengine wanakusema una-google lakini tunachoangalia ni kile kinachowasilishwa na namna kinavyowasilishwa.

Una-contents za kutosha/ sio content Bali contents za kutosha alafu ni unlimited.
Kuanzia ulipoanza kutoa Nondo mpaka hivi leo angekuwa mwingine angeshapasua matairi.
Na hii tafsiri yake ni kuwa Unakipaji, Kwa maan kipaji ndio mtu huzaliwa nacho na huzikwa nacho, Hakiishi.

Hongera Sana Mkuu
 
Hakuna utambulisho ulionifurahisha kama wa Kiranga aysee!
Mkuu ROBERT HERIEL ukiweza utafute uupandishe hapa! Alinifurahisha sana namna alivyocheza na lugha ya kiswahili

Huyo mtu anatakiwa akutane na Mtu mahiri zaidi kwenye masuala ya Imani na dhahania.
Ili kujadiliana Naye.
Mtu anayetakiwa kujadiliana na kiranga anatakiwa awe katika level Sawa naye kielimu na kiuelewa.
Vinginevyo wengi watamshindwa
 
Unamjua bujibuji wewe? Ana miaka 59 sasa utanuweka kundi lipi? la 1960-1989 au 1990-2022?
 
Uliowataja ni theluthi au ni idadi ndogo sana ya malegend wa kweli waliomo humu, inawezekana hukubahatika kusoma maandiko yao au bado ulikuwa mdogo au umewasahau

1. Barafu
2. Nguruvi3
3. Mzee Mwanakijiji
4. MtiMkavu
5. NyaniNgabu
6. MsemajiUkweli
7. Habíb Hanga ( The Bold)
8. MTAZAMO
9. Paschal

Hawa ni baadhi ya watu wenye kuanzisha/kucomment vitu sensitive sana, huwa na nawakubali sana michango yao/nyuzi zao

Baadhi yao JF imewamiss sana sana

Ngoja niongeze baadhi yao
 
  • Thanks
Reactions: tyc
Uliowataja ni theluthi au ni idadi ndogo sana ya malegend wa kweli waliomo humu, inawezekana hukubahatika kusoma maandiko yao au bado ulikuwa mdogo au umewasahau

1. Barafu
2. Nguruvi3
3. Mzee Mwanakijiji
4. MtiMkavu
5. NyaniNgabu
6. MsemajiUkweli
7. Habíb Hanga ( The Bold)
8. MTAZAMO
9. Paschal

Hawa ni baadhi ya watu wenye kuanzisha/kucomment vitu sensitive sana, huwa na nawakubali sana michango yao/nyuzi zao

Baadhi yao JF imewamiss sana sana
Alikua ajamaliza ndio mana akasema wengine tutaongezea pamoja sana miamba ni wengi.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Bila kumsahau Masanilo kwenye lile jukwaa letu pendwa. Huyu mwamba alikuwa active sana kule [emoji1787]
 
Kwema Wakuu!

Nimeanza kufuatilia JF tangu 2010 hivyo mpaka sasa ni miaka 12. Hivyo ninauzoefu WA kutosha na mambo ya humu ndani. Ingawaje kipindi kile yaani 2010-2013 nikiwa sekondari nilikuwa Kama msomaji tuu lakini bado ninakumbukumbu nzuri ya mambo yalivyokuwa.

Nakiri kuwa humu JF kuna miamba inatupa chakufanya kizazi cha sasa. Ili kutopoteza muda nitataja njemba/ma-legend/ miamba minne ya JF inayowakilisha vyema kizazi cha Kaka au Baba zetu. Ninaposema Kaka au Baba zetu nijazungumzia watu wote waliozaliwa miaka kuanzia 1960 - 1989.
Sisi wa 1990 mpaka Leo tujiite ndio kizazi cha Leo.

Miamba au njemba hizo ni Kama ifuatavyo;

1. Mshana Jr ( Mzee wa Vilinge, Lozi la kimataifa)
2. Pascal Mayalla. (Mzee wa Kura moja)
3. Malcom Lumumba (
4. Gudume. (Mzee wa Fix na Storyteller)
5. Vuta Nkuvute ( Kwa sasa Dodoma)
6. Kiranga. ( Mzee wa metaphysics)
7. Barafu
8 Nguruvi3 (wakimataifa)
9. Mzee Mwanakijiji
10. NyaniNgabu ( USA Baby)
11. MsemajiUkweli
12. Habíb Hanga ( The Bold)
13.. MTAZAMO
14. Mag3

Hao ni wawakilishi WA kizazi cha Kaka na Baba zetu.
Embu linganisha vitu wanavyoandika, namna wanavyoandika, alafu linganisha na siye watoto wa 1990 mpaka hivi leo.
Ndio utajua Sisi bado tunakunywa Uji wa Mgonjwa. Yaani bado uwezo wetu ni mdogo Sana WA kufikiri na kupokea mambo.

Yaani Storage yetu ipo chini.
Sio ajabu watu kulalamika nyuzi zikiwa ndefu,
Nataka kukuhakikishia Makala nyingi zilizondefu ndizo zinazoweza mfanya mtu awe na contents nyingi kichwani.
Kadiri unavyosoma vitu na mambo mengi ndivyo akili yako inavyozidi kupanuka na kutanuka.
Akili yako lazima Uizoeshe kusoma vitu vizito, virefu, na kuweza kuviweka akilini na kuvichambua.

Kuna Taaluma hauwezi Kuhitimu Kama akili yako imezoea vitu vifupifupi au maandiko mafupi fupi mathalani;
Uanasheria, uinjinia, udaktari, Falsafa, uchambuzi wa maandiko n.k.

Ukiona mtu anachoka mapema kusoma maandiko marefu ujue ubongo wake ni Low Storage.
Jambo moja nataka nikuibie Siri, ukiona mtu yeyote ana-content nzito na kubwa kichwani elewa huyo ni msomaji wa vitu virefu na vizito.
Mtu yeyote Yule ukiona unamu-appreciate kuwa Anauwezo mkubwa wa kufikiri au Akili au kuchambua mambo elewa kuwa Siri ni kusoma vitu virefu na vizito.

Kadiri unavyosoma Sana ndivyo ubongo wako unavyozidi kutumika na kuwa Bora zaidi.

Hongereni Sana Kaka na Baba zetu.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Labda wewe hapo.
 
Back
Top Bottom