Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
- Thread starter
- #61
Utandawazi na mabadiliko ya kimifumo ya kimaisha pamoja kumezalisha kizazi Cha aina mbili Cha vijana......
1) kizazi Cha hovyo
Hiki ni kile kizazi kinachosukumwa na upepo wa matukio ya kijamii na mabadiliko ya kimifumo ya maisha kwenye jamii pasi na kutumia fahamu zao.......wimbi hili huzalisha kundi la vizazi jeuri, wabishi, wasio na adabu na wenye viburi.....wao hufanya kile wanachoona kinafaa nafsini mwao bila kuangalia matokeo ya matendo yao......hawana adabu na heshima hata chembe........ kuishi vyema na vijana hawa ni kukaa nao mbali na kuheshimu maamuzi hasa yakiwa hayana muingiliano na mambo yako..... kujaribu kuwashauri au kuwarekebisha kunaweza kukugharimu heshima yako, utu wako na hata usalama wako.......
2) Vijana wenye weledi
Hili ni kundi la vijana walioupokea utandawazi na mabadiliko ya kimifumo ya kimaisha kwenye jamii katika mlengo chanya na ni wanufaika wa mchakato huo kwani wao kwenye hayo huangalia yanayowafaa na kushikamana nayo kuachana na yasiyowafaa........
Vijana hawa hawaoni uzia kutaka ushauri au muongozo Kwa wale waliowatungulia na hujisikia fahari kufanya hivyo.... daima wako kwenye njia sahihi.......
Matunda yake yanaonekana Kwa ustawi wa maisha yao kwenye jamii kwenye yale waliyoshikamana nayo.........
Tumekwisha.
Yaani Vijana wa sasa Waite kwenye Ajira, wafanyie usaili Kwa lugha ya Kiswahili tuu utaona uwezo wao jinsi ulivyo.
Wengi hawajiamini, kujieleza ni shida, sijui nini kimetokea