😁
Umeandika bei kubwa sana aisee...
Kwa Bongo, bei zipo kama ifuatavyo kwa ambazo ni OG kwa wanaume...
EDT zinarange kati ya 120,000 hadi 250,000 inategemea na brand, bei ya chini ni kama Jaguar, Cool Water, CR7, Issey Miyake na jamii zote hapo...
EDP kwenye familia hii, O.G zinarange kati ya 250,000 hadi kwenye 480,000 hapo inategemea na brand, bei ya chini hapa unaweza ukapata Montblanc zote, Mr Burberry n.k, ukiwa na budget nzuri utapata perfume nzuri kama Gucci Guilty, Versace Eros, Ralph's Club, Invictus, ADG n.k
Parfum hapa utakuta bei zake ni 500,000 kwenda juu na kwa bongo sana utakuta kuna Sauvage Exilir, Amouage, Creed, BVLGARI Le Gemme, Tom Ford Oud Wood n.k
Ingawaje siku hizi Dubai naona wamekazana kutoa copy ambazo ni low budget na inaonesha zinafanya vizuri, sijawahi tumia lakini nimeona unyunyu wa Amraf kama Club de Nuit una reviews nzuri...