Pre GE2025 Hizi pesa zinazotumika kuchafua chaguzi za CHADEMA, zimeingia kupitia "Mlangoni" au " Dirishani"

Pre GE2025 Hizi pesa zinazotumika kuchafua chaguzi za CHADEMA, zimeingia kupitia "Mlangoni" au " Dirishani"

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Rabbon

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2022
Posts
21,625
Reaction score
33,688
Salaam, Shalom!!

Amesikika Makamo Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu akitahadharisha wanachama wa CHADEMA kuwa makini sababu tayari Kuna pesa zimeingia kuchafua chaguzi ndani ya chama.

Amedai pesa za kuandaa mikutano ndani ya chama imekuwa ikipatikana Kwa taabu, lakini Cha kushangaza, katika chaguzi ndani ya chama, pesa zimekuwa nyingi, na amesema hadharani kuwa, pesa hizo zimetoka Kwa Abdul na Mama yake ingawa hakufafanua.

Pesa kuingia kupitia " MLANGONI" ni pesa Rasmi, Ruzuku, michango ya chama kama Join the chain nk nk, ila ikiwa zimepitia " DIRISHANI" ni pesa haramu.

Swali linakuja kuwa ikiwa zimepitia DIRISHANI, nani wahusika ndani ya chama waliohusika kuruhusu hujuma hizo?

Na ikiwa zimepitia MLANGONI Kwa maana ya kuwa ni pesa Rasmi, nani wako nyuma ya pesa hizo kutumika kuhonga wanachama wa CHADEMA?

Kwa mara ya kwanza Makamo Mkt, anakeemea hadharani RUSHWA ndani ya chama ilhali viongozi wa Iringa na njombe waliotajwa wako kimya!!

Swali: Pesa hizo, ni Rasmi za Ruzuku, michango ya wanachama kujitolea, au ni za Dirishani/ mlango wa uani?

Karibuni🙏

Pia, soma=> Tundu Lissu atahadharisha uchaguzi ndani ya chama kuingiliwa na fedha za Rais Samia na mwanae Abdul
 
CHADEMA imeonyesha ukomavu wa " Kujisahihisha" Ili kukisafisha chama Ili kisihujumiwe na mapandikizi,

Mnachagua kiongozi Kisha anageuka kukihujumi chama, kumbe Hawa ambao Huwa wanauza majimbo, ndio Hawa mapandikizi aliowataja Leo Lissu?

Ni kwema mbeleni.
 
Samahani mkuu, unaweza ukawa na video akizungumza haya uiweke? Ukomavu wa Chadema utaonekana wakikubali kujisahihisha. Siasa ni chess, ukizubaa kidogo umeliwa.
 
Samahani mkuu, unaweza ukawa na video akizungumza haya uiweke? Ukomavu wa Chadema utaonekana wakikubali kujisahihisha. Siasa ni chess, ukizubaa kidogo umeliwa.
Ameyasema hayo Leo Iringa. Ingia U-Tube.
 
Chadema mnarithisha siasa za kuriaria hv hamjui hli dude lipo tayari hata kumwaga damu hili kuwepo marakani hv hamna mbinu mbadala
Lissu amesanua mapema,

Mipango ovu inafail yote.

Mapandikizi yote yangolewe mapema!!
 
Uchaguzi wa 2024 na 2025 ni WA aina yake.

Naona kama CHADEMA wamedhamiria kuondoa CCM.

Tusubiri.
Sio mchezo, kwa hizi mambo zinaendelea kwa sasa, uchaguzi utakuwa na vitu vingi sana ngoja tusubiri.
 
Bora Lisu ameweka wazi huo uhuni, haya mambo ya kukalia kimya fedha chafu ndio yamefanya tumekosa imani na siasa za kupigania tumbo.
Lile jukwaa la miti alilowekewa Lissu, ni Ishara chama hakina pesa,

Sasa kwenye chaguzi zimetoka wapi?

Na Zina intention Gani?

Tujisahiihishe!!
 
Uchaguzi wa 2024 na 2025 ni WA aina yake.

Naona kama CHADEMA wamedhamiria kuondoa CCM.

Tusubiri.
Kama mkojani fc akishupaza Shingo halafu like jabali lilifanya mikutano nchi nzima Kila jimbo likapewa nafasi upande was pili bhas hata mwenyekiti was kampeni was mkojani na kamati nzima itapigia kura chadema!!
 
Nia ya kupandikiza viongozi mapandikizi ndani ya chama, wake kugombea ubunge na nafasi zingine, waijua?

Ndio hao wanaweza kuzuia Jabali asiingie chamani.

Jambo zuri ni kuwa, mipango ovu inaharibiwa Kwa wakati sahihi.
 
Lisu ni ngumu kumpisha jabali ujue!!

Maana kazi anayoipiga lisu siyo ya kitoto kabisa!!
 
Waliopoteza matumaini na Sanduku la kura warudishe tumaini!!

Tume huru na Katiba mpya kabla ya Uchaguzi wowote itapatika a kupitia njia ya maandamano.

Tujitokeze kujiandikisha katika zoezi la kuboresha daflali la mpiga kura hivi karibuni.
 
Back
Top Bottom