Hizi pocket router za Voda zikoje? Naombeni ushauri kabla sijajichanganya

Ukichukua leo hii Router ya Airtel zile ODU, kuna form unajaza. Soma ile form vizuri wameandika pale kwamba unapaswa kutumia huduma yao ndani ya miezi 24.

Ukishindwa kununua Internet kwao ndani ya miezi mitatu mfululizo, Router inabaki kuwa mali ya Airtel.

Hivyo ndivyo form inavyosema.
 
sahihi kabisa
 
Kwa sasa ni bora Kununua router yenye unlimited maana hizi za GB 10, 20 nk zinakata ndani ya siku mbili wakati unategemea umalize mwezi.
 
A
Achana na maandishi yalioandikwa kwenye form tafuta uhalisia. Wanachuo wamenunua sana hizo router kwa ajili ya biashara na wameshindwa kulipa wanaziuza wengi tu, Usikariri hii ni Tz sio US.
 
Ninayo laini ya ya Yas unlimited bundle unaweka kwenye simu sio lazima router au Mifi ila sasa unapata 10Mbps kwa 70k
 
A

Achana na maandishi yalioandikwa kwenye form tafuta uhalisia. Wanachuo wamenunua sana hizo router kwa ajili ya biashara na wameshindwa kulipa wanaziuza wengi tu, Usikariri hii ni Tz sio US.
Mkuu, mimi nimezungumzia hali ya mkataba ulivyo, ishu ya utekelezaji sijaelezea, nimesema tu kwamba mkataba unasema hivi na hivi.
 
Ziko vizuri tu, Nina Alcatel router ya Vodacom tangu mwaka juzi inapiga kazi kulindana na mahitaji yangu ya kila siku. Kwa miaka yote natumia vifurushi vya Internet vya wiki kwa shs 5000.
Sijawahi kukwama labda pale CCM/TCRA wanapoingilia kati kama ilivyokuwa October 29. 😆
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…