Hivo wewe unaona kuna maendeleo hapo?kama maendeleo ni picha basi hayo ni maendeleo tena makubwa sana.
Kipindi ujenzi wa barabara za Mwendokasi unaanza tulionyeshwa hivi hivi mipicha ya kung'aa ila kwenye reality wenyewe tumeona matokeo yake,pale pale tulipoonyeshwa picha za kituo kizuri cha hayo mabasi pamekuwa ndo hapakaliki panatia hasara bus zinafia pale barabara lenyewe halipitiki alimradi vurugu.
Mie sio mwanasiasa,fuatilia post zangu humu na ujue sio kila anaepingana na wewe ni mwanasiasa na kwa sababu siasa zimekujaa kichwani hata ile akili yakufikiri tofauti umeitoa.hii sio dalili nzuri kwa kizazi chako.