Hizi sadaka ambazo wahubiri wakristo wanazipigia debe mpaka mapovu yanawatoka ni kwa sababu zinaingia mifukoni mwao?

Hizi sadaka ambazo wahubiri wakristo wanazipigia debe mpaka mapovu yanawatoka ni kwa sababu zinaingia mifukoni mwao?

raslimali

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2014
Posts
1,958
Reaction score
1,744
Huwa najiuliza maana siku hizi huko kwenye redio na mikutano ya kikristo msisitizo mkubwa ni sadaka. Ingekuwa sadaka hizi haziwanufaishi hawa wahubiri( wao husema mtolee Mungu), wangekuwa kweli na bidii ya kutengeneza mafundisho haya (aghalabu mengi ni ya uongo na matisho tu) yenye msisitizo wa kutoa sadaka?

Hakuna tena mkazo kwenye kuokoa roho za watu maana hizi hazina faida kwao. Wahubiri wamegeuka kuwa watu wa kujipatia mapato ya aibu kama biblia inavyosema. Pesa,pesa,pesa. Wameipa majina mengi mara sadaka, mara matoleo, mara sadaka maalum....n.k lakini yote ni PESA inatakiwa. Unaitwa kwenye mikutano ya injili uanaambiwa eti hakuna kiingilio.

Ukifika huko unahubiriwa habari za kutoa na kutishwa kwa laana zitakazokupata usipotoa. Ni aibu kabisa kwa imani yetu ya kikristo. Hakuna tena apostolic succession. Mtu anaibuka from nowhere na motive yake ni kutengeneza pesa anaanzisha kanisa lake. Shame on those who have turned the gospel into a commodity to sell. Watapata adhabu iliyo kuu.
 
Lakini hakuna kifungo kama usipotoa. Kama utaona sio sawa usitoe tu...... Mimi nikiwa nayo huwa naona sawa kutoa tu...ila kipindi sina nikisikia toa huwa nakua mnungunishi lakini sijaacha kutoa......... Kama wanafanya ndivyo sivyo shauri lao na Mungu wao (Kkkt )
 
Kutoa ni hiari kwa mwenye nayo, usiende mikononi Mwa Bwana mikono mitupu na kama hauna usiache kwenda ibadani kisa huna kesho utapata.
SAsa usipotoa Tanesco watalipwa nini,maji je,vocha je,nauli, chakula ,mafuta,betri,walinzi,nk.
Kazi ya sadaka ni kuhudumia kanisa,
 
Huwa najiuliza maana siku hizi huko kwenye redio na mikutano ya kikristo msisitizo mkubwa ni sadaka. Ingekuwa sadaka hizi haziwanufaishi hawa wahubiri( wao husema mtolee Mungu), wangekuwa kweli na bidii ya kutengeneza mafundisho haya (aghalabu mengi ni ya uongo na matisho tu) yenye msisitizo wa kutoa sadaka? Hakuna tena mkazo kwenye kuokoa roho za watu maana hizi hazina faida kwao. Wahubiri wamegeuka kuwa watu wa kujipatia mapato ya aibu kama biblia inavyosema. Pesa,pesa,pesa. Wameipa majina mengi mara sadaka, mara matoleo, mara sadaka maalum....n.k lakini yote ni PESA inatakiwa. Unaitwa kwenye mikutano ya injili uanaambiwa eti hakuna kiingilio. Ukifika huko unahubiriwa habari za kutoa na kutishwa kwa laana zitakazokupata usipotoa. Ni aibu kabisa kwa imani yetu ya kikristo. Hakuna tena apostolic succession. Mtu anaibuka from nowhere na motive yake ni kutengeneza pesa anaanzisha kanisa lake. Shame on those who have turned the gospel into a commodity to sell. Watapata adhabu iliyo kuu.
Tenganisha kidogo si wakristo.Ni hao wa makanisa yanayoitwa ya wokovu yanayo milikiwa na mtu binafsi.
 
Hakuna mafanikio ya bure si kwa shetani wala Mungu wote utumia kanuni moja, Ili upate ni lazima utoe. Masikini ni masikini kwa sababu awatoi.
Sasa ulitaka masikini atoi nini mzee na yeye mwenyewe hana kitu.
 
Kutoa ni hiari kwa mwenye nayo, usiende mikononi Mwa Bwana mikono mitupu na kama hauna usiache kwenda ibadani kisa huna kesho utapata.
SAsa usipotoa Tanesco watalipwa nini,maji je,vocha je,nauli, chakula ,mafuta,betri,walinzi,nk.
Kazi ya sadaka ni kuhudumia kanisa,
Sijaacha kutoa na siwezi acha.
 
Na huko watu hutoa kwa uaminifu mkubwa sana..... Hata wakiambiwa damu za watu wapo tayari.
Kabisa. Kifupi kila mtu ale anakopeleka mboga. Tusipangiane kabisa. Hela ni zetu tunazotoa sadaka, wao anawalaumu nani wanapopeleka ng'ombe kwa waganga? Wakae kimya kabisa.

Kila mtu ashinde mechi zake
 
Sasa ulitaka masikini atoi nini mzee na yeye mwenyewe hana kitu.
Hao ndo watuaji wazuri sasa.... Tena wakipewa mfano wa yule mama alokuwa na unga kidogo akampikia mtushi halafu akabarikiwa zaidi ndo kabisa wanatoa mpaka utashangaa..... Waumini wa mwamposa,wanunuzi wa mafuta yake ni watu gani zaidi?
 
Back
Top Bottom