Hizi shule za English Medium zimetugeuza Wazazi kuwa Walimu?

Niliwahi kumfanyia dogo homework akaenda akakosa yote
Hebu kila mtu afanye kazi yake wasee mi na stress zangu za pesa na kujipiga na nyundo kwenye vidole badala mwalimu ufanye kaz yako unaniongezea mzigo na mm tena?
[emoji1] [emoji1] [emoji1] halagu ukikosea tu mtoto anaanza kusema hujui,kesho yake anatafuta mwingine wa kumsaidia
 
1. Zero grazing 2. Non zero grazing
 
Nilikataa kbs habari za tution
Wanatafuta pesa tu kiujanja
 
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]
 
Niliwahi kumfanyia dogo homework akaenda akakosa yote
Hebu kila mtu afanye kazi yake wasee mi na stress zangu za pesa na kujipiga na nyundo kwenye vidole badala mwalimu ufanye kaz yako unaniongezea mzigo na mm tena?
Sipati picha..ulivyomdisappoint dogo
 
Nyie ndo wazazi mtoto atakuja kukuambia nimevunja photosynthesis ya shule tunadaiwa afu ulivyo boya unampa pesa kulipia fidia! Jitaidi ujue hata Yes and no!
 
Mtoto anapewa "Homework" ili aushughulishe ubongo wake na siyo akuulize wewe mzazi umsaidie. Siyo jukumu lako wewe mzazi kumsaidia mtoto wako kufanya "homework" , ukimsaidia unamfanya kuwa tegemezi.

Lengo la homework ni kumfanya mtoto atumie akili zake mwenyewe kupata majibu kwa kufikiri zaidi na siyo kuuliza majibu kwako wewe mzazi.
Na hata kama mtoto atakuuliza umsaidie homework yake, kama wewe mzazi una uwezo kielimu basi usimpe majibu ya moja kwa moja, mpe majibu yatakayomfanya aushughulishe ubongo wake yeye mwenyewe kupata majibu sahihi.
Mtoa mada usilalamike, inaonekana wewe ndiyo hujui lengo la mtoto wako kupewa homework. Akija kwako na homework mwambie anapaswa kutafuta majibu yeye mwenyewe na ni lazima aifanye. Tena mwanao akikwambia eti hawajafundishwa huyo ni mwongo, ni lazima wamefundishwa, sema yeye hakuwa makini darasani wakati Mwalimu anaelekeza. Kikawaida Mwalimu hawezi kuwapa watoto homework kwa mambo ambayo hajawafundisha.
 
Hivi kuna kilimo cha kuhamahama 🤣🤣🤣🤣
 
Nasoma koment nacheka jamani ...

Ngoja nmpe mwanangu swalehe simu na yeye acheke
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mleta mada upo sahii sana. Home work si kitu cha kujifunza upya ni kitu cha kujikumbusha.

Mimi haiwezekani nimfundishe mtoto.

[emoji117]Jinsi ya kuanza sentensi na herufi kubwa
[emoji117]Kupiga mistari
[emoji117]Kuachanisha sentensi.

Huu ni ujinga nafundisha jinsi hata ya kusoma yani mzazi niligundua mtoto hajui kusoma anakariri halafu mwalimu hajui hilo. Siku nitawaibukia shule watajua hawajui.....

Hizi shule ni bomu sana...
 
Nilikataa kbs habari za tution
Wanatafuta pesa tu kiujanja
Of course, hata mimi nimekataa. Ila tatizo mtoto wangu hajaelewa vizuri. Mfano, kwenye maths mtoto naona amefundishwa kujua missing number in an ascending order. Mfano, akipewa swali kama: fill in the missing numbers: 1, 2,--, --, 5,--, --, ---, 9, etc anajua. Lakini akipewa swali kama: fill in the missing numbers: 11, --,--, --, 7, --, --, --, 3, mtoto ataandika 12, 13, 14, 15, 16, 17. Kwa hiyo, inawezekana mwalimu hajawahi kuwaonyesha hizi njia mbili kwamba kwenye ascending order unaanza na namba ndogo kwenda kubwa na kwenye descending order unaanza na namba kubwa kwenda ndogo. Sasa hivi nimeamua nitenge muda wangu angalau kila siku kwa nusu saa nipitiea vitabu wanavyotumia na ni'formulate' maswali kwa muda kadhaa mpaka nitakapojiridhisha kwamba ame'catch up'. Otherwise, akienda darasa la 2 akiwa tabula rasa hivi, hatakuwa amepta background nzuri kwa mambo ya msingi.
 
Ili mtoto aweze kufanya vizuri kimasomo kuna factor mbili ambazo huwa za msingi sana,external na internal!external ni mazingira yanayomzunguka kuanzia nyumbani mpaka shuleni,na internal ni yeye mwenyewe mtoto!
Ukielewa hili kama mzazi wala hutapata shida na hizo homework za mwanao
Kwenye internal pia watoto wanatofautiana kuna ambao wanajiweza wenyewe wakiwa nyumbani bila kuwa pushed kuanzia kwenye masomo mpaka activitiez zingine,lakini wengine ni mpaka mzazi utoe msaada haswa akiwa home
Wewe kama mzazi lazima uelewe hili as hiyo ni future ya mwanao na huo mzigo huko mbele unaubeba wewe na wala sio mwalimu
 
[emoji1787] wanachosha na huwa hawakubali kirahisi ukiwaambia ntasaini kesho...ninao wawili basi kila siku ni kusoma...!
 
Acha tu, kijana wangu kaisha kabaki kichwa tu...! Akirudi ana homework zaidi ya 1 anafanya kisha analala anaamka tena alfajiri kumalizia namuhurumia lakini simuoneshi...ajikaze tu si kwa ubaya [emoji5]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…