Hizi shule za English Medium zimetugeuza Wazazi kuwa Walimu?

Hizi shule za English Medium zimetugeuza Wazazi kuwa Walimu?

[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1], Eti anakufikiriaje?? Si anakufikiria hujasome au we ulitakaje
Kwa kweli ni kero na udharirishaji kwa sisi wazazi tusiosoma yani mwanangu daily homework ngumu lugha ndio sielewi basi inabidi nimsukume kwa jirani akamsaidie uko, Sasa sijui jirani ananifikiriaje[emoji1]
 
Acha kabisa mkuu, binafsi pia inaniboa mnoo. Hapa dogo kaniletea maswali,nmejibu lakini kuna maswali mawili nmechemka.wajuzi wanisaidie please.

1.Farming involving permanent settlement is called...........
2.Farming with no permanent settlement is called.............

Nmemuambia akalale,namtafutia majibu atajaza alfajiri..nmejaribu ku Google lakini wapi
1- Settled farming
2- Migratory farming
 
Kwa kweli ni kero na udharirishaji kwa sisi wazazi tusiosoma yani mwanangu daily homework ngumu lugha ndio sielewi basi inabidi nimsukume kwa jirani akamsaidie uko, Sasa sijui jirani ananifikiriaje😄
duuh mkuu unampeleka kwa jirani yani baba na mama wote weupe kichwani??? hata google kutumia ikupe mwanga 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣
 
Enzi zetu somo kama hilo 'Social' ndio ilikuwa Historia,Jiografia. Nakumbuka, mfano
Mtu unasoma vitu vya kueleweka kabisa; mf: Kilimo cha mahindi - Marekani, kilimo cha migomba -Kagera, nk.
Historia, Jiografia, na Civil studies. Ilkuwa inaeleweka vizuri. Sahi mambo yanabadilika sana.
 
Walimu wanatugeuza wazazi tuwe wanafunzi! Too much work na watoto wanasema hawajafundishwa! Alafu mtoto amerudi saa 12 jioni unampa home work maswali 30 -50 kweli?

Hizi shule ndio zitafanya watoto wachukie shule! Darasa la 3 au 4 lakini anakuwa overloaded.
 
Na kimsingi haina maana kwa sababu homework ni yake yeye na anatakiwa afanye yeye mwenyewe ili kujua kama ameelewa au la... Sasa mwalimu anaposema nimsaidie huwa nashindwa kuelewa kabisa!
 
Watoto kila siku wanarudi na homework mpya mzazi uwasaidie. Ukimuuliza anakuambia mwalimu hajamuelekeza akaelewa.

Sasa nalipia ada zaidi ya milioni ili watoto wapewe homework niwe mwalimu wao?
Kwa nini hawawafundishi wanafunzi wakaelewa ndipo wawape hizo home work wakazifanye!?

Wazazi wengine hatuna hulka ya kufundisha na wengine ndio tuliishia la sababa.

Tunatafuta hela na kulipa ada ili walimu wawafundishe sio watuletee homework kuja kutupima ujinga wetu..!! Walimu fanyeni kazi yenu ya kufundisha msihamishe goli.

Mbona kwenye ada hatupunguziwi kwamba tumeshiriki kufundisha watoto hivyo tulipwe stahiki zetu!
yes , lipa ada kama hutaki peleka Kayyumba huko.
 
Dogo aliwahi kuja na hii, "Parents use mobile phones, ___________, ___________ and ________.

😂😂😂😂😂!

Utopolo mtupu.

Swali ambiguous lisilokuwa na mbele wala nyuma!
Tecno, Huawei and Oppo. 😂😂😂😂

Nimecheka hilo swali ni utopolo indeed!
 
Siku moja jioni tumetoka job Boss akaniambia tupite kwake kwani mkewe amepika maandazi ya motomoto tukale. Kufika tukakuta ubishani kati ya mama na mwanae kuwa namba X kwa kirumi ni namba ngapi kwa kiingereza, Mama anamwambia mwanae ni 20 mtoto naye anadoubt ni kama vile anakumbuka na hakumbuki vizuri. Tulivyofika mtoto akamdaka babaake akamuuliza, baba akajibu ni 10. Mtoto akamwambia "mom said it's 20", nikaona Boss anabana kicheko na mimi nikabana kicheko, mkewe akaona akamind fulani hivi, Boss akamwambia hujui X kweli? akajibu najua nilikuwa namchallenge dogo, deep down alikuwa hajui. Boss akamwambia tena "hujui bwana" (saa hiyo mtoto yuko huko hasikiin kinachoendelea), Mama kuambiwa vile akang'aka nusu alimanusra tusipewe maandazi, Ikabidi Boss amzugie mkewe kwa kumwambia unajua bwana, tena kuanzia leo jina lako ni profesa wa hesabu. 😀😀😀 Nilicheka sana kimoyo moyo siku hiyo, Uzuri ni kuwa hawaogopi kutaniana mbele yangu kwani wamenizoea pia, Mke wa Boss ni kama wifi yangu tu. Hadi leo tunamuita mama H, Profesa wa hesabu.

Siku nyingine nikamwambia ujue wii unatumia iphone X ambayo ni iphone 10 tulicheka mno tena.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Aisee elimu ya tz ni upumbavu mtupu,

Sasa hapo hiyo homework atakuwa kafanya mwanafunzi au mzazi?

Lengo la homework ni kumpima mwanafunzi kama kaelewa alichofundishwa au la!
Yani unampa kazi akafanyie nyumbani kulingana na kile alichofundishwa!

Sasa mzazi ukimfanyia akaenda kupata vema atajiona na akili lakini kiuhalisia anakuwa hajaelewa chochote.

Hizi shule kumbe bora mtoto umpeleke kayumba tu.
Mkuu,mimi ni mhanga wa hili tatizo. Walimu wengi wanatoa kazi ya nyumbani kwa topic atakayofundisha kesho. Ukiwauliza walimu majibu yao wanasema wanamuandaa mtoto kuelewa haraka.
Kama amefundishwa mgogoro wa mtoto na mzazi siku hiyo unakuwa haupo zaidi ya kusaini diary.
 
Watoto kila siku wanarudi na homework mpya mzazi uwasaidie. Ukimuuliza anakuambia mwalimu hajamuelekeza akaelewa.

Sasa nalipia ada zaidi ya milioni ili watoto wapewe homework niwe mwalimu wao?
Kwa nini hawawafundishi wanafunzi wakaelewa ndipo wawape hizo home work wakazifanye!?

Wazazi wengine hatuna hulka ya kufundisha na wengine ndio tuliishia la sababa.

Tunatafuta hela na kulipa ada ili walimu wawafundishe sio watuletee homework kuja kutupima ujinga wetu..!! Walimu fanyeni kazi yenu ya kufundisha msihamishe goli.

Mbona kwenye ada hatupunguziwi kwamba tumeshiriki kufundisha watoto hivyo tulipwe stahiki zetu!
Elimu ni shuleni na nyumbani.
 
Hii ishu haikubaliki!! Kuna mzazi hajasoma anapambana kutafuta pesa amsomeshe mwanawe apate Elimu bora!! Nenda shule kwa Mkuu wao, muulize lengo la homework ni nini??? Maana ni mazoezi ya kurudia alichofundishwa!! Na sio kuwapa wazazi kazi ya kufundisha!!!
 
Hayo ya kuwategemea 100% ndio yaliyotufikisha hapa hivi sasa, hata mwanao akikuuliza kitu unashindwa kujibu kwa kuwa hukufunzwa kujishughulisha!
Japo mimi sina taaluma ya kufundisha lakini kwa sasa bila shaka mfumo wa utoaji elimu umebadilika!

Umetoka kwenye content based hivi sasa ni competence based, ambapo mwanafunzi ndiye anayepaswa kuwajibika zaidi! Mwalimu kazi yake ni kumwelekeza mtoto cha kufanya, hivyo kumtengenezea namna ya kufikiri na kutafiti zaidi!

Binafsi mwanangu anapofika nyumbani na homework ninavyoona anavyopambana kutafuta maelezo, nafurahia sana! Japo mara chache nipatapo nafasi namsaidia kidogo ila ameshazoea, na mara nyingi inabidi kitu kiwe kigumu sana ndio aulize!

Na hiyo ni baada ya kukosa majibu aliyoyaelewa maana hapendi kabisa kuandika kitu ambacho hakielewi!

Hivyo tusiwalaumu waalimu wa watoto wetu hivi sasa kwamba wanawabebesha mizigo, badala yake tuulaumu mfumo tuliopitia sisi ambao zaidi ulitufanya tuwe tegemezi pasipo kupata ujuzi wa kutosha!
Naunga mkono hoja. Mzazi hutakiwi kumpa au kufanya wewe hiyo home work.Mtafutie nyenzo.Mfano, uwe na vitabu husika vya darasa analosoma mwanao waandishi tofauti.Mfano: Tie, Longhorn,adamson , na kama unajiweza uwe na kompyuta na umfundishe namna ya kuitumia n.k hivyo akikosa jibu anaweza kutafuta mwenyewe kwenye hivyo vitabu.EMitaala ya sasa ni "competency based"
 
Back
Top Bottom