Stori zako mkuu zinaweza kuwa kweli ila si sababu ya kisayansi ya Yanga kufungwa, hizo ni taarabu tu mtani.
Shida ya Yanga kwasasa ni ndogo sana tu, ni timu kukosa mbadala wa Baka na Job, yaani wachezaji wengine wafundishwe tu namna Baka na Job wanacheza pale nyuma ili hao jamaa wakikosekana pasiwe na Shida, wanapokosekana timu inakosa balance pale nyuma hasa akili ya kukaba na kuanua mipira, simple problem wala sio ishu kubwa Tabora United walistudy goli la Azam lilivyopatikana baada ya Baka kutolewa kukawa free pale nje ya box nao wakarudia na kushinda Yanga, ishu ndogo tu wala si jambo la kutuhangaisha wana utopolo . Tushajua panapovuja ni kuimarisha kukaba katikati nje na ndani ya box letu wapinzani wasipige mipira, problem fixed.
Magoli manne Yanga imefungwa hadi sasa yote yametokea katikati juu kidogo ya box la Yanga, au ndani ya box ila katikati sehemu ambayo Baka au Job hucheza na kuanua mipira, hivyo ni kazi ndogo tu Master Gamondi tunajua ashaona, kama bado basi walio karibu nae wamwambie Yanga itafute mchezaji wa kuziba pengo la Baka au Job kazi kwisha, sote tunajua bado ubingwa uko pale pale Yanga ndo maana tuliwapigia makofi wachezaji badala ya kung'oa viti!!