Hizi tozo kubwa kwenye uingizaji magari zinalenga nini hasa?

Mtu hajachangia hata mia ila anakunja zaidi ya mtengenezaji na mnunuaji.

Hizi pesa ndizo wanahongea wanachuo
 
Vipi ukinunulia gari Malawi au huko Zambia halafu ufanye kuileta hapa bongo, kodi yake imekaaje.??
Hawaeleweki muda mwingine inakua juu kuliko ya kutoa SA kama hizi Cruiser ila zingine watajifanya kukokotoa uchakavu wa huko harafu unalipia kidogo ila naona haipo sawa maana unaweza kununua gari iliyolipiwa kodi Malawi na ukaja nalo Tanzania kama Scania hizi au Fuso..
 
RAV hazikamatiki
Zipo zina kodi ya Tsh 40m zingine mpaka 50m wakati kununua ni Tsh 25m tu ya miaka ya karibuni sijui Watanzania nani alituroga tunataka watu watumie magari masumbufu na mabovu mabovu huku wakiwafukuza wauza parts mijini lakini hawatatui tatizo la kupunguza kodi kwa magari ya miaka ya karibuni au mazuri..
 
Tuna madini, gesi, mito na bahari, mbuga kibao.....hivi ni vichache?
 
Tuna madini, gesi, mito na bahari, mbuga kibao.....hivi ni vichache?
Mbona mna vichwa vigumu? Nimeandika hawa watu (gov) sio wabunifu ndio maana wamekomaa no magari kwasababu ni rahisi kutega pale bandarini.
Hawaangalii vyanzo vingine wanakomaa na vile vile vyanzo rahisi. Hata wafanyabiashara wanasumbua wale wale wanawapandishia kodi kila mwaka baada ya kutafuta wengine wapya ambao hata hawalipi kodi.
Kwa nchi yenye wabunifu magari used sio chanzo cha mapato.
 
Well
 
et kuhamasisha bidhaa za ndani...
Tunazalisha gari wapi au matoroli ni substitute products za magari
Sijui waliwaza nini wakati wanaseti hivi viwango Malawi,Congo ,Zambia ,Burundi ,Uganda na Rwanda wana sera nzuri za ku encourage uingizaji magari mapya yenye uchakavu mdogo na wanapitishia bandari yetu hii hii ya Dar ila wanatozwa pesa kidogo ila sisi bado tunaumizana kwa kutwishana mizigo ya kodi mpaka tunarithishana magari mabovu utafikili hatuna bandari
 
Mtu wa Uganda au Zambia mkiwa na mtaji sawa vitu mtatumia tofauti majumbani mwemu kwa sababu ya kodi Tanzania unalipia gari harafu wahuni wanakuja kukagua kama umebeba microwave wanakuuliza kama mpya inatakiwa ulipie kodi hata kama ulikotoka nayo uliitumia kidogo ukairudisha kwenye Box wao ni utata mpaka unawashangaa umasikini tulio nao upo kwenye damu na imekua kama kansa..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…