Hizi zilizowekwa katika barabara za miji ndani ya Wilaya ya Mbulu ni Lami au Kitu gani?

Hiyo ni lami ya kichina, baada ya kushindilia wanamwaga mchuzi wa lami, baadae wanamwaga kokoto kubwa, na baadae kokoto ndogo hapo mchezo umeisha.
 
Hiyo ni lami ya kichina, baada ya kushindilia wanamwaga mchuzi wa lami, baadae wanamwaga kokoto kubwa, na baadae kokoto ndogo hapo mchezo umeisha.
Yeah. Mtaani kwangu huku mwanza wamejenga barabara ya hivi. Kifusi kinashindiliwa wanamwaga huo mchuzi wa lami then kokoto.

Magari yakipita baada ya mda kokoto inashikana na huo mchuzi wa lami nyingine zinakaa pembeni ndo barabara hiyo
 
Naomba kujua kuna aina ngapi za lami, maana lami iliyowekwa ktk miji hii haifananni na lami ninazoziona ktk miji mingine ktk nchi hii.
Lami zipo za aina nyingi. Kuna lami inayochangywa kati ya lami(binder) na kokoto kwenye mtambo kabla ya kuwekwa barabarani na hii huwezi kuona kokoto zikitoka.
Kuna lami ambayo unatanguliza uji uji wa lami kisha kokoto hufuata huku zikikandamizwa na roller na hii kuona kokoto pembeni zilizotoka hakuepukiki na sio kwamba imejengwa chini ya kiwango. Ni kwamba lami ya aina hii lazima baadhi ya kokoto zitatoka yaani lazima itatokea baadhi ya kokoto kutogundishwa na lami lakini haitakiwi zitoke zote na layer ya chini ionekane.

Lami nilizotaja ni zile ambazo tunazitumia sana hapa nchini lakini katika ulimwengu wa lami kuna zaidi ya hizo na kati ya hizo nilizotaja lami bora na ambayo ni gharama ni ile inayochanganywa kati ya lami na kokoto kwenye mtambo kabla ya kuwekwa barabarani.

Ahsante.
 
Picha
 
Hatuelewi weka picha
 
Yeah. Mtaani kwangu huku mwanza wamejenga barabara ya hivi. Kifusi kinashindiliwa wanamwaga huo mchuzi wa lami then kokoto.

Magari yakipita baada ya mda kokoto inashikana na huo mchuzi wa lami nyingine zinakaa pembeni ndo barabara hiyo
Barabara ya Malimbe ndio imetengenezwa hivyo mi nikajua ujenzi haujaisha kumbe ndio imetoka ivyo
 
Hii ni bitumen au lami iliyochanganywa na kokoto kwenye mambo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…