Hofu yatanda kwa wafanyabiashara wa Coco Beach, wadai kupewa mwezi mmoja kuondoka kumpisha mwekezaji

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251
Hofu yatanda kwa wafanyabiashara wa Coco Beach: Wadai kupewa mwezi mmoja kuondoka kumpisha mwekezaji.

Wakizungumza na The Chanzo leo, wajasiriamali na wafanyabiashara wadogo kwenye fukwe za Coco wamesema baadhi ya viongozi na watendaji wa Halmashauri ya Kinondoni waliwaita na kuwapa taarifa ya kutakiwa kuondoka ndani ya siku 30 kupisha uwekezaji.

Katika malalamiko ya wafanyabiashara hao, wameeleza pia kusikitishwa na kauli za watendaji hao kwa mfanyabiashara wa kike, kauli zenye viashiria ya kutaka rushwa ya ngono. Kufuatia malalamiko haya ya wafanyabiashara wadogo, The Chanzo inaendelea na jitihada za kuwapata halmashauri ya Manispaa ya kinondoni kutoa ufafanuzi juu ya madai ya wafanyabiashara hawa.

Ni wakati wa jiji la DSM kuwa na maeneo ya kupumzikia (parks)... Kama mwekezaji atapaendeleza coco beach kwa ajili ya wananchi kupumzika haina tatizo cha muhimu gharama ziwe rafiki na kodi zilipwe. Tatizo ni kama mwekezaji atajenga majengo ya hotel na kuzuia wananchi kujinafasi. Hawa wafanyabiashara wadogo mara nyingi hawafuati sheria na kutaka kuonewa huruma kipuuzi. JPM alikuwa na mazuri yake ilakuruhusu wafanyabishara wadogo wapange biashara hadi barabarani ilikuwa sio sawa. Ninasubiri maelezo ya halmashauri ili niweze kutoa maoni yenye tija.
 
Mara ya kwanza kufika Dar, nilikuwa nasikia Coco Coco ikabidi niandae Siku nifike hapo.

Labla mm n mshamba ila sikuwa na ule msisimko wa kupajua mana kila kitu nilikiona cha kawaida hapo.

Anyway, JPM alisema hiyo sehemu ibaki ya wananchi.

Sasa, Acha wenye nchi wafanye watakavyo mana JPM mlimuona ni dikteta.

Samuya hoyeeeeeeee
 
Hoyeeeeeee
ccm safiiiiiiiiiii?
 
Ni wakati wa jiji la DSM kuwa na maeneo ya kupumzikia (parks)... Kama mwekezaji atapaendeleza coco beach kwa ajili ya wananchi kupumzika haina tatizo cha muhimu gharama ziwe rafiki na kodi zilipwe. Tatizo ni kama mwekezaji atajenga majengo ya hotel na kuzuia wananchi kujinafasi. Hawa wafanyabiashara wadogo mara nyingi hawafuati sheria na kutaka kuonewa huruma kipuuzi. JPM alikuwa na mazuri yake ilakuruhusu wafanyabishara wadogo wapange biashara hadi barabarani ilikuwa sio sawa. Ninasubiri maelezo ya halmashauri ili niweze kutoa maoni yenye tija.
Kwamba watakuwa wanapumzika bure kama ilivyo sasa?
 
Hofu yatanda kwa wafanyabiashara wa Coco Beach: Wadai kupewa mwezi mmoja kuondoka kumpisha mwekezaji.

Wakizungumza na The Chanzo leo, wajasiriamali na wafanyabiashara wadogo kwenye fukwe za Coco wamesema baadhi ya viongozi na watendaji wa Halmashauri ya Kinondoni waliwaita na kuwapa taarifa ya kutakiwa kuondoka ndani ya siku 30 kupisha uwekezaji.

Katika malalamiko ya wafanyabiashara hao, wameeleza pia kusikitishwa na kauli za watendaji hao kwa mfanyabiashara wa kike, kauli zenye viashiria ya kutaka rushwa ya ngono. Kufuatia malalamiko haya ya wafanyabiashara wadogo, The Chanzo inaendelea na jitihada za kuwapata halmashauri ya Manispaa ya kinondoni kutoa ufafanuzi juu ya madai ya wafanyabiashara hawa.

View attachment 3563164
Mnayemwita mama ndio amewachomoa hapo 😂, mjomba wa Oman kapewa beach
 
Back
Top Bottom