Hofu yatanda kwa wafanyabiashara wa Coco Beach, wadai kupewa mwezi mmoja kuondoka kumpisha mwekezaji

Hofu yatanda kwa wafanyabiashara wa Coco Beach, wadai kupewa mwezi mmoja kuondoka kumpisha mwekezaji

Ukifika tu pale na gari kabla hujaoingia kupaki, wanakja mawinga kama 10 wanazunguka gari kila mmoja anakuita huku mara kule makelele mengi ni kero tupu mpaka utaka kuwagonga wengine wanasima mbele ya gari wanapigapiga boneti na makelele yao
Unaongea tu ni kwa vile huko njema, assume hauna kitu, na wewe ungekuwa unapambana mahali. Shida ya Tanzania ni kutosaidia wafanya biashara kama hao. Hao ni kama kondoo waliokosa mchungaji au kukua wa kienyeji. Generally CCM hawana mipango na watu wake.
 
Ni wakati wa jiji la DSM kuwa na maeneo ya kupumzikia (parks)... Kama mwekezaji atapaendeleza coco beach kwa ajili ya wananchi kupumzika haina tatizo cha muhimu gharama ziwe rafiki na kodi zilipwe. Tatizo ni kama mwekezaji atajenga majengo ya hotel na kuzuia wananchi kujinafasi. Hawa wafanyabiashara wadogo mara nyingi hawafuati sheria na kutaka kuonewa huruma kipuuzi. JPM alikuwa na mazuri yake ilakuruhusu wafanyabishara wadogo wapange biashara hadi barabarani ilikuwa sio sawa. Ninasubiri maelezo ya halmashauri ili niweze kutoa maoni yenye tija.
Uwekezaji wa Coco beach ni wa hotel kubwa subiri utaona.
 
Ukifika tu pale na gari kabla hujaoingia kupaki, wanakja mawinga kama 10 wanazunguka gari kila mmoja anakuita huku mara kule makelele mengi ni kero tupu mpaka utaka kuwagonga wengine wanasima mbele ya gari wanapigapiga boneti na makelele yao
Si ndiyo kuchangamka penyewe hapo watu mchakamchaka

Ova
 
Mara ya kwanza kufika Dar, nilikuwa nasikia Coco Coco ikabidi niandae Siku nifike hapo.

Labla mm n mshamba ila sikuwa na ule msisimko wa kupajua mana kila kitu nilikiona cha kawaida hapo.

Anyway, JPM alisema hiyo sehemu ibaki ya wananchi.

Sasa, Acha wenye nchi wafanye watakavyo mana JPM mlimuona ni dikteta.

Samuya hoyeeeeeeee
Oyee
 
Si ndiyo kuchangamka penyewe hapo watu mchakamchaka

Ova
Kwa kweli hapana, mbona wewe mwenyewe umehama nchi
Inatakiwa uende kwa utilivu, ufike upaki gari kama zamani miaka ya 90 kumetulia mpaka wahindi walikuwa wanakuja picknic pale familia nzima, walivyoweka yale mabanda kumekuwa tena sio sehemu ya kistaarabu, ni kama wameweka sehemu ya migahawa kama vile uko manzese.
 
Ni wakati wa jiji la DSM kuwa na maeneo ya kupumzikia (parks)... Kama mwekezaji atapaendeleza coco beach kwa ajili ya wananchi kupumzika haina tatizo cha muhimu gharama ziwe rafiki na kodi zilipwe. Tatizo ni kama mwekezaji atajenga majengo ya hotel na kuzuia wananchi kujinafasi. Hawa wafanyabiashara wadogo mara nyingi hawafuati sheria na kutaka kuonewa huruma kipuuzi. JPM alikuwa na mazuri yake ilakuruhusu wafanyabishara wadogo wapange biashara hadi barabarani ilikuwa sio sawa. Ninasubiri maelezo ya halmashauri ili niweze kutoa maoni yenye tija.
bravo COCO pale kuingia 30,000
yaan ni ushetani tu kunyanganya maeneo ya maskini kusingizia uwekezaji
 
Kwa kweli hapana, mbona wewe mwenyewe umehama nchi
Inatakiwa uende kwa utilivu, ufike upaki gari kama zamani miaka ya 90 kumetulia mpaka wahindi walikuwa wanakuja picknic pale familia nzima, walivyoweka yale mabanda kumekuwa tena sio sehemu ya kistaarabu, ni kama wameweka sehemu ya migahawa kama vile uko manzese.
Uzuri historia ya muuza mihogo coco hapo naijuwa vizuri sana,longtime pale mbuyuni primary school st peters, kuna mzee mmoja alikuwa anaishi hapo(mzee masharubu) alikuwa akiuza mihogo shuleni na ikifika jioni anasogea mdogo mdogo na familia coco kuuza mihogo badaye wengine wakaanza kuunga tela.

Tukirudi kwenye mada,hapa serikali ndy inatakiwa iwaboreshe hao wafanyabiashara kuanzia mazingira +miundo mbinu
Wakisema wawalete wawekezaji wajenge restaurants sehemu za kisasa zaidi,yaani watu wa class fulani ndiyo waingie
Itakuwa imeathiri watu
Kumbuka hapo kuna watu wanaenda kufanya mazoezi mchangani pia

Ova
 
Hofu yatanda kwa wafanyabiashara wa Coco Beach: Wadai kupewa mwezi mmoja kuondoka kumpisha mwekezaji.

Wakizungumza na The Chanzo leo, wajasiriamali na wafanyabiashara wadogo kwenye fukwe za Coco wamesema baadhi ya viongozi na watendaji wa Halmashauri ya Kinondoni waliwaita na kuwapa taarifa ya kutakiwa kuondoka ndani ya siku 30 kupisha uwekezaji.

Katika malalamiko ya wafanyabiashara hao, wameeleza pia kusikitishwa na kauli za watendaji hao kwa mfanyabiashara wa kike, kauli zenye viashiria ya kutaka rushwa ya ngono. Kufuatia malalamiko haya ya wafanyabiashara wadogo, The Chanzo inaendelea na jitihada za kuwapata halmashauri ya Manispaa ya kinondoni kutoa ufafanuzi juu ya madai ya wafanyabiashara hawa.

Mlisha tiki October, huu ndo muda wa kukinywea kikompee
 
Back
Top Bottom