Hoja alizoibua CAG sio ufisadi mpaka zikose majibu

Wewe jamaa akili kubwa sana
 
Mpaka CAG anatoa report kwenda kwenye mihimili ujue hoja zimekosa majibu huko zilikokaguliwa. Baada ya ukaguzi huwa kuna exit meeting ambapo mkaguliwa lazma atoe majibu ya queries zote zilizoibuliwa na mkaguzi.

Nadhani wewe mleta uzi ndo hujaelewa vema..punguza jazba.

Sent from my SM-G935U using JamiiForums mobile app
 
Kimsingi huo ni wizi wa wazi kabisa...cha msingi hapo ni utekelezaji wa mapendekezo yake ikiwemo kuwachukulia hatua wahusika.

Sent from my SM-G935U using JamiiForums mobile app
 
Unaleta pumba? Hoja hapa ni kama audit querries ni ufisadi we unaleta ngonjera.
Audit queries ambazo hazielewek or hazina majib always zinakwenda bungeni! Kwanza mbona kama unapamban kuliko uwezo wako ili kulinda legacy? Kuna vitu ambavyo havifichiki mfano..pembe la ng'ombe!! Think about it
 
Audit queries ambazo hazielewek or hazina majib always zinakwenda bungeni! Kwanza mbona kama unapamban kuliko uwezo wako ili kulinda legacy? Kuna vitu ambavyo havifichiki mfano..pembe la ng'ombe!! Think about it
Acha PAC na LAAC watoe majibu.
 
Sikia jamaa yangu labda kama hujui kitu,mkaguzi hutoa hoja za kiukaguzi na kuwapa wahusika ili wajibu,wapojibu akiridhika huwa anaondoa hoja hizo,baada ya hapo sasa,ndipo hutoa hadharani ripoti yake,na akishaitoa huwa ni final,kinachobaki ni hatua tu kuchukuliwa na wahusika,hivyo hiyo ripoti ya c.a.g ni final report
 
CAG huwa anaimba ngojera tu wenzake wanapiga pesa na hakuna hatua zinazochukuliwa na mwakani atakuta tena madudu.
Sijui nini maana ya. Auditing zaidi ya serikali kujivua nguo kwa wananchi. Sijawahi ona watu wamewahi chukuliwa hatua kwa ripot ya CAG
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…