Dam55
JF-Expert Member
- Oct 8, 2015
- 5,641
- 11,958
Wasalaam wakuu,
Hili ni wazo langu tu kwaajili ya kuleta afya ya kiuongozi kwa Tanzania yetu ili kupunguza hatari za kiuongozi zinazoweza kutokea na nchi kujikuta ikiangukia kwenye mikono ya watu ambao hawakujiandaa kuwa kwenye nafasi fulani fulani za kiuongozi.
Katiba yetu iko wazi jinsi madaraka yanavyoweza kubadilika ikiwa kitatokea chochote wakati wowote.
Hivyo basi ni muhimu sasa kwa vyama vya siasa viweke umakini mkubwa kwenye uteuzi wa wagombea wenza ili tuhakikishe watu wanao patikana tuwe na uhakika na uwezo wao kwenye nafasi kubwa kama hiyo pindi itakapotokea dharura yoyote ile tusiteteleke kiutawala.
Ni ukweli ulio wazi kuwa vyama vya siasa mara nyingi sana vimekuwa vikifanya mizaha kwenye uteuzi wa wagombea wenza bila ya kuangalia kwa makini takwa la kikatiba kuwa watu hao wanaweza kuja kuwa wakuu wa nchi siku moja.
Wagombea wenza limeonekana Kama suala dogo sana lisilo na uzito wowote na maranyingi limechukiliwa kirafiki na kishikaji sana bila kujali madhara yake.
Rejea uchaguzi wa 2020 angalia wagombea wenza wote kwenye vyama vyote kisha angalia katiba yetu inasemaje ndipo utagundua mzaha tunao ufanya Watanzania.
Mungu tusaidie waja wako, kama ugombea wenza ni ushkaji basi tuimulike Katiba kwenye vipengele fulani.