Hoja binafsi: Vyama vya siasa viwe makini sana kwenye uteuzi wa wagombea wenza katika chaguzi zijazo ama sivyo Katiba imulikwe

Hoja binafsi: Vyama vya siasa viwe makini sana kwenye uteuzi wa wagombea wenza katika chaguzi zijazo ama sivyo Katiba imulikwe

Swala hapa sio ugombea mwenza pekee ila swala ni vyama kuwa makini katika swala zima la uchaguzi wa Rais. Rejea tena uchaguzi wa 2020.
 
Ni kweli; hata mimi nimeshaona tatizo la kikatiba hata. Ile katiba ya zamani ilikuwa inasema rais akifa, basi uchaguzi mwingine unafanyika kujaza nafasi yake kama ambavyo anapokufa mbunge nafasi yake inajazwa kwa uchaguzi mdogo. Mabadiliko ya kusema makamu wa rais anakuwa automatic na akishachukua madaraka anafanya lolote atakalo ikiwa ni pamoja na kupangua serikali aliyokuta, linaweza kuwa unintended consequences kwa mustkhabali wa nchi.
Wacha tukadese kwenye katiba ya Zanzibar. Naona imekaa kimkakati.
 
Sheria hazitungwi hivyo! Sheria zinaangalia long term na inabidi ziheshimiwe, siyo ikifika wakati wa kutekeleza sheria husika mnaona ni inconvenience. Ndiyo maana mmebadili sheria nyingi kwa sababu mliona zinazuia kutekeleza matamanio yenu!

Ila unachosema kina ukweli kwa upande mwingine. Kutokana na mfumo wa Muungano, Zanzibar imependelewa sana. Imagine kama wagombea wa Rais wa JMT wakiwa 20, kinchi kama Zanzibar nacho kinajihakikishia at least wagombea (wa Urais au Makamu) 20 kati ya hao! Matokeo yake, vyama vingi havipati wagombea wenza makini au wale wanaoonekana wana hadhi ya kuwa Marais.
Mkuu kwenye hili nimecheka sana. Hivi tulipoungana haikujulikana ukubwa wa eneo la Zanzibar? Au ndiyo ile dhana ya kuitawala ili isifurukute? au ndio mbadala wa kutupwa kwenye bahari ya Hindi? Waswahili husema ukipenda boga, penda na mti wake. Hata hivyo mama yupo, ni Raisi kikatiba na ataendelea kuwepo mpaka muda wa kuondoka utakapofika.
 
Ndg Yangu Kubaliana na Khali tu Rais wa JMT ni Mama SSH, Hauna Namna. Mama SSH anatosha na ametuonyesha ni Jinsi gani anatosha. Je ulishawahi Kujua tangu Ndege ya Kwanza hadi ya Nane ni Hasara kila Mwaka kwa Kwenda Mbele. Je angekuwepo Mwendazake ungejua hizi hasara BIl.150 only kwa Midege tena Mibovu.

Serikali halali ni seriali ya watu na kuna transparency, sasa ya Mwendazake iligubikwa na usiri mkubwa kwani ni serikali iliyokwishakujua ina Makandokando Mengi na ya Kutisha. Wenye Hakili Tuliliona hili Mapema ya Mwaka wake wa Mwanzo wa Utawala wake.. Karagabaoo.
Hasara na midege mibovu, unaongea kwa hasira sana mkuu. Unaonaje tukimshauri mama hii midege iuzwe yote kisha na shirika lifutwe watanzania tuachane kabisa na mambo ya usafiri wa anga tuachie tu wenzetu wanao nunua midege mizima na wasio pata hasara wao ni mwendo wa faida tu.

Hi biashara imetushinda au sivyo mkuu?
 
Ni kweli vyama vyote vilikuwa vinadharau sana juu ya hili kwa kuchagua wagombea wenza incompetent. Ila kwa hili lililotokea naamini litakuwa no funzo tosha.
Incompetent kwenye nn ,mana ubovu wakiongozi na uzuri wake nimatokeo yakatiba....msichanganye maswala
 
KATIBA imulikwe mengine hayo yote yatakaa sawa..kikwete alikua mzoefu ,magufuli mzoefu,Samia suluhu mzoefu ...sasa mnataka nn
 
Nimeandka nimefuta karibu mara 5 kwa hyo mgombea mwenza wa CCM mwaka 2020 alikuwa mzaha au una maana gani?
 
Achana na mambo ya mgombea mwenza wewe mataga Katiba mpya itakayoimarisha taasisi ndio kila kitu.
 
Wasomaji wa biblia wanajua Daudi kabla ya kuwa mfalme alikuwa mchunga kondoo ni Mungu tu mwenye uwezo wa kuinyanyua mtu na kumshusha bila kujali background yake.
 
Sheria hazitungwi hivyo! Sheria zinaangalia long term na inabidi ziheshimiwe, siyo ikifika wakati wa kutekeleza sheria husika mnaona ni inconvenience. Ndiyo maana mmebadili sheria nyingi kwa sababu mliona zinazuia kutekeleza matamanio yenu!

Ila unachosema kina ukweli kwa upande mwingine. Kutokana na mfumo wa Muungano, Zanzibar imependelewa sana. Imagine kama wagombea wa Rais wa JMT wakiwa 20, kinchi kama Zanzibar nacho kinajihakikishia at least wagombea (wa Urais au Makamu) 20 kati ya hao! Matokeo yake, vyama vingi havipati wagombea wenza makini au wale wanaoonekana wana hadhi ya kuwa Marais.
CCM ni chama cha kizanzibari kiasili kwa sababu mapinduzi yalifanyika visiwani na si bara. Hivyo subirini wazanzibari waendeshe chama na nchi yao.
 
Huwezi kuwa mgombea mwenza kama huna sifa za kuwa Rais kwa mujibu wa katiba. Acha dharau,Acha ujinga.
 
Mama Samia ndio Rais wetu wether like it or not,nyie team mwendazake kubalianeni na matokeo, Samia is far better than jiwe Mungu kamleta wakati sahihi kabisa
 
Chama changu kilikosea jambo moja kuu kutuwekea mgombe ambaye kwanza walijua ni mgonjwa lakini pua walizijua tabia zake
Wasirudie Tena uraisi si wamajaribio tunataka kiongozi wa kulinganisha na sio kuharibu Mambo na umoja wa kitaifa, na sio kiongozi hafati katiba na Sheria, Yani anakuwa top of everything kila kitu aliharibu Mara democracy,Uhuru wa kujieleza, Mara Sheria za mitandao almradi purukushani tupu
 
KATIBA imulikwe mengine hayo yote yatakaa sawa..kikwete alikua mzoefu ,magufuli mzoefu,Samia suluhu mzoefu ...sasa mnataka nn
Mkuu hakuna tunachotaka zaidi ya kupunguza mizaha kwenye kuteua wagombea wenza ukinielewa hapo basi hakuna kesi mkuu
 
Back
Top Bottom