Habari za Zanzibar
JF-Expert Member
- Dec 18, 2024
- 651
- 433
Hoja Dhaifu za ‘Wheel Cover’: Kutoka kwa Maria Sarungi
Kwanza kabisa, hoja ya kuunganisha “wheel cover” kutoka kwa Maria Sarungi ni dhaifu sana kimantiki. Hii ni correlation fallacy kuona vitu vinafanana halafu unahitimisha vina uhusiano bila ushahidi wa moja kwa moja. Tanzania kuna maelfu ya magari yanayotumia wheel covers za aina moja au zinazofanana kimuonekano; hii si kitu cha kipekee wala ushahidi wa uhalifu.
Pili, unapotaja tukio lililomhusisha Mwigulu, ni muhimu kuweka muktadha sahihi wa muda na nafasi za uongozi. Wakati wa matukio ya maandamano unayorejea, Mwigulu hakuwa Waziri Mkuu. Hivyo, kujaribu kumhusisha moja kwa moja na tukio kwa kutumia picha au muonekano wa gari ni kupotosha ukweli na kuchanganya umma.
Tatu, hoja yako inategemea hisia badala ya uchambuzi wa ushahidi. Katika uchunguzi wa masuala mazito kama mauaji, vyombo vya dola hutumia:
Nne, hata hoja yako yenyewe inaonesha udhaifu: unasema “plate namba tofauti lakini gari muundo uleule.” Hapa tayari kuna contradiction kama namba ni tofauti, basi unahitaji ushahidi mwingine mzito kuunganisha magari hayo, sio kubahatisha kwa muundo ambao upo kwa maelfu ya magari nchini.
*** lazima muache kubuni mambo wananchi si wajinga

- Namba za chassis (VIN)
- Rekodi za umiliki wa gari
- CCTV na ushahidi wa kitaalamu