Kwakuwa tuko wengi na kila mmoja kwa ufahamu na uwezo wake wa akili, basi kila swali ni sahihi bila shaka...
Kwa sababu binadamu tumejengwa ktk mazoea. Mazoea mengine yakiwa mazuri na mengine siyo...
Rais John P. Magufuli hana mazoea ya kujificha au kutenda kazi zake kwa kificho kwa muda mrefu kiasi hiki. Linapotokea hili, ni halali watu kuuliza maswali kwa namna yoyote ile...
Kwa maoni yangu, labda serikali wangejibu watu wote jibu moja tu kuwa;
"....Rais amebadili mazoea yake ya kutoonekana hadharani na sasa atakuwa anafanyia kazi zake mafichoni. Kwa hiyo na ninyi wananchi, badilisheni mazoea ya kumwona Rais wenu mara kwa mara, kumsikia anasema nanyi mara kwa mara. Kuanzia sasa atakuwa anasemewa na VP au PM...."
Kwa jibu hili labda watu tungeelewa na kuchukua mazoea mapya japo isingekuwa mwisho wa maswali kuendelea kuulizwa..
Nje ya jibu hili hakuna wa kuelewa maana hata wewe hujaelewa wala huamini majibu haya...
Aidha, wote tunajua kuwa kwa mtu ambaye tunakutana naye kazini mara kwa mara, siku zote na ghafla kwa takribani mwezi mzima anakuwa haonekani kazini tena bila taarifa za kwanini, na yuko wapi na akiwa ktk state gani, basi moja ya haya laweza kuwa jibu..
1. Anaumwa sana, na amefichwa sehemu...
2. Katekwa nyara na haijulukani watekaji wamemficha wapi..
3. Kafa, amezikwa na walioshirki mazishi hawataki kusema..
Hivi ndivyo ilivyo, na ndipo tulipofikia...