Hoja dhidi ya Hoja: Maswali Sahihi Huleta Majibu Sahihi: Tatizo la Kudhania Kutoonekana kwa Magufuli

Hoja dhidi ya Hoja: Maswali Sahihi Huleta Majibu Sahihi: Tatizo la Kudhania Kutoonekana kwa Magufuli

Mzee uneandika mengi mno.
Andika machache tu.

Yuko wapi? Jibu lake fupi litamaliza yote
 
Mwanakijiji umetandawaza vizuri uwanja sahihi wa kuuliza maswali sahihi, mahali sahihi, wakati sahihi na kwa lengo sahihi kuliko kuuliza maswali yenye majibu pendekezwa tayari huharibu mahusiano kati ya muuliza swa;li na mtoa jibu.

TANBIHI: Napingana na wewe kwamba kuna upako kutoka kuzimu (Anointment from Hell?) No, You can't be serious

Kilichopo ni kwamba kuna kufuru kutoka kuzimu (Irreverence/profane from hell).

Kwa hiyo hicho kitabu acha kukitangaza kwa kuwa kina haribu fikra sahihi.
 
Mimi nashukuru Magufuli hapotezi muda kujibizana na wahuni!

Angalia yule mhuni Amsterdam aliandika vibarua wee hakuna hata balozi wa nyumba 10 alimjibu.

Sembuse hili la wahuni waliojazana kule twiter?
 
Cha kushangaza ni kwamba wanaoulizia Rais aliko ni walewale waliotuambia yuko nairobi hospital, ni walewale waliotuambia yuko kati ya sehemu mbili[emoji849] india au china [emoji848][emoji848]

Yohane johnthebaptist hawa watu tuwaiteje!?
Na wataendelea kuuliza ikiwa hawataridhishwa na majibu.
Mleta Uzi atoa ufafanuzi wa Aina ya maswali.
Mojawapo maswali chokonozi
 
Mkuu mimi naona ni vyema wasaidizi wa Rais wawe mbele katika kutoa taarifa sahihi ili kuepuka watu kuanza kuwa na hisia tofauti. Muda wa zaidi ya wiki mbili kwa Rais kutokuonekana hadharani ama katika luninga ama hata kusikika redioni ni jambo ambalo ni lazima litaamsha shahuku na udadisi kwa watu wengi..
Siku hizi humuanini Lissu? Si ameshawaambia alipo?
 
Hili swala la mzee wetu kutingwa na majukumu kiasi cha kushindwa juzi kwenda kanisani linakuzwa sana na wahuni akina kigogo2014, hivi kweli kama rais angekuwa amepelekwa nje ya nchi unadhani tusingetangaziwa,maana sioni sababu ya rais kwenda nje ya nchi bila kututaka watanzania tumuombee

Dunia inavyomhofia na kumhaha Rais John Pombe Magufuli wangeshatangaza.... kweli MAGUFULI anawatia matumbo joto😃😃😃

Yaani hadi BBC na reporter wao Tundu na koloni lao la Kenya waligeuka kuwa kituo cha uzushi

Mungu ibariki Tanzania Mungu mbariki Rais wetu John Pombe Joseph Magufuli 😍🇹🇿🙏
 
Nimekusoma tu we bwana kwamba ni mbishi sana. Lakini kama maswali yanayoulizwa ju ya kitu kizur na anayehoji unaona kabisa anania ovu. Haina mana asihoji lakini picha ya nadharia ni kiroho mbaya huna haja ya kumuamini. Unampuuzia. Na huu ni wakati sahihi kupuuza upotoshojaji wenye nia katili,ovu kwa watu wema.

Hapa Hoja ni moja tu unastarehe unapoteleza kwenye lami? Unapopita kuna amani? Unalala ukaamka mtaani kwako kumetulia, huoni raha mwanao anaposomeshwa, kazi yako kuchangia kwa kumsimamia afaulu na wewe kushiriki kwenye shughuli za kukuza uchumi na kazi za kijamii. Huombi dua njema?? Kwa nn uombe dua mbaya kwa watendaji wa Mungu, wateule....why
 
Tatizo lenu mnataka rais ajitokeze vile mnavyotaka nyie.. hata Kama ningalikuwa mimi nisingelijitokeza kwa maneno ya watu ili niwaridhishe. Kama haipo sababu ya maana ya kujitokeza heri aendelee na ratiba zake ni ujinga cheo Kama chake afanye kitu kwa mashinikizo ya watu fulani tu wa kupakaza maneno!. Tena ikibidi akae hata miezi mitatu hivihivi tena ndo raha..😊😁
 
Ulichoandika sijaona hoja hapa

Zaidi zaidi naona kama unataka kujikosoa nakuona ulikosea kwenye ile thread yako ya "ya rais kama anaumwa tuambiwe"

Umeingiwa na woga.

Swali linabakia lile like "Rais yuko wapi"?

Kama ni mzima ajitokeze hadharani, kama anaumwa tuambiwe.
Mzee yuko kwenye Mfungo, Kwaresma hii! watu muambiwaje ili muelewe? subirini amalize mtamuona! simple and clear!

Na nikipindi nimeshuhudia uimara wa TISS, na wale wanaojifanyaga wana connection hadi ndani ikulu safari hii wameprove wrong! kazi kubahatisha bahatisha tu habari! hahahahahahaha,
Vijitundu vyote vimezibwa
 
Kwakuwa tuko wengi na kila mmoja kwa ufahamu na uwezo wake wa akili, basi kila swali ni sahihi bila shaka...

Kwa sababu binadamu tumejengwa ktk mazoea. Mazoea mengine yakiwa mazuri na mengine siyo...

Rais John P. Magufuli hana mazoea ya kujificha au kutenda kazi zake kwa kificho kwa muda mrefu kiasi hiki. Linapotokea hili, ni halali watu kuuliza maswali kwa namna yoyote ile...

Kwa maoni yangu, labda serikali wangejibu watu wote jibu moja tu kuwa;

"....Rais amebadili mazoea yake ya kutoonekana hadharani na sasa atakuwa anafanyia kazi zake mafichoni. Kwa hiyo na ninyi wananchi, badilisheni mazoea ya kumwona Rais wenu mara kwa mara, kumsikia anasema nanyi mara kwa mara. Kuanzia sasa atakuwa anasemewa na VP au PM...."

Kwa jibu hili labda watu tungeelewa na kuchukua mazoea mapya japo isingekuwa mwisho wa maswali kuendelea kuulizwa..

Nje ya jibu hili hakuna wa kuelewa maana hata wewe hujaelewa wala huamini majibu haya...

Aidha, wote tunajua kuwa kwa mtu ambaye tunakutana naye kazini mara kwa mara, siku zote na ghafla kwa takribani mwezi mzima anakuwa haonekani kazini tena bila taarifa za kwanini, na yuko wapi na akiwa ktk state gani, basi moja ya haya laweza kuwa jibu..

1. Anaumwa sana, na amefichwa sehemu...

2. Katekwa nyara na haijulukani watekaji wamemficha wapi..

3. Kafa, amezikwa na walioshirki mazishi hawataki kusema..

Hivi ndivyo ilivyo, na ndipo tulipofikia...
 
Kama anaumwa kweli majaliwa na mama samia mtaonekana waongo na wasanii itabidi mjiuzulu
 
Cha kushangaza ni kwamba wanaoulizia Rais aliko ni walewale waliotuambia yuko nairobi hospital, ni walewale waliotuambia yuko kati ya sehemu mbili🙄 india au china 🤔🤔

Yohane johnthebaptist hawa watu tuwaiteje!?

You are wrong 100%...

Kwa akili yako na mimi unaniweka kundi hili?

Lakini pia hata ingekuwa hivyo, kwani kuna kosa kuuliza hivyo?
 
Back
Top Bottom