Uchaguzi 2020 Hoja fikirishi: CHADEMA kwanini mnadai Uhuru wa Vyombo vya Habari huku mkivinyima haki, kufukuza na kuvidhalilisha!?

Wasamehe bure... watu wanaongea wakiwa bwii kwa nyagi unategemea kuna busara hapo???
 
Mjinga mkubwa. Unafikiri kwa tako badala ya kichwa.
 
Wewe jamaa mahaba yako kwa ccm yanakufanya kuwa taahira. Mbona bwana yule huwa hadi anatukana kabisa, kuita wateule wake wapumbavu lakini huwa hawazimi sauti wala kufanya walichofanya leo? Acha kutetea ujinga.

Siku nyingine hua anasema atapiga mashangazi lkn tbccm hua hawaoni hayo.
 
Kama unafikiri kuwa TBC ni chombo cha habari basi wewe ni miongoni mwa ma-punguani...!!
 
Tatizo liko wapi? hata kama wakitoa uchambuzi huoni kama walikuwa wakitimiza majukumu yao na wanapaswa waachwe wafanye kazi yao kwa uhuru?
Tuone kesho Mzee meko atakatishwa hotuba yake
 
..ungejitahidi kuwa BALANCED kwa kueleza makosa ya pande zote, yaani TBC, na CDM.

..lakini mimi kwa upande wangu sijaona tatizo lolote ktk kauli ya TL kwamba wananchi waandamane kwa AMANI kudai haki yao.
Jokakuu hapa suala sio kauli ya TL au kauli ya Mbowe.

Kukifukuza chombo cha habari huoni ndiyo uminywaji wenyewe wa habari?

Mfano mzuri tu ni ukandamizaji wa serikali dhidi ya vyombo vya habari ambao tumekuwa tunaupigia kelele hapa.

Kama serikali inafungia chombo cha habari kisa tu kinatofautiana na serikali iweje leo utetee chama kinachojinadi cha demokrasia kufukuza chombo cha habari kisichoripoti kinavyotaka.

Kiongozi anayefukuza chombo cha habari hadharani keshi ukimpa Dola si ataishia kuwachoma moto waandishi watakaoenda kinyume na matakwa yake?
 
Kama hawawezi kutangaza hivyo unavyosema TBC walienda kufanya nini mkutanoni
 
Wewe jamaa mahaba yako kwa ccm yanakufanya kuwa taahira. Mbona bwana yule huwa hadi anatukana kabisa, kuita wateule wake wapumbavu lakini huwa hawazimi sauti wala kufanya walichofanya leo? Acha kutetea ujinga.
Na wewe mahaba yako kwa Lissu yasi-overcloud thinking capacity yako, ina maana kisa CCM kuna mtu huwa anafànya hivo hicho ndio kina justify CHADEMA pia kufanya hicho hicho?

Kama ni hivo basi CHADEMA pia ikipata nchi itaanza kuua wapinzani wake kisa CCM inafanya hivo, naamini uwezo wako wa kufikiri ni zaidi ya ulichokiandika, usijidhalilishe.
 
Nitailoga TBC
 

..nilidhani TBC ndio waliokuwa wanaminya habari.

..au wewe mwenzangu uliona kitu tofauti?

..Mbowe alikuwa anawataka TBC watangaze habari.

..lakini TBC walikuwa hawataki kutangaza, badala yake wanaminya habari.

..nadhani wa kulaumiwa ni TBC. Na kwa kweli walikuwa ni KERO kubwa haswa kwa sisi watazamaji.
 
Mkuu kwa sheria zetu wewe ukisimama ukasema manbo ambayo yanakiuka amani au yanahatarisha usalama kisha TBC wakakurusha hewani, vyombo vya Dola vitamfuata TBC. Tuelewe hili kwanza.

Pili, Demokrasia gani ya kuamulia chombo kirushe unavyotaka? Ulitaka TBC warushe matangazo kama Mbowe alivyotaka iwe!

Je, Kesho serikali ikivitaka vyombo vyote virushe tu maudhui serikali inayoyataka (jambo ambalo linafanyika mara nyingi) tutaweza kukemea.

Tusiwe na double standards...tualike vyombo vyote vya habari virushe matangazo kwa kadri viwezavyo.

La kuzingatia tu ni wasirushe ambacho hatujakisema. Ila kwa sababu zao ama za sheria wasiporusha baadhi ya vipande tunavyovisema hakuna shida.

Uhuru haupo kwenye kuudai tu...tukumbuke pia kwenye kuutekeleza.
 
Wewe bwekaa lakini ndo washafukuzwa siku nyengine watakua na heshima!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…