Uchaguzi 2020 Hoja fikirishi: CHADEMA kwanini mnadai Uhuru wa Vyombo vya Habari huku mkivinyima haki, kufukuza na kuvidhalilisha!?

Uchaguzi 2020 Hoja fikirishi: CHADEMA kwanini mnadai Uhuru wa Vyombo vya Habari huku mkivinyima haki, kufukuza na kuvidhalilisha!?

Mkuu kwa sheria zetu wewe ukisimama ukasema manbo ambayo yanakiuka amani au yanahatarisha usalama kisha TBC wakakurusha hewani, vyombo vya Dola vitamfuata TBC. Tuelewe hili kwanza.

Pili, Demokrasia gani ya kuamulia chombo kirushe unavyotaka? Ulitaka TBC warushe matangazo kama Mbowe alivyotaka iwe!

Je, Kesho serikali ikivitaka vyombo vyote virushe tu maudhui serikali inayoyataka (jambo ambalo linafanyika mara nyingi) tutaweza kukemea.

Tusiwe na double standards...tualike vyombo vyote vya habari virushe matangazo kwa kadri viwezavyo.

La kuzingatia tu ni wasirushe ambacho hatujakisema. Ila kwa sababu zao ama za sheria wasiporusha baadhi ya vipande tunavyovisema hakuna shida.

Uhuru haupo kwenye kuudai tu...tukumbuke pia kwenye kuutekeleza.

..hicho unachozungumzia wewe ni kufanya editting.

..lakini TBC walikuwa wanafanya kitu kipya kabisa, sijui hata utaita nini.

..kile walichokuwa wanafanya was very UNPROFESSIONAL, nadhani ni afadhali walivyozuiliwa wasiendelee.

..historia ya TBC huko nyuma nayo ilichangia yaliyotokea leo.
 
Lissu kawaharibu Chadema. Lissu anaidharau Tanzania, anadharau rasilimali, tunu, tamaduni zetu kama taifa na mbaya sana anatudharau watanzania!!! Chadema wamemfuata kwenye hili la dharau!
 
Bavicha huwa wanatamba Mbowe ni tajiri tangu enzi za Nyerere lakini kila unapofika uchaguzi Chadema huwa hoi sana kipesa kwenye kampeni!!

Mfano uzinduzi wa kampeni leo ni hovyo kabisa na ni dhahiri chadema hawana pesa.

Je utajiri wa Mbowe una manufaa gani kwa Chadema??
 
Bavicha huwa wanatamba Mbowe ni tajiri tangu enzi za Nyerere lakini kila unapofika uchaguzi Chadema huwa hoi sana kipesa kwenye kampeni!!

Mfano uzinduzi wa kampeni leo ni hovyo kabisa na ni dhahiri chadema hawana pesa.

Je utajiri wa Mbowe una manufaa gani kwa Chadema??
hujasikia mwenyekiti wa tume kasema kwenye kampeni msitumie pesa nyingi
 
Nasikitika kusema kwamba sera hii sasa inakosa mashiko kabisa kwa hiki kilichotokea leo hii.

Ni ngumu sana kuamini watu wanao pigania Uhuru wa vyombo vya habari kushindwa kuwa wavumilivu na kuviacha vyombo hivyo vifanye kazi kwa Uhuru na utashi wao.

Kama kweli CHADEMA inapigania Uhuru wa Vyombo vya Habari basi wangeacha TBC warushe mkutano wao kwa Uhuru bila ya kushinikizwa kufanya hivyo kwa matakwa ya CHADEMA.

Ifahamike kuwa TBC ni chombo Cha habari Cha Taifa hivyo basi hakiwezi kurusha matamko yoyote yenye viashiria vya kueneza Chuki na uvunjifu wa amani. Ni lazima wafanye uchambuzi wa kipi kinayakiwa kiwafikie watanzania sasa matamko ya viongozi wa CHADEMA hayakuwa mazuri.

Mfano ni Tundu Lissu alikuwa akisema haya.
"Kama wanategemea tutajitoa kwenye Uchaguzi huu, hilo wasahau. Kwenye kila mkutano wetu wa kampeni, wananchi nchi nzima muanze mikutano kwa maandamano ya amani kudai wagombea wetu warudishwe bila masharti yoyote. Watanzania msikubali kukaa kimya tena,"

"Tunaziomba Jumuiya za Kimataifa zituunge mkono katika jambo hili la kupigania wagombea wa vyama vya upinzani ambao wameunguliwa kwasababu za kihuni maana jambo hili ni kinyume pia na sheria za kimataifa.."

Rais Magufuli aliwaambia wasimamizi wa Tume ya uchaguzi, ambao ni wateule wake, “Siwezi kuwalipa mishahara mikubwa na magari mazuri, halafu mkatangaze wapinzani kuwa washindi kwenye uchaguzi.” Haya ni matokeo ya maelekezo hayo!



Sasa Chombo Cha habari Cha Taifa hakiwezi kutangaza kauli za namna hiyo popote pale dunia sio kwa Tanzania tu pekee.

Mhe Mbowe alienda mbali zaidi na kusema kuwa hawana haja ya kunadi Ilani ya uchaguzi badala yake wanatakiwa wananchi wakadai haki, alipoanza kudai kuwauliza watu kuwa wangapi wapo tayari kwenda kudai haki ndipo hapo TBC wakakata matangazo walipo rudi hewani mhe Mbowe akawapa dk 15 waondoke kwenye mkutano wao.

Je huu Uhuru wa vyombo vya habari tunao upogania ni upi hapa ikiwa hawataka kuviacha vyombo vya habari vitangaze kulingana na weledi wao ? Kwanini walitaka TBC watangaze kwa matakwa ya CHADEMA tu?.View attachment 1550947

Katika hili CHADEMA mnajiharibia wenyewe.View attachment 1550950

Je hiki walicho kifanya leo CHADEMA hakijawanyima haki watanzania kupata habari? Huu sio ukandamizaji wa vyombo vya habari?
Ndugu yangu chadema na tbc uliwahi ona wapi au wewe c mtanzania hujui.
 
Back
Top Bottom