N'yadikwa you are fighting the wrong enemy..
Hebu acha kujadili mambo haya emotionally. Let argue kwa hoja na kuyatazama mambo ktk uhalisia na ukweli. Hebu acha kutumia mazoea kujadili mambo magumu yanayohitaji utumie akili yako sawasawa ktk kufikiri..
Nakuhakikishia jambo moja ndugu
N'yadikwa..
Kwamba, kwa mfumo wa utawala wa nchi hii hata kama Rev. Josephat Gwajima amue leo kukupa wewe huo unaoitwa "ubunge" bure tu bila hata kupigiwa kura, barabara hiyo hutaijenga leo wala kesho hata kama utaongea bungeni huku ukiwa umevua nguo zako zote, uwe uchi..!
Kwa mfumo wetu wa utawala uliojisimika chini ya "imperial president" mnaweza kujengewa barabara hiyo hata ndani ya mwezi mmoja tu iwapo Rais mwenyewe ataamua hivyo kwa sharti moja tu...
Nalo ni kwa wewe mbunge kumjudia na kulamba miguu yake huyo mtu mwenye cheo cha "u-Rais" na uzini naye spiritually ili akupe utakacho...!
Likely hujanielewa. Ngoja nikupe mfano huu, labda akili yako itafunguka na kuanza kuelewa:
Kule mkoani Manyara kuna jimbo linaitwa Mbulu na mbunge wa sasa ni Flatei Massay wa CCM...
Huko kuna barabara moja very strategic kiuchumi na kiutalii. Inaanzia Karatu [Arusha] - Mbulu - Hydom [Manyara] - inapita Mkalama [Singida] - Meatu [Simiyu] na ina - connect eneo moja linaitwa Kolandoto [Shinyanga] kisha inaelekea Mwanza..
Kwa miaka zaidi ya 20 wabunge wa maeneo haya wamekuwa wakilia bungeni ili ijengwe kwa kiwango cha lami...
Na siku mbili au tatu zilizopita mbunge wa jimbo la Mbulu alizungumza bungeni mpaka akatoa machozi na kubinuka sarakasi ili kumuomba Rais aijenge barabara hiyo, lakini NO BODY CARES..!
Wakati huohuo, kuna maeneo hata yasiyo kipaumbele kabisa barabara zinajengwa, viwanja vya ndege vinajengwa tena bila hata mbunge/wabunge wa maeneo hayo kusema lolote bungeni. Reference ni Chato International Airport..
Why?
Ni kwa sababu kwa ilivyo sasa, practically ubunge hauna maana hiyo unayodhania wewe...
Ubunge ni ajira tu kama ajira nyingine. Na wewe kama unataka kum - knock out Gwajima kwa sbb hii, basi do it right away ili upate ajira hiyo na ukapate posho na marupurupu mengine, ule ushibe kisha usubiri kufa kesho...!
Lakini nakuhakikishia jambo moja, kuwa, kwa mfumo huu wa utawala ambao uko "centralized", pengine wewe ndiye unaweza kuwa mbunge HOPELESS na USIYE NA MAANA kuliko hata Rev. Josephat Gwajima au yule aliyepita Halima Mdee - CHADEMA..
Fungua akili yako. Elewa unataka nini. Kisha dai mfumo mpya wa utawala unaotoa mamlaka ya moja kwa moja kwa watu/wananchi ktk local communities zao i.e kitongoji, kijiji/mtaa, kata, wilaya, mkoa au jimbo kuamua wenyewe juu ya matumizi ya raslimali za maeneo yao kwa maendeleo yao. Hili linawezekana kwa sisi sote kukaa chini na kuamua na kisha ku - document maamuzi yetu kwenye document ya kisheria inayoitwa itwa KATIBA. Ndo kusema madai ya katiba mpya ya wananchi is an undisputed fact kwa sasa...!
But as it is for now, ni kujidanganya ndani ya nafsi yako kudhani kuwa, mbunge anaweza kuwatatulia changamoto za kimaendeleo katika maeneo yenu, kwa mfano eti awajengee barabara..!!