Uchaguzi 2020 Hoja tatu ni kwanini wapinzani hawatoshi kwenye Uchaguzi huu

Hebu tuleteeni na mapungufu ya awamu ya 5 tupime!
Mapungufu yapo

Mfano:

Baadhi ya wateule wa Rais Magufuli hawafanyi kazi zao ipasavyo kwa ubunifu, bidii na uaminifu. Hawa wanapoyumba, wanamyumbisha Rais.

Bado kuna mianya ya ukwepaji wa kodi. Pamoja na ongezeko la makusanyo, bado Kuna mianya ya ukwepaji wa kodi na kuzembea katika kukusanya. Aidha, Kuna muda baadhi ya watumishi wa TRA hawatendi haki na kuchafua kazi nzuri inayofanywa na ndugu Rais

Pamoja na kupungua sana, rushwa bado haijaisha nchini mwetu.

Bado kuna changamoto ya ajira kwa vijana ( hili nitaliandikia panapo uzima). Kuna sehemu vijana tunakosea. Hii sio ishu ya serikali peke yake.

Ndio maana nasisitiza, chagua Magufuli, chagua mbunge na diwani wa CCM ili tuendelee kushughulikia changamoto zilizobaki
 
Hoja zako zote hazina mashiko .Tueleze kwanini NEC imepokea mapingamizi 557, nasikia yamefika hadi 1000 mapingamizi yote hayana mashiko,tueleze pia kama unazijua sheria mpya za uchaguzi 2020 ambapo msajili wa vyama ndiye kiranja mkuu
Ben rafiki yangu, uko nje ya mada. Hukustahili heshima ya kujibiwa, ila nitakujibu.

Mapingamizi yapo kwa mujibu wa sheria. Vyama vyote vinayo haki ya kumwekea mgombea mwingine pingamuzi.

Kwa mfano: pamoja na mambo mengine, sheria inamtaka mgombea aweke picha kwenye fomu zake. Inapotokea mgombea hakuweka na mgombea mwingine akamuwekea pingamizi (kumbuka wagombea wanaruhusiwa kukagua fomu za wagombea wengine). Mgombea asiyeambatanisha picha akienguliwa Kuna uonevu?

Wewe zingatia sababu za kuenguliwa. Baadhi ya wagombea wenu wanakosa umakini kwenye ujazaji was fomu na mchakato mzima wa Uchaguzi
 
Kwani nani alisababisha isifike?
Tigershark, Mimi sijui mengi, ila moja kuu nilijualo ni kuwa treni ziliacha kwenda ila Sasa zinakwenda na mpelekaji ni Rais Magufuli na timu yake. Hilo kwangu na kwa wanaarusha ndio kubwa na la muhimu.

Tunampa Magufuli miaka mitano tena, tunampa Gambo hatamu za uongozi wa jimbo ili aendeleze miradi aliyoiasisi na kuibua mipya kwa Arusha
 
Huwa najiuliza kati ya majimbo yanayoongozwa na CCM VS upinzani ni majimbo yapi yana watu fukara?
Kuna factors nyingi sana zinazipelekea ufukara, ila kubwa ni mindset. Kwenye majimbo fukara,hata ukimfanya Bill gates kuwa mbunge kama wananchi hawapo tayari kutumia fursa walizonazo na zinazoletwa na Serikali yao lazima tu wawe fukara. Ila kama Chadema wangekuwa madarakani tangu uhuru, wao hata nchi wangeiuza hawa jamaa.
 
Bado ninaomba wachangiaji wajikite kwenye hizo hoja tatu. Msitoke nje ya mstari
 
Kuna factors nyingi sana zinazipelekea ufukara, ila kubwa ni mindset. Kwenye majimbo fukara,hata ukimfanya Bill gates kuwa mbunge kama wananchi hawapo tayari kutumia fursa walizonazo na zinazoletwa na Serikali yao lazima tu wawe fukara. Ila kama Chadema wangekuwa madarakani tangu uhuru, wao hata nchi wangeiuza hawa jamaa.
Asante sana Agitator. Nikipata wasaa nitaandika kuhusu ajira kwa vijana. Ingawa serikali inasehemu yake lakini It's about mindset ya wahusika.
 
Watoto wa hao wa Nanyamba na Kyabakari wanasoma bure ili siku moja wapate elimu kubwa ya kuweza kuzipanda mara kwa mara hizo ndege wakienda Ulaya kwa ajili ya kufanya biashara kubwa.

Akili zinazoangalia mbali huwa zinahoja masuala kwa kina.
IMG-20200903-WA0036.jpg
 
Ben rafiki yangu, uko nje ya mada. Hukustahili heshima ya kujibiwa, ila nitakujibu.

Mapingamizi yapo kwa mujibu wa sheria. Vyama vyote vinayo haki ya kumwekea mgombea mwingine pingamuzi.

Kwa mfano: pamoja na mambo mengine, sheria inamtaka mgombea aweke picha kwenye fomu zake. Inapotokea mgombea hakuweka na mgombea mwingine akamuwekea pingamizi (kumbuka wagombea wanaruhusiwa kukagua fomu za wagombea wengine). Mgombea asiyeambatanisha picha akienguliwa Kuna uonevu?

Wewe zingatia sababu za kuenguliwa. Baadhi ya wagombea wenu wanakosa umakini kwenye ujazaji was fomu na mchakato mzima wa Uchaguzi
Umeongelea kuhusu kuungana sheria inavitaka vyama vinavyotaka kuungana miezi 3 kabla vieleze ni vitugani watavisimamia kwenye huo muungano kwa msajili wa vyama vya sisasa, sheria imempa mamlaka msajili wa vyama vya siasa kukubali ama kukataa mapenekezo hayo. Msajli atatoa majibu kwa muda unao mpendeza yeye hata kama ni siku 2 kabla ya kuanza mchakato huo
 
Sasa vyama vyenu si vilipaswa kufuata na kutii sheria?
 
Wapinzani wanajichangamsha kama wanavyojichangamsha siku zote,yaan ni hovyo kabisa hakuna kitu.
 
Kuna factors nyingi sana zinazipelekea ufukara, ila kubwa ni mindset. Kwenye majimbo fukara,hata ukimfanya Bill gates kuwa mbunge kama wananchi hawapo tayari kutumia fursa walizonazo na zinazoletwa na Serikali yao lazima tu wawe fukara. Ila kama Chadema wangekuwa madarakani tangu uhuru, wao hata nchi wangeiuza hawa jamaa.
Kwanini waendelee kuichagua CCM muda wote?
 
Wanajamvi,

Ninaomba nilete kwenu hoja tatu ni kwanini tusichague Upinzani. Hoja hizo ni Kama ifuatavyo:

1. Njia za kushughulikia janga la korona
2. Kushindwa kuwa mfano kwenye chama na majimbo
3. Kushindwa kuungana

Njia za kushughulikia janga la Corona

Wakati serikali ikija na mpango mkakati wa kushughulikia janga la korona, wapinzani nao walikuja na mpango wao. Serikali ilisisitiza kufuata masharti lakini watu walikuwa huru kufanya shughuli zao (there was no curfews). Kwa upande wao, wapinzani (hasa CHADEMA na ACT - Wazalendo), walisisitiza kufuata masharti lakini walitaka watu wafungiwe ndani (country lockdown).

Njia ya serikali ya CCM chini ya Rais Magufuli (akisaidiwa kwa Karibu na waziri Ummy Mwalimu) iliunganisha mambo mawili; ubunifu wa kisayansi uliozingatia mazingira yetu na kuweka imani kubwa kwa Mungu. Wapinzani walitaka kufanya "copying and pasting" pasipo kuzingatia mazingira yetu.

Unamfungiaje mtu ambaye mlo wake unategemea yeye kutoka? Watu si wangekufa njaa? CCM waliona hilo. Wananchi walipokea kwa furaha maamuzi ya Rais maana yalijaa matumaini, yalitoa Faraja na yalituvusha.

Rais Magufuli na serikali yake hawakulala. Walifanya majaribio, waliagiza NIMR na matabibu watafute suluhu. Mengi aliyoyafanya Rais Magufuli yalikuja kuthibitika baadae kuwa ni kweli na hakika ingawa wakati akiyasema alishambuliwa na maadui wa ndani na nje na kuitwa majina your mabaya.

Wakati Rais Magufuli na CCM wakichukua hatua hizo, wapinzani walikebehi, kubeza na kulaani. Walitutaka tusubiri kuokota maiti. Walienda mbali zaidi wakachukua posho halafu wakatokomea kusikojulikana, wenyewe wakiita "karantini ya kishua" huku wapiga kura wao wakihangaika kutafuta riziki zao.

CHADEMA walienda mbali zaidi kwa kutoa onyo Kali pamoja na kuwafukuza uanachama wabunge waliokataa mpango huo. Inashangaza wanajiita chama cha demokrasia.

Kwa hili tuu la ugonjwa wa Corona, ilitosha kabisa kuwakataa wapinzani na kuipa CCM kura zote.

Kushindwa kuwa mfano kwenye chama na majimbo

Ukipata nafasi unatakiwa uitumie vizuri. Wabunge wa Upinzani walitakiwa wajiongeze kwa kufanya kazi kwa bidii Sana, ubunifu wa hali ya juu na uadilifu usiotiliwa shaka. Vyama vyao vilitakiwa kuongozwa Kidemokrasia. Hii ingewasaidia sana kuwathibitishia watanzania kuwa hata wakipewa nchi wanaweza. Wanasema "Charity begins at home".

Kinyume chake, chamani na majimboni, ni "business as usual". Siku zote mchepuko unajitahidi kumfunika madhahausi. Wapinzani kwa hili mmeshindwa pakubwa. Mmeshindwa kuthibitisha kuwa mnaweza kuwa mbadala wa CCM. Endeleeni kujiandaa kwa sasa hamtoshi.

Kushindwa kuungana

Wapinzani kushindwa kuungana hasa mnapomkabili mgombea wa aina ya Rais Magufuli ni udhaifu mkubwa sana. Ni wazi kuwa hamuaminiani. Zitto Zuberi Ruyagwa Kabwe aliahidi ahadi hii hewa. Kama nyie binafsi hamuaminiani, sisi wananchi wa kawaida tutawaaminije?. CCM itawapiga kipigo cha mbwa koko mwaka huu. Hamna rangi mtaacha kuona.

Amani Msumari
Tanga
Hoja pumba kabisa. Asilimia kubwa ya majibu yanapatikana katika mahojiano ya TL na ITV jana. Kaisikilize.
 
Tafuta kiswali kizuri huo utoto wako usiuite hoja.
Labda kama hujui maana ya hoja
 
Kwanini waendelee kuichagua CCM muda wote?
Nimeipenda hi. Kuna mambo mawili hapo kwa harakaharaka.
1. Wanatumia uhuru wao kuamua.
2. Nimefurahi umesema kuchagua. Waambie wenzako, hatuibi kura, tunachaguliwa Kidemokrasia
 
Tafuta kiswali kizuri huo utoto wako usiuite hoja.
Labda kama hujui maana ya hoja
Natoka hapa, usihangaike kutoka hapo. Njomba Nchumali nachema, ukichimama nchale, ukikaa nchale, ukitoka hapo nchale vilevile bwana wewe.
 
Tigershark, Mimi sijui mengi, ila moja kuu nilijualo ni kuwa treni ziliacha kwenda ila Sasa zinakwenda na mpelekaji ni Rais Magufuli na timu yake. Hilo kwangu na kwa wanaarusha ndio kubwa na la muhimu.

Tunampa Magufuli miaka mitano tena, tunampa Gambo hatamu za uongozi wa jimbo ili aendeleze miradi aliyoiasisi na kuibua mipya kwa Arusha
Sema wewe wampa!Wengine tuna mitazamo tofauti!Tunataka ifike mahali chama kikishindwa kudeliver kiondoke madarakani na hapo ndio uwajibikaji wa kweli utakapopatikana kwa wale tunaowakabidhi nchi!Lakini ikiendelea kuwa mgombea wa CCM lazima ashinde,tutaendelea na hizi ngonjera miaka nenda rudi!Huyu anaua hichi mwingine anakuja kurudisha na mapambio juu huku na yeye ameua la kwake!So Magufuli tumeona uwezo wake,nadhani hana jipya zaidi ya flyover na barabara!Sekta ambazo ndio uti wa mgongo kwa maisha ya watanzania hazina kipaumbele kwake!Uchumi wa mtu mmoja mmoja sio muhimu kwake!
JPM out,tuyape mawazo mbadala fursa tuone baada ya miaka 5 watatufanyia yapi!
Kuendelea kuamini hakuna mtu wa kuongoza nchi zaidi ya Magufuli ni ujinga!

Yeye mwenyewe anasema tusichague upinzani hata kama anafaa,sasa hapo anatuambia nini wananchi?
 
Back
Top Bottom