Unajua mkuu Mleta mada hebu jifunze kutofautisha tamaa za mwili na mambo ya rohoni.
Usije ukadhani BIBLIA TAKATIFU Iko tu hapa Kwa uwazi.
Ukweli ni kwamba kuna mamilioni ya watu waliuwawa, kifo Cha kikatili kabisa Kwa sababu walikataa kuukana uKristo na wengine waliuwawa wakikatazwa kusoma BIBLIA TAKATIFU, usijifariji mkuu, wao wameshaiua Ile hisi asili ya kukushtaki mwenyewe.
Ngoja nikupe mfano, mara Yako ya kwanza kabisa ikiwa ulifanya mapenzi bila utaratibu wa dini Yako moyo wako ulijiskiaje?
Sasa ukiendelea kuipuuza hiyo sauti ya ndani unaendelea kuikandamiza Kisha inakufa kabisa ndipo unakuta umefikia kiwango Cha uhayawani mpaka waweza Fanya mapenzi hadharani.
Kwani si Hadi miaka ya 1980 ikiwa sikosei Marekani waliutambua ushoga kama ugonjwa wa akili?
Miaka kadhaa mbele wanasemaje kuhusu jambo Hilo?
Mbingu ipo moto upo, Ninaamini ila Kwa kukazia niliwahi kuwa na mchawi karibu bila kumjua akawa ananambia, Kanisani utakuta ni mtu Mmoja au wawili tu katika Kanisa lote ndio Wacha Mungu wa kweli...
Ni hivi, wanajua wengi wataenda motoni, ndio sababu hawaangaiki, tofauti na zamani...