Ritz
JF-Expert Member
- Jan 1, 2011
- 57,035
- 46,479
Wanakumbi.
Hoja ya Jaji Mstaafu Warioba Kuhusu Vifo vya Oktoba 29 ni Uongo na Uchochezi wa Kisiasa.
Katika Vita ya Kagera (1978–1979), takwimu zinazokubalika kitaifa zinaonesha wazi kuwa
Wanajeshi wa Tanzania waliopoteza maisha walikuwa 373
Askari wa Kikosi cha Ukombozi cha Uganda (UNLA) walipoteza takribani 150 kina M7 hawa
Raia wa Tanzania waliouawa na uvamizi wa Idi Amin walikuwa takribani 1,500
Hizi ni takwimu za vita halisi, vita ya wazi dhidi ya adui wa nje.
Kwa mantiki hiyo, kauli ya Jaji Mstaafu Joseph Warioba kudai kuwa waliokufa kwenye machafuko na jaribio la mapinduzi ya tarehe 29 Oktoba ni wengi kuliko Vita ya Kagera ni ya uongo mtupu, ya kizushi, na ya uchochezi wa kisiasa.
Ni jambo linalojulikana wazi kuwa Warioba ana chuki binafsi dhidi ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na amekuwa mshabiki wa CHADEMA kwa njia ya kificho,
Kauli yake si ya haki, si ya kitaifa, bali ni statement ya kisiasa inayobeba ajenda za CHADEMA.
Serikali tayari imeunda Tume ya Kuchunguza Jaribio la Mapinduzi lililofeli.
Kama kweli Warioba ana takwimu za vifo anazodai, njia sahihi ni kuziwasilisha mbele ya tume, si kuzitupa hadharani bila ushahidi kwa lengo la kuchochea hisia na kuvuruga amani ya taifa.
Cha kushangaza zaidi, hata magaidi wa kisiasa waliopanga na kutekeleza vurugu hizo wameshindwa kutoa idadi hiyo wanayodai. Walichobaki nacho ni
Orodha za majina zilizojirudia (duplication)
Majina ya watu waliopo mahabusu au hai kabisa
Hakuna uthibitisho wowote wa idadi hiyo kubwa wanayodai.
Ni muhimu kufahamu kuwa
Vita ya kawaida ni bora kuliko vita ya ndani ya kiuchumi na kisiasa, kwa sababu katika vita ya wazi unamuona adui wako.
Lakini vita ya kuvizia, uchochezi wa ndani na jaribio la kupindua serikali ni hatari zaidi, kwa kuwa hulenga kulivunja taifa kutoka ndani.
Kwa msingi huo, Warioba hana uhalali wa maadili wala kitaifa kutumia hadhi yake kuchochea chuki dhidi ya CCM na Rais Samia kwa maslahi binafsi ya kisiasa.
Aache uchochezi. Taifa ni kubwa kuliko chuki binafsi.