Hoja ya Spika Ndugai: Nitawafukuzaje wabunge ambao Rufaa zao hazijasikilizwa na Baraza kuu kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA?

comte soma hapo👆👆
 
Hivi mfungwa akikata rufa snatolewa jela hadi rufaa yaje ipite au anakuwa jela hadi hukumu?
 
Ndigai ni hopeless kabisa. Arudishwe tu hospitali

CHADEMA wanasema hawajawahi kuteua wabunge wa viti maalum, yeye anaongelea rufaa ya uwanachama. Hivi huyu spika kama anashindwa kujua hata hoja inayojadiliwa, kweli bado ana akili timamu?
 
lissu alikuwa anajifanya kuwa kila mtu anajuwa kuwa anaumwa kumbe akasahau kuwa taarifa ya maandishi lazima halafu akawa anadanganya bado anaumwa huku anaendelea kuzurura ulaya na kuichafua nchi huyo mhuni
Hivi Lisu amewahi kuichafua nchi? Magufuli siyo nchi. Ndiyo maana ameondoka, lakini Tanzania inasonga mbele, tena kwa ubora zaidi.
 
Hao chadema wako very very selfish Yani wew mwanaume unapigania mwanamke afukuzwe kazi yake kisa wew huna that's very foolishness and stupidity, Spika kawajibu kwa hoja sana sana huwezi tu kumfukuza kazi mtu hivi hivi bila a fair justice never..
Umetoa hoja kipunguani. Hao wabunge waliteuliwa na nani? CHADEMA hawakuwateua.

CCM wana uhuru wa kuwapa ubunge hao akina mama kama walivyofanya majimboni, lakini wasiwaite kuwa ni wabunge kupitia CHADEMA. WANAWEZA KUITWA, WABUNGE WA MAREHEMU MAGUFULI.
 
Prove what? Wao walichosema ni kuwa hawajapeleka fomu au barua yeyote NEC ya kuwateua wakina Halima. Aliyetakiwa ku initiate hiyo investigation ni NEC na Spika kama watu ambao wamedanganywa...
Nadhani tutakwamia hapa until October 2025...
 
Aida, kwa mujibu wa tume alishinda uchaguzi na amefata taratibu zote kuwa mbunge. Chadema walieleza wazi kuwa hawawezi kumzuia akitaka kuapa, na uki
Aida alishinda uchaguzi upi? ule ule haramu ila yeye ni sawa kuingia bungeni na si sawa kupeleka wabunge 19? Double standards mkuu na akina NEC/Bunge wanapita humohumo.
 
Mfano wa kijinga- itisheni baraza kesi iishe mnaogopa nini?
Nani anawaogopa ? Labda Ndugai ambae yawezekana KUNA SIRI wanafichiana. Waliitwa Kamati kuu hawakutokea
 
Nani anawaogopa ? Labda Ndugai ambae yawezekana KUNA SIRI wanafichiana. Waliitwa Kamati kuu hawakutokea
Hivi kinachowauna ni nini maana hamuwalipi mishahara na ubunge haumtaki au mnataka Mbowe ndiye ashike nafasi ya Mdee bungeni
 
Aida alishinda uchaguzi upi? ule ule haramu ila yeye ni sawa kuingia bungeni na si sawa kupeleka wabunge 19? Double standards mkuu na akina NEC/Bunge wanapita humohumo.
Dah mkuu mbona hatuelewani jambo dogo sana, Aida anaweza kukataa ubunge yeye mwenyewe, chama kiliishia kwenye kumpitisha kuwa mgombea unless kuwe na allegations ambazo kwa mujibu wa katiba ya chama adhabu yake ni kuvuliwa uanachama.

Sasa Chadema watamvua uanachama kwa hoja zipi? Huyu labda kwa next time wasimpitishe ndani ya chama kugombea ila umvue uanachama sababu ye kashinda/kashindishwa? Hapo CDM hawana cha kumfanya na ndio maana wamekaa kimya, in short wameamua kukubaliana kutokubaliana naye.
 
Elimu unayo ikosa hapa ni ya kwa nini kuna rufaa????
Ukikata rufaa ni kwamba umehukumiwa tayari lakini wewe ukubaliani na hukumu hiyo igawa unaitumikia hadi hapo tufaa itakaposikilizwa!!!!!!!!
Akina COVID - 19 walipokea hukumu yao ila hawakuridhika na wakakata rufaa.
Tumeshuhudia Ndugai akifukuza wabunge na kutamka kuwa kama hawajaridhika nenda ukakate rufaa huku akiwaweka nje hadi rufaa zao zitakapo sikilizwa.
That being said it is obvious Ndugai ana special agenda na COVD - 19 nothing else.
 
Nadhani tutakwamia hapa until October 2025...

Sidhani.
The situation is untenable and there has to be some movement. Serikali haitakubali kuonekana kama ina disregard Katiba kwa sababu ita impact uwezo wake wa kuvutia pesa nzito tunazohitaji za budget support na investment.
Ndio maana nasema mpira uko kwao. Spika ataambiwa alimalize tu. Kumbuka Rais ni Mwenyekiti wake na theoretically ana uwezo wakushawishi mwanachama yeyote kuvuliwa uanachama.

Amandla....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…