Hoja ya Spika Ndugai: Nitawafukuzaje wabunge ambao Rufaa zao hazijasikilizwa na Baraza kuu kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA?

Hoja ya Spika Ndugai: Nitawafukuzaje wabunge ambao Rufaa zao hazijasikilizwa na Baraza kuu kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA?

Dah mkuu mbona hatuelewani jambo dogo sana, Aida anaweza kukataa ubunge yeye mwenyewe, chama kiliishia kwenye kumpitisha kuwa mgombea unless kuwe na allegations ambazo kwa mujibu wa katiba ya chama adhabu yake ni kuvuliwa uanachama.
Kaka tunaelewana vizuri. Hoja yangu ilikuwa kwamba hatuwezi kukubali kupeleka wabunge wa viti maalumu kwani "hiyo itakuwa ni sawa na kubariki ile haramu ya uchaguzi". Swali likawa sasa Aida anaingiaje mule kwa uchaguzi haramu?

Ila nimekusoma vyema. Ni kweli kwamba CHADEMA haina la kumfanya Aida, imekubali kutokukubaliana nae bila kelele na kumfukuza kwa kuwa tu amepishana misimamo na viongozi itakuwa kumuonea sana na inaweza kuleta madhara zaidi
 
Me si mtaalam wa sheria ila nahisi kama kuna jambo tunajichanganya. Nadhani si tu kwamba kitendo cha we kukata rufaa kinakurejeshea haki.

Ninavyo elewa mimi (niko tayari kusahihishwa) ni kuwa hadi rufaa yako ikubaliwe kusikilizwa baada ya kuonekana kuna hoja za msingi kisheria zinazoweza kutengua hukumu/maamuzi ya awali. Nadhani na Mkaruka pia ndiyo hoja yake hii.

Kwa hii hata kama mtu alisha hukumiwa nadhani kuna kitu wanaita 'Bail Pending Appeal' ambapo mshitakiwa anaweza pewa dhamana wakati rufaa yake inasikilizwa baada ya hukumu ya awali kumtia jela.

Sasa hawa covid-19 nadhani hoja yao ni kuwa hawakupewa haki ya kusikilizwa na CC ya chama kitu ambacho si kweli, waliitwa na hawakutokea.

Na pia katiba ya chama inaruhusu kufanya maamuzi kwa jambo la dharura, na issue ya covid-19 ilikuwa na dharura ndani yake i.e kuzuia wasiapishwe kuwa wabunge baada ya ile 'forgery'.
Pamoja kwamba mimi ni mshabiki wa Chadema lakini nafikiri kwenye hii case chadema wameacha matobo ambayo wanaweza kupigwa mawe.

Ni kama kwenye ile ishu ya CUF wakati Profesa Lipumba amejivua uenyekiti alienda akaaa huko then baada ya miezi mingi akaja na akarudi kuwa mwenyekiti.

Sababu ni kubwa ni kwamba wakina Maalim Sefu na Mtatiro hawakufanya mambo kwa kufuata taratibu za katiba yao kwa mtu kujiuzulu uenyekiti. Hawakutarajia ya mbeleni.

Ishu ilikuwa ni ile barua idhibitishwe na mkutano mkuu nafikiri. Hawakuwahi kufanya hivyo na Lipumba akalitumia hilo tobo kwa back up ya state (government) kurudi kwenye uenyekiti.

Somo hapo juu ni kutokufuta mambo kwa utaratibu.

Hata hii case ya chadema japokuwa i wazi kwamba spika hawapendi chadema lakini wameacha matobo kwa spika huyo huyo kuwapiga nayo.

Katiba ya chadema inaruhusu mwanachama kukata rufaa kwa baraza kuu baada ya kutoridhika na maamuzi ya kamati kuu. Haya kamanda hebu nipe sababu za mpaka leo ni kwa nini chadema hawajasiliza rufaa hiyo?

Rufaa ingemaliza ukakasi mwingi kwenye hili jambo kama vile haki ya kusilizwa (kumbuka na hawa covid pia walitoa sababu ni kwa nini hawakwenda kusilizwa walipoitwa) na zinaweza kuwa za msingi kwa upande.

Conclusively mimi naamini covid 19, chadema na spika kila mmoja ana matatizo yake lakini yana uzito (weight) tofauti tofauti.
 
Spika ataambiwa alimalize tu. Kumbuka Rais ni Mwenyekiti wake na theoretically ana uwezo wakushawishi mwanachama yeyote kuvuliwa uanachama.

Amandla....
This is a wish and I hope it prevails. Kimsingi unaweza kuwa sahihi na ndio maana Speaker ameanza kutoka kijanjajanja na kujifanya kutoa maelekezo ya nini kifanyike ili na yeye aweze kuchukua hatua.

Let's wait and see kwa sababu a week is a very long time in politics.
 
Kwa nini CHADEMA wasiende Mahakamani kwa hoja yao kuwa Wabunge hao 19 hawakuteuliwa na Chama?. Short and clear.
 
chadema huwa mnakurupuka, ndio maana hawa jamaa huwa wanawashinda kwa hoja tu.
 
Aida alishinda uchaguzi upi? ule ule haramu ila yeye ni sawa kuingia bungeni na si sawa kupeleka wabunge 19? Double standards mkuu na akina NEC/Bunge wanapita humohumo.
Unalinganisha machungwa na apples. Aidan alitangazwa ameshinda na NEC na alikuwa na kila haki ya kuapishwa. Wakina Halima hawakuteuliwa na chama chao kwa hiyo hawakuwa na haki ya kuapishwa. Chadema wakimfukuza Aidan na madiwani wao watawakwaza wapiga kura wao ambao wanaamini kuwa walipambana vya kutosha kuhakikisha chaguo zao zinatangazwa. Chadema wataweza ku spin na kusema kuwa Aidan na madiwani ni sehemu ndogo tu ya stahili yao.

Wakina Halima hawana jimbo ambalo waliloshinda hivyo hamna hatari ya kuwakwaza wapiga kura wao. Mbaya zaidi kwao ni kuwa wanaonekana ni wasaliti ambao wamewatelekeza wapiga kura wao ambao wameumizwa katika kuwatetea. Matiko amewasemea baadhi lakini sidhani kama watu wake watamuelewa kwa sababu katika hali aliyonayo hawezi hata kwenda kuwatembelea wakiwa mahabusu. Na kwenye jimbo lao kubwa la BAWACHA ndio kabisa hawana mpango nao.

Mimi bado naamini kwa dhati wakina Halima sio wasaliti bali ni watu walikosea hesabu. Hawezi kabisa kuimba wimbo nzuri ugenini. Sitashangaa wakijiuzuru na kuomba msamaha kwenye chama chao. Wale ni wapiganaji na hapo walipo nafsi zao zinawasuta. Naamini wakiomba msamaha watakubaliwa lakini watarudi kama wanachama wa kawaida tu.

Amandla...
 
Hoja kuu sio kufukuzwa. CHADEMA wanadai hawajawateua hao wabunge kupitia vikao vyao vya kikatiba. Hapo Mh Dugai mbona anapakwepa? Kufukuzwa likikuwa ni zao la kukiuka utaratibu za chama.

Chama chao kimesema hakijawateua kwa kuwa hakuna vikao vilivyokaa. Mbona hakikusikilizwa? Vikao vya rufaa ndio muhimu sasa?

Hata kama utaratibu wa kuwafukuza haukufuatwa, lakini hilo la kuteuliwa na vikao ama la ni factual issue. Kwa hivyo hoja kuu ni kuwa hawakuteuliwa na Chadema kama sheria inavyotaka, hiyo ya kutokuwa wanachama wa chama cha siasa ni nyongeza ambayo haina athari kwenye hoja kuu.

Pathetic!
Shida chadema hawajitambui. Mwenyekiti form four failure, Katibu mkuu form six failure.

Spika huwa anaepelekewa majina na tume ya uchaguzi kuwa hawa ndio wabunge wa chama fulani. Hivyo Spika huwatambua kupitia utambulisho wa Tume ya Uchaguzi.

Hivyo kumuandikia Spika ni kupoteza muda kwani yeye mamlaka anayoitambua ya kumtambulishia wabunge ni Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Na hii ndio shida ya viongozi waliofeli shule.
 
Unalinganisha machungwa na apples. Aidan alitangazwa ameshinda na NEC na alikuwa na kila haki ya kuapishwa. Wakina Halima hawakuteuliwa na chama chao kwa hiyo hawakuwa na haki ya kuapishwa.
Hukuelewa context ya hii comment iliyokuwa ikijibu comment nyingine. Hoja ilikuwa kwamba the common denominator hapa ni process ya Uchaguzi.

Kama hatuutambui, then tunakataa mazao yote ya process ile, including ushindi wa Aidah pamoja na kura alizopewa Lissu (ruzuku).

Kama ni halali Aida kwenda Bungeni, then ni halali pia kupeleka wabunge wa viti maalumu pamoja na kuchukua ruzuku. Kwenye process ya nani aende na anaendaje ndipo shida ilipo.
 
Shida chadema hawajitambui. Mwenyekiti form four failure, Katibu mkuu form six failure.

Spika huwa anaepelekewa majina na tume ya uchaguzi kuwa hawa ndio wabunge wa chama fulani. Hivyo Spika huwatambua kupitia utambulisho wa Tume ya Uchaguzi.

Hivyo kumuandikia Spika ni kupoteza muda kwani yeye mamlaka anayoitambua ya kumtambulishia wabunge ni Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Na hii ndio shida ya viongozi waliofeli shule.
Anairbua rufaa!?
 
Spika wa bunge mh Job Ndugai hana tatizo na wabunge wa viti maalumu wa Chadema akina Halima Mdee na wenzake bali anachotaka ni utaratibu wa natural justice kufuatwa.

Kwa mujibu wa katiba ya Chadema Baraza kuu ndio lenye maamuzi ya mwisho ya kumvua mtu uanachama endapo hajaridhika na utaratibu wa awali.

Anachohoji Spika Ndugai ni kama wabunge hao akina Halima Mdee walipewa fursa ya kusikilizwa na kama ndio ameomba mihtasari ya vikao husika ili ajiridhishe na kuchukua maamuzi stahiki.

Ni vema JJ Mnyika akatoka na kuzijibu hoja za Spika Ndugai kwa mujibu wa katiba na siyo blah blah.

Mnyika aseme tu kwanini anasita kuitisha kikao cha baraza kuu ili kukata mzizi wa fitina?

Pia J J Mnyika aufahamishe Umma iwapo wabunge wote 19 hawakuridhika na maamuzi ya kamati kuu hivyo walikata rufaa au kuna baadhi waliridhika na maamuzi hayo kama alivyokiri mjumbe wa kamati kuu mh Jesca Kishoa.

Hili swala linatutia doa kama taifa ni vema likamalizwa sasa.

Tusisahau kufuatilia hotuba ya Rais Samia bungeni leo.

Kazi Iendelee!
Wale wa CUF ya mwalimu walikata rufaa wapi?
Je ilisubiriwa rufaa yao iamuliwe kwanza au?
Acheni ujinga nyie watu
 
Hukuelewa context ya hii comment iliyokuwa ikijibu comment nyingine. Hoja ilikuwa kwamba the common denominator hapa ni process ya Uchaguzi.

Kama hatuutambui, then tunakataa mazao yote ya process ile, including ushindi wa Aidah pamoja na kura alizopewa Lissu (ruzuku).

Kama ni halali Aida kwenda Bungeni, then ni halali pia kupeleka wabunge wa viti maalumu pamoja na kuchukua ruzuku. Kwenye process ya nani aende na anaendaje ndipo shida ilipo.
Mimi nadhani ultimately Chadema wangepeleka wabunge 19 bungeni. Uko sahihi kuwa ingewawia ngumu kukataa kuwapeleka kwa sababu ya kutotambua uchaguzi na kumwacha Aida na madiwani waendelee kushiriki. Kama chama, aidha hiyo ruzuku itasaidia katika kuhakikisha uhai wao. Wataweza kushiriki under protest bila kuutambua uchaguzi katika ujumla wake.

Wakina Halima wangevumilia wangerudi bungeni na heshima zao intact. Sasa hivi hamna jinsi Chadema watawapeleka bungeni hata kama watawasamehe utovu wao wa nidhamu.

Amandla...
 
Wakati wanamvua Lissu ubunge 'principles of natural justice' ilikuwa bado haija asisiwa?
hajawahi peleka hata medical report bungeni akataka tu spika aamini kuwa anaumwa!!! Bila documentary evidence alitaka spika afanyaje? kwa nini akina mbowr walikaa nairobi mwezi mzima kwa kujitia wanauguza wakati wao sio madaktari wala manesi kwa nini hawakupeleka medical report kwa spika?
 
Shida chadema hawajitambui. Mwenyekiti form four failure, Katibu mkuu form six failure.

Spika huwa anaepelekewa majina na tume ya uchaguzi kuwa hawa ndio wabunge wa chama fulani. Hivyo Spika huwatambua kupitia utambulisho wa Tume ya Uchaguzi.

Hivyo kumuandikia Spika ni kupoteza muda kwani yeye mamlaka anayoitambua ya kumtambulishia wabunge ni Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Na hii ndio shida ya viongozi waliofeli shule.
Bahati mbaya track record ya viongozi walioenda shule sio nzuri. Ndio maana wakina Musukuma wanawabeza.

Chadema kumwandikia Spika ni sahihi kwa sababu yeye ndie mwenye mamlaka ya kuapisha na sio NEC. Vyama vyote vilivyotimua wabunge wao ( pamoja na CCM) walimwandikia kumpa taarifa halafu yeye ndio anaipa taarifa NEC kuwa nafasi iko wazi. Chadema kuiandikia NEC ndio kungempa sababu ya kusema hana taarifa ya kufukuzwa kwao.

Mwisho, usipende kutumia lugha za kejeli kwa wanachama wa vyama vingine maana utamfanya Nyalandu aonekane muongo aliposema chama chako kina lugha ya staha.

Amandla...
 
Katiba ya chadema inaruhusu mwanachama kukata rufaa kwa baraza kuu baada ya kutoridhika na maamuzi ya kamati kuu. Haya kamanda hebu nipe sababu za mpaka leo ni kwa nini chadema hawajasiliza rufaa hiyo?
Kwenye kwa nini rufaa yao haijasikilizwa hadi leo hata me sifahamu kwa kweli. Of course kwa uhuni unaoendelea hii inaweza kutumika vizuri kama loop hole.

Ukiangalia bunge lilikuwa linakana kupokea barua ya Chadema kuwavua uanachama lakini bunge hilo hilo linakiri kupokea taarifa toka kwa covid-19 kuwa wamekata rufaa ya huo uamuzi, sasa logically unajiuliza wanatambuaje taarifa ya rufaa ambayo umekana kupokea taarifa za hukumu yake.
 
Spika wa bunge mh Job Ndugai hana tatizo na wabunge wa viti maalumu wa Chadema akina Halima Mdee na wenzake bali anachotaka ni utaratibu wa natural justice kufuatwa.

Kwa mujibu wa katiba ya Chadema Baraza kuu ndio lenye maamuzi ya mwisho ya kumvua mtu uanachama endapo hajaridhika na utaratibu wa awali.

Anachohoji Spika Ndugai ni kama wabunge hao akina Halima Mdee walipewa fursa ya kusikilizwa na kama ndio ameomba mihtasari ya vikao husika ili ajiridhishe na kuchukua maamuzi stahiki.

Ni vema JJ Mnyika akatoka na kuzijibu hoja za Spika Ndugai kwa mujibu wa katiba na siyo blah blah.

Mnyika aseme tu kwanini anasita kuitisha kikao cha baraza kuu ili kukata mzizi wa fitina?

Pia J J Mnyika aufahamishe Umma iwapo wabunge wote 19 hawakuridhika na maamuzi ya kamati kuu hivyo walikata rufaa au kuna baadhi waliridhika na maamuzi hayo kama alivyokiri mjumbe wa kamati kuu mh Jesca Kishoa.

Hili swala linatutia doa kama taifa ni vema likamalizwa sasa.

Tusisahau kufuatilia hotuba ya Rais Samia bungeni leo.

Kazi Iendelee!
Baelezee hao comrade, baelezee!
 
Kwenye kwa nini rufaa yao haijasikilizwa hadi leo hata me sifahamu kwa kweli. Of course kwa uhuni unaoendelea hii inaweza kutumika vizuri kama loop hole.

Ukiangalia bunge lilikuwa linakana kupokea barua ya Chadema kuwavua uanachama lakini bunge hilo hilo linakiri kupokea taarifa toka kwa covid-19 kuwa wamekata rufaa ya huo uamuzi, sasa logically unajiuliza wanatambuaje taarifa ya rufaa ambayo umekana kupokea taarifa za hukumu yake.
Mimi nadhani Chadema wanajivuta kusikiliza rufaa kwa sababu watakapoisikiliza tu na uamuzi unaotegemewa ukatolewa, wakata rufaa wataweza kwenda Mahakamani na Mahakama ina mamlaka ya kuzuia utekelezaji wa hukumu yeyote. Kwa maneno mengine, inaweza kusema wakina Halima watabaki kuwa wanachama wa CHADEMA na viongozi wa Bawacha mpaka kesi yao itakapoamuliwa. Wakishindwa hapo wanapanda Mahakama ya Rufaa na mara tayari 2025 na uamuzi bado. Wakina Halima wanajiuzulu Chadema na kujiunga na CCM na wanapewa ubunge wowote wanaoutaka. Mchezo umekwisha. Kwa hii danadana ni vigumu kwa wakina Halima kwenda Mahakamani.

Amandla...
 
Back
Top Bottom