#COVID19 Hoja za Askofu Gwajima zimewaumbua wataalam wetu na waliomuingiza 'mkenge' Rais Samia kwenye chanjo ya Corona

Hakuna wa kuweza kumjibu Gwajima , sababu hzo chanjo ni agenda ya Siri ambayo gwajima yeye mwenyewe anaijua na Raisi anaijua...!! Sema Raisi kabanwa na wala sio maamuz yake hayo ....!!Hana namna , na sote tutachanjwa ni Suala la mda tuu
Point iko hapa kaka.
 
Unamtafutia Gwajima matatizo, hizi nyuzi zikiendelea endelea zinaweza kusababisha avulie ubunge wake.
Hana Cha kupoteza Wala usiogope tulio nyuma yake ni weeeeeengi Sana.

Mimi nishacopy na kupaste sehemu kabisa ili isambae vizuri watanzania wapone.
 
hoja kwamba chanjo ni mpango wa 666 na agenda ya mpinga kristo?
Kwanini mtu akichanjwa anaendelea kuambukiza /kuambukizwa?

Kama chanjo ni kinga, kwanini mtu aliyechanjwa anaendelea kuvaa barakoa?

Kwanini kwenye vaccine form serikali imejitoa kuwajibika endapo mtu aliyechanjwa atapata madhara?

Toa majibu
 
Hatuna wataalamu, tuna wachumia tumbo. Wananchi wamefanywa majuha, jana wataalamu wanasema wazungu hawaaminiki, chanjo haziaminiki. Leo hao hao, akiwemo na Samia wamebadiri wimbo, wananchi mkachanjwe, chanjo ni bora kwa kinga ya corona. Hawana aibu, wanaongea kwenye majukwaa bila kupepesa macho.
 
Sijaona hata kama kuna hoja ya kuumiza mtaalam kichwa.
Ila hii nchi nayo ina vituko? Watu kujitia ujuaji kwenye taaluma za watu; na wanawapata kweli wa kuwapata!
Mi naona Wizara haiwezi jibu hoja za Gwajima kwa sababu moja kuu,kua wao Wizara siyo watengenezaji wa hizo Chanjo,sana sana watamwambia akitaka majibu ya hizo Chanjo aende Google akaulizie!! Na hii ndiyo shida ya copy & paste!!
 
Kwanini mtu akichanjwa anaendelea kuambukiza /kuambukizwa?

Kama chanjo ni kinga, kwanini mtu aliyechanjwa anaendelea kuvaa barakoa?

Kwanini kwenye vaccine form serikali imejitoa kuwajibika endapo mtu aliyechanjwa atapata madhara?

Toa majibu
Usijichoshe na mambo ya kisayansi,
nenda ukajifukize, kula mapapai alafu nenda kajumuike na misukule mingine kwenye godown la Kibwetere, chanjo ni hiari
 
Pongezi kwa ASKOFU kwa Ushindi dhidi ya Watalaamu

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Hata mm sijawahi kupata majibu haya nikaridhika. Tujiulize
Kama kweli Samia kachanja kwanini anavaa barakoa? Yeye ana tofauti gani na mimi ambaye sijachanja? Kuna umuhimu gani wa chanjo kama utaendelea kuchukua tahadhari zile zile?
Mbona hilo limejibiwa sana!Tatizo hamtaki kuelewa au sijui ni kujitia upofu!

Chanjo ni kwa ajili ya kuongeza uwezo wa mwili kupambana na virus wa Covid,waliochanjwa wakiugua wanakuwa na chance kubwa ya kupona na kutokuwa kwenye critical condition kama ambao hawajachanjwa!Kuva barakoa ni kwa ajili kujiepusha kuambikizwa na kuambukiza wengine!
Sasa pima halafu utaona kama uchanje au la hasha!

Hayo ndiyo majibu ya wataalamu waliotengeneza Chanjo!
Kama hujaridhika,usichanje!Full stop
 
Hoja za Gwajima ni kijinga jinga.Asi.kwamishe mama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…