Hoja za Heche zimejaa harufu ya usaliti. Haya yafanyike kabla ya kufanyika maridhiano yoyote yale

Hii ni fake news. Heche hajaongea hivyo.

Mnapata faida gani kuleta habari za uongo? Mnafikiri Watanzania ni wajinga sana na wataamini tu maandiko yenu?
Taarifa sio fake.
Mwananchi wamepost.
 
Matunda ya 2b ya contents creator hivyo uwongo unaoongea kumsifia mfadhili unaoongeza credit huenda na ufadhili zaidi!
Mkuu, uongo upo wapi hapo.

Ameongea Heche, wamepost Mwananchi.
 
Matunda ya 2b ya contents creator hivyo uwongo unaoongea kumsifia mfadhili unaoongeza credit huenda na ufadhili zaidi!
Mjomba, mimi si sehemu ya huo mgao, na tafadhali usinihusishe na huyo muuaji. Tuheshimiane.
 
Yupo sahihi tu, Hawawezi kukaa kwenye maridhiano wakati mwenyekiti wa chama yupo Gerezani.

Na pia wote tunajua TAL akitoka hayo maridhiano hayatakuepo, labda Baadhi ya watu waamue kuwajibika kwa yaliyo tokea Mo29
Uwajibikaji uwe wa kwanza, mambo mengine yatafuata baadaye. Huwezi kukaa kwenye meza iliyojaa damu kufanya maridhiano na wauaji, isipokuwa kama wewe ni mnufaika.
 
Umechukua screenshot out of context na kuifanya ndio taarifa sahihi hiyo inaitwa fake news!! Kwanini hukuweka hapa script nzima?

Yeye alikataa maridhiano na sio kwamba aliweka masharti ili waingie kwa maridhiano.
Mkuu, usiwaamini sana wanasiasa. Tupiganie uwajibikaji kwanza wa wale wote waliohusika na mauaji ya Watanzania tarehe 29 Oktoba, mengine yatafuata baadaye.
 
Poa mkuu 🤣
Maridhiano ya Sasa ni utapeli laZima aliyeuwa Watanganyika awajibishwe., laZima Samuya ajiuzulu, laZima katiba mpya na tume huru ya uchaguzi ipatikane na laZima uchaguzi urudiwe
 
Maridhiano ya Sasa ni utapeli laZima aliyeuwa Watanganyika awajibishwe., laZima Samuya ajiuzulu, laZima katiba mpya na tume huru ya uchaguzi ipatikane na laZima uchaguzi urudiwe
hapo labda tuambulie katiba na tume
- katiba wameahidi

Hayo mengine nani anayatekeleza?
 
Mkuu, usiwaamini sana wanasiasa. Tupiganie uwajibikaji kwanza wa wale wote waliohusika na mauaji ya Watanzania tarehe 29 Oktoba, mengine yatafuata baadaye.

Kuachiliwa kwa TAL na kufunguliwa kwa CHADEMA sio sehemu ya Maridhiano.

Japo kuna Chama kinaona hayo ndo maridhiano yenyewe, kama walivo Fungulia kanisa la askofu.
 
Hili suala sio la chadema ni polis ccm na wananch wasitake kujiweka kimbele mbele
 
Kuachiliwa kwa TAL na kufunguliwa kwa CHADEMA sio sehemu ya Maridhiano.

Japo kuna Chama kinaona hayo ndo maridhiano yenyewe, kama walivo Fungulia kanisa la askofu.
Na hili nimekuwa nikilitafakari sana. Je, CCM wanadhani kuachiliwa kwa Tundu Lissu ndiyo maridhiano? Kwa kweli, haliusiani kabisa. Wakati tukio la tarehe 29 Oktoba lilipotokea, tayari walikuwa wamemshikilia Lissu, na CHADEMA ilikuwa imewekewa vikwazo
 
Heche, tunakufuatilia kwa umakini mkubwa. Hoja zako za maridhiano, kwa mara nyingine tena katika mahojiano Wasafi TV, zinaanza kuonekana kuwa na viashiria vya usaliti kwa Watanzania waliojitokeza kwenye maandamano, na wengine kupoteza maisha tarehe 29 Oktoba. Tunakuangalia kwa makini.
 
Hili suala sio la chadema ni polis ccm na wananch wasitake kujiweka kimbele mbele
Kwa mara nyingine tena, Heche amejitokeza Wasafi na kuiweka CHADEMA kama kipaumbele katika kufikia maridhiano. Hali hii inanifanya nianze kuwa na wasiwasi kuhusu mwelekeo wake katika jambo hili zito.
 
Punguza mihemko msikilize Kwa makini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…