Hoja za Utanganyika na Uzanzibari ni Hoja Muflis za Ujinga wa Ukosefu Elimu ya Uraia. Tuwatoe Ujinga Huu Kwa Elimu ya Uraia au Tuwaache na Ujinga Wao?

Huu ndio umuhimu wa elimu hii, muungano wetu adhimu ni very unique kwasababu kwa kimataifa ni muungano wa union ya nchi mbili kuungana na kuunda nchi moja ya JMT.
Hakuna elimu hapa, kuna ubabaishaji tu. Nitafafanua
Federation ya JMT na Zanzibar, real! and you write with confidence ! Unajua maandiko yatasomwa miaka ijayo!
Kimataifa muungano wetu ni union ya nchi moja tuu ya JMT na Zanzibar kimataifa sio nchi, ni sehemu ya JMT lakini Kitaifa ni muungano wa federation ya nchi mbili, JMT na Zanzibar.
Mkuu una roho ngumu sana, unarudia tu
Matatizo ya Muungano yalianza wakati wa Nyerere , akayaacha. Mwinyi kidogo yamuondoe, Mwl akazuia kiaina.
Huwezi kuniambia kwamba
Jaji Nyalali
Jaji Kisanga
Jaji Warioba
Mzee Shelukindo
Dr Salim
Mzee Butiku
Mzee Malecela

Wote hawa hawakuwa na akili ya kuona 'uniqueness' ya Muungano isipokuwa ni Pascal peke yake
Mkuu you're better than this, hakuna kitu kinaitwa Federation kati ya ''nchi mama na nchi washirika''

Ni kwasababu ya muundo uliopo matatizo hayaishi na sasa yamefikia pabaya sana
Huko CCM kunafukuta na wasipoangalia ipo siku tutaamka hatuna Muungano

Hivi unajua wenye muungano ni akina nani? Wameamka ndiyo maana husikii upande wa pili kwasababu wanajua kinachofuata, dude limeamka . Watanganyika wanataka Tanganyika yao , Wazanzibar wakitaka Muungano wataomba kwasababu Tanganyika has nothing to lose ! nothing
 
Hakuna elimu hapa, kuna ubabaishaji tu. Nitafafanua
Huu ni ukosefu wa shukrani! , ila mimi hata wakosefu wa shukrani ninawashukuru, na hata vitimbakwiri pia ninavishukuru kwasababu ndio motivation ya ututoaji wa elimu hii na leo ni jumatano ni siku ya elimu kwa umma kupitia gazeti la mwananchi na kipindi on channel Ten, japo wewe hausomi na huangalii, lakini wengine wanasoma na kipindi wanaangalia, hivyo kwangu kazi inaendelea
Federation ya JMT na Zanzibar, real! and you write with confidence ! Unajua maandiko yatasomwa miaka ijayo!
waliotunga miungano sio sisi ni wenzetu waliotangulia ndio wakatutungia miungano ama ya unions ama ya federations ,kwa hakuna muungano mwingine wa union na federation at
the same time, then hakuna jina rasmi la muungano wa aina yetu ,tulipaswa kubuni jina la muungano wa aina yetu na kuupa jina la “uniofedera” ambayo ni type mpya ya muungano duniani ambao ni union na federation at the same na kuwataja Nyerere na Karume kuwa ndio wagunduzi wa “uniofedera”
Mkuu una roho ngumu sana, unarudia tu
ni kweli sio tuu nina roho ngumu sana, mimi pia ni mgumu sana, ukisikia mtu ni mwandishi wa habari amedumu kwenye uandishi huu ni mwaka wa 34!, ujue mtu huyo ni mgumu, ana roho ngumu sana
Matatizo ya Muungano yalianza wakati wa Nyerere , akaayaacha. Mwinyi kidogo aondoke Mwl akazuia kiaina.
miungano yote duniani ina changamoto zake na “uniofedera” is no exception!。
Huwezi kuniambia kwamba
Jaji Nyalali
Jaji Kisanga
Jaji Warioba
Mzee Shelukindo
Dr Salimu
Mzee Butiku
Mzee Malecela

Wote hawa hawakuwa na akili ya kuona 'uniqueness' ya Muungano isipokuwa ni Pascal peke yake
binadamu tuko tofauti tofauti na tunauwezo tofauti wa uoni inawezekana wote hao hawana jicho hilo la kuona the uniqueness ya muungano wetu adimu na adhimu. Kuna vitu vingi tuu waliowengi hawakuviona lakini mimi jicho langu likaona na nikaleta humu, mfano mzuri ni ujio wa Magufuli, ni mimi kuna kitu niliona kumhusu JPM na nikaeleza humu tangu ile 2014 Elections 2015 - Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli kuna kitu ni mimi tuu nilikiona na nikakisema.

Baada ya uchaguzi, kabla JPM hajatangazwa mshindi, ni mimi nilisema kitu humu Elections 2015 - If you can't beat them, join them! He is the worst dictator. Let's pray for him! wengine wote hili hawakuliona.
Miaka yake 4 nilisema mengi, ila kuelekea uchaguzi wa 2019/2020 kuna kitu ni mimi tuu nilikuona nikashauri Ombi Maalum, Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa 2020, Uendeshwe kwa Ceteris Peribus, Sio Kwa Mutatis Mutandis. Tutabarikiwa! kwenye ushauri huu niliweka the consequences, ushauri ulipuuzwa, the consequences ikatokea!.

Hivyo nikashauri JPM asigombee, 2020 ampishe Samia, Pascal Mayalla alitabiri mwaka 2017 kuwa Samia atakuwa Rais wa JMT baada ya 2020 hili likatokea.

Nilizungumzia hivi kuhusu DC wa Kinondoni Nimemkubali Sana DC Makonda, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam akawa!.

Kuna sumu fulani ni mimi tuu niliiona ikienezwa na nikashauri Dkt. Shein Mfute Kazi Haraka, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Kabla Hajamwaga Sumu Hii hili lilitekelezwa!.

Hata Job Ndugai nilimshauri Voices from within: Nimesikia sauti, Dr. Tulia Ackson ndiye Spika ajaye! Sauti hiyo imenieleza Ndugai, japo atatamani aendelee lakini...

Kubwa kuliko ni uchaguzi mkuu wa
2025, kama sauti HII ni kweli, then post 2025, tutaheshimiana tuu mbele ya safari,
Mkuu you're better thatn this, hakuna kitu kinaitwa Federation kati ya ''nchi mama na nchi washirika''
miungano ya unions na federations ni facts, huwezi kubisha na muungano wetu ni union na federation is fact you cant denies!
Ni kwasababu ya muundo huo matatizo hayaishi na sasa yamefikia pabaya sana
Huko CCM kunafukuta na wasipoangalia ipo siku tutaamka hatuna Muungano
hili haliwe kutokea kwasababu huu muungano wetu adhimu, tutaulinda kwa gharama yoyote.
Hivi unajua wenye muungano ni akina nani?
muungano ni wa Watanzania.
Wameamka ndiyo maana husikii upande wa pili kwasababu wanajua kinachofuata. dude limeamka .
duh...!
Watanganyika wanataka Tanganyika yao , Wazanzibar wakitaka Muungano wataomba kwasababu Tanganyika has nothing to lose ! nothing
japo ni kweli kuna Watanganyika wenye umri wa miaka 60+, wote ni wastaafu, wameisha jichokea, waliowengi sasa ni Watanzania.
P
 
Kwa upande wangu, sioni hivyo bali ni kutaka kuufanya muungano wetu uwe halisi na wa maana zaidi kuliko ulivyo kwa sasa kufuatia maoni ya Tume ya Warioba. Kama kuwa na maoni hayo ni kuwa na hoja muflisi na za kijinga basi hata maoni yaliyokusanywa na hii tume upande wa Tanzania Bara na Zanzibar ya kuwa na serikali 3 na kutetewa na wajumbe wa tume (licha ya baadhi yao kusema ni waumini wa serikali mbili/moja) yalikuwa muflisi na ya kijinga pia (kwa mantiki hiyo hiyo).
 
Paskali wazo lako ni zuri ila bahati mbaya naona kama unadhani wanaolizungumzia ndio wameuanzisha ubaguzi huu, hapana. Ubaguzi huu umeanzishwa na serikali kwa kushindwa kuwa na serikali moja nchi moja. Paskali ninaamini ulipofunga ndoa na mkeo hapo nyumbani kwenu hamkuweka vyumba viwili kitanda kimoja kila chumba kwa ajili yako na mkeo, naamini mliingia chumba kimoja kitanda kimoja.
Wakati wewe unaamini sisi ni raia wa Tanzania serikali inaamini kuna raia pia wa Zanzibari na serikali yao waliyoipigia kura na wakapewa kitambulisho cha uraia wa Zanzibari ambacho wewe haujapewa, hivyo hauna haki kwenye mambo yao kama usivyokuwa na haki kwenye mambo ya uingereza! Ni hivi karibuni niliona picha ya rais wa Tanzania akionesha kuwa sasa amepewa kutambulisho chake cha uraia wa Zanzibari, sikuelewa hilo kwani sikujua kabla ya hapo alikuwa raia wa wapi.
Nimalize kwa kusema sheria ndiyo chanzo cha ubaguzi uliopo kati ya wazanzibari na wazanzibara, hivyo sisi tusilaumiane kwani tunatekeleza sheria ya muungano bila shuruti.
 
Mtafuteni Askofu Zachary Kakobe anatoa darasa zuri kuhusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Hii shule ya Paskali haileweki!!!
 
Sasa wewe pamoja na umahiri wako unashindwa kuona kama Nyerere katuingiza chaka! Huu ni muungano gani usiyoeleweka nchi kubwa(Tanganyika) yenye watu karibu milioni 60 kutawaliwa na mtu kutoka katika kisiwa kidogo kisichozidi idadi ya watu milioni 2 na kujidanganya eti Rais wa muungano wakati anaitawala Tanganyika peke yake maana kama angekuwa Rais wa muungano angekuwa na madaraka hadi Zanzibar lakini ona pamoja ni Mzanzibar lakini hana mamlaka yoyote huko kwao bali madaraka yake yanaishia Tanganyika tu! Muungano huu ni wa ovyo kuliko Muungano mwingine wowote uliowahi kutokea katika dunia hii!
Sasa mtu kama huyo aliyeisaliti nchi yake kiasi hicho sijui unawezaje kumuona kwamba eti alikuwa sahihi!
 
Hoja hii huibuka rais anapotokea huko visiwani haziibuki kipindi cha urais wa mtu wa huku bara.

Ni hoja ambazo zina msingi wa udini na chuki ndani yake na Hayati Nyerere aliigundua hiyo chuki na akaikemea mapema sana.

Eneo la hekari laki tisa la Tanzania nzima sehemu kubwa yake ni huku nchi kavu huko visiwani ni sawa tu na wilaya moja au mbili za mkoa wa Morogoro au Arusha, kudai haki kabisa na usawa kwa kila kila kitu kwa nchi hizi mbili ni ukosefu tu wa akili pamoja na roho za kuendekeza visasi.
 
Mtu kutoka sehemu kubwa ya muungano kutawala ni haki kabisa tena mlele yote lakini kutoka sehemu ndogo kutawala sio haki!.

Maana ya muungano ni ule upendo wa kujishusha na sio kutanguliza ubinafsi na ukabila unaojaa kila ubaya wa umimi na usisi.
 
Hoja hii huibuka rais anapotokea huko visiwani haziibuki kipindi cha urais wa mtu wa huku bara.

Ni hoja ambazo zina msingi wa udini na chuki ndani yak

Mbona huyu hakuwa wa kutokea Zanzibar, cheti cha uzanzibari amekipata akiwa madarakani! Sijui kama ameukana ubara au anavyo vyote yaani cha uraia wa Tanzania na cha Zanzibar.
Kuhusu udini unataka kutuaminisja kuwa Zanzibar hakuna wakiristu! Hapana wapo japo ni wachache lakini wapo, kwa hoja ya udini ni hoja potofu kwani Kikwete na Mwinyi ni wa bara sijui nao ziliibuka? Ukweli ni kuwa muungano ulifanywa na watu wawili waliojua malengo yao bila kuwashirikisha satu wengine, nihitimishe kwa kihoni nini kinachozuia kuwa na serikali moja ndani ya nchi moja, vinginevyohuko mbele ya ya safari tutakuja sikia Zanzibar inataka kuungana na Komoro, na kutazua mgogoro mwingine.
 
Mtu kutoka sehemu kubwa ya muungano kutawala ni haki kabisa tena mlele yote lakini kutoka sehemu ndogo kutawala sio haki!.

Maana ya muungano ni ule upendo wa kujishusha na sio kutanguliza ubinafsi na ukabila unaojaa kila ubaya wa umimi na usisi.
Japo sijaelewa vizuri ulichoandika lakini niseme tu huu unaoitwa Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar hata haueleweki kwa sababu huyo Rais anayeitwa wa muungano ni Rais wa Tanganyika tu kwa sababu hana mamlaka yoyote Zanzibar, Tena sasa hivi ndiyo kabisa kwa sababu kwa katiba ya zamani ya Zanzibar ilimtaka Rais wa Zanzibar akitaka kuteua au kugawa eneo la kiutawala katika mikoa na wilaya alitakiwa ashauriane na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lakini kwa sasa wamefanya marekebisho ya katiba yao Rais wa Zanzibar halazimiki tena kushauriana na Rais wa JMT, lakini pia bunge likitunga sheria inayotakiwa itumike pande zote mbili za Muungano basi kule Zanzibar sheria hiyo haitoanza kutumika hadi iridhiwe na Baraza la Wawakilishi.
Hata sasa hivi pamoja kwamba Rais aliyopo madarakani ni Mzanzibar lakini hana mamlaka hata ya kumteua afisa mtendaji wa kata kule Zanzibar haijalishi huyo mtu ni Mzanzibar au Mtanganyika lakini anateua Wazanzibar wenzake kwenye mambo yasiyo ya Muungano hata sasa wapo Wazanzibar Wakurugenzi wa halmashauri na Wakuu wa Wilaya huku Tanganyika.
Sasa je Rais kama huyo unawezaje kumuita Rais wa muungano?
Tuseme tu Tanganyika inatawaliwa na Mzanzibar.
 
Huwa najiuliza ujinga wa watu hao wame barikiwaje kuwa na ujinga walio nao?

Huwa najiuliza ni ipi tofauti ya mtanzania na mzambia,mkenya,md.r.c,mmalawi,nakuja kugundua wote Niwa moja

Na pia Ukiangalia mipaka yetu udongo wetu,mimea yetu vyote vinatuambia sisi ni ndugu,sisi damu moja.

Cha ajabu wakati watu wachache wanao tambua mzungu alituganya Nini mpaka akatu tawala na anaendelea kutu tawala kupitia watawala ambao nindugu zetu

Watu hao wakiwa wanawaza kui unganisha Africa kuwa taifa moja ili kuka biriana na neo colonialism kwa maisha ya Sasa na baadae ya Africa

Cha ajabu huku nyuma unamkuta mtu Tena msomi tunae mtegemea anapambana majukwaani kuhakikisha muungano wa Tanzania/Tanganyika na Zanzibar una vunjika" inashangaza kwa kweli

Nabaki najiuliza Nini faida ya elimu kwenye kujikomboa ki fikra?

Tuna paswa kuiona east Africa inakua one nation thein Africa state tuwe na pesa yetu,bank yetu tujikomboe kutoka kwa mikopo yenye mashart magumu ya Hawa I.m.f,wb, nk

Sasa Hawa Hawa wasomi wetu ndio wanao ongoza kuupinga muungano wetu na undugu

Hapo ndipo nachoka kabisa
 
wenye kuumizwa tuko kimya wenye kuogelea neema ya muungano midomo juu, ningekuwa siupendi muungano ningependekeza tuwaachie tu hata miaka mitano waonje upweke na shida ndo waje kwa adabu. jamani muungano una gharama zake ni pamoja na kujishusha kama ambavyo bara imefanya miaka yote.
kama wanaweza kila mmoja achambue mchanga wake katika ule uliochang,anywa 1964 ndo asepe vinginevyo agenda hii ifungwe haina mashiko.
 
Nguruvi3 Soma taratibu umesoma ukiwa na maoni yako na itikadi yako mpaka unapoteza uwezo wako mkubwa wa ujengaji wa hoja. Paskali amesema kuhusu upekee wa muungano wetu kuwa wenyewe ni Union cum federation ndo uadimu wake huo. Amesema Tanganyka ilikuwepo ila ikawa replaced na Tanzania Bara ila Zanzibar ikasalia kwasababu ya jina lake japo pia mara zingine inatumia Tanzania visiwani. Hoja ya msingi ni uadimu na uadhimu wa muungano huu sasa wewe weka hoja kwanini muangano huu sio adimu wala adhim.
 
Mzanzibari asiye na mamlaka ya kuteua yoyote huko kwao Zanzibar!.

Zanzibar haina kiti umoja wa mataifa na muwakilishi kule ni Tanzania. Hayo mengine ni ufahari tu wa kibinadamu kupenda utukufu wa kidunia.
 
Kwa wakati ule Nyerere alikuwa na haki zote za kuishikilia Zanzibar, ilikuwa ni dunia ya vita baridi kati ya magharibi na mashariki. Wakubwa wa magharibi wakampa darasa lililomuingia juu ya suala la ulinzi wa Tanganyika na wepesi wa mashariki kuivamia nch hii kupitia hivyo visiwa viwili.

Leo tunampigia kelele RIP Nyerere kwa kutazama vigezo vya dunia ya leo wakati yeye alitazama vigezo vya wakati ule. Alikuwa na uhalali wa kuja na maamuzi yale kama tulivyo na uhalali wa kuhoji kilichofanyika wakati ule.
 
Upuuzi.
 
Ukiwa mwendawazimu au una matatizo ya akili utasimama na kutetea huu upumbavu unaoitwa muungano, uzuri tunakujua wewe ni chawa pro max uko kwenye juhudi za kupambania teuzi lakini ulipigwa kimavi kibaya Sana hata uimbe pambio kwa kiasi gani hutoboi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…