Hoja za Utanganyika na Uzanzibari ni Hoja Muflis za Ujinga wa Ukosefu Elimu ya Uraia. Tuwatoe Ujinga Huu Kwa Elimu ya Uraia au Tuwaache na Ujinga Wao?

Ukiwa mwendawazimu au una matatizo ya akili itasimama na kutetea huu upumbavu unaoitwa muungano, uzuri tunakujua wewe ni chawa pro max uko kwenye juhudi za kupambania teuzi lakini ulipigwa kimavi kibaya Sana hata uimbe pambio kwa kiasi gani hutoboi
Asante
P
 
Kuna mbunge anasema yeye sio Mtanzania ila ni Mzanzibari wakati Tanzania imetokana na muungano wa nchi mbili Tanganyika na Jamuhuri ya watu wa Zanzibar huyo ni mmoja wa watu waliokosa elimu ya Uraia bunge limtake atengue kauli yake mara Moja.
 
Nguruvi3 Soma taratibu umesoma ukiwa na maoni yako na itikadi yako mpaka unapoteza uwezo wako mkubwa wa ujengaji wa hoja. Paskali amesema kuhusu upekee wa muungano wetu kuwa wenyewe ni Union cum federation ndo uadimu wake huo. Amesema Tanganyka ilikuwepo ila ikawa replaced na Tanzania Bara ila Zanzibar ikasalia kwasababu ya jina lake japo pia mara zingine inatumia Tanzania visiwani. Hoja ya msingi ni uadimu na uadhimu wa muungano huu sasa wewe weka hoja kwanini muangano huu sio adimu wala adhim.
OK, hebu tuanze mjadala na wewe
1. Federation kati ya nchi zipi?
2. Kwa mujibu wako Tanganyika imekuwa replaced na Tanzania Bara, tofauti ipo wapi ?
 
kuzira, kususa, kugoma tena kwa mihemko na ghadhabu kwa hoja na majadiliano ya kawaida na ya kiungwana namna hii si ndio utimbakwiri wenyewe huu. Sasa unapanic nini na wakati naona una mawazo na hoja nzuri tu?

si utulie upate elimu ya uraia, fatilia vipindi na makala mbalimbali ili kuongeza uelewa na ufahamu zaidi juu ya masuala haya ya Muungano. kughafilika au kupotoka ni mambo ya kawaida tu 🐒
Elimu ipi !.
 
OK, hebu tuanze mjadala na wewe
1. Federation kati ya nchi zipi?
2. Kwa mujibu wako Tanganyika imekuwa replaced na Tanzania Bara, tofauti ipo wapi ?
Mkuu Nguruvi3, unapoteza muda. Kwa bahati mbaya watu aina ya Pascal Mayalla wamejaaliwa kuwa na akili kubwa lakini zisizo za kawaida. Mtu kama huyu akiwa mwizi na akabahatika kuishi ndani ya taifa hili la wajinga ataiba hadi avimbiwe hadi kupasuka!

Wizi kama huu hujulikana kama wizi usio na staha. Yaani mtu anaanza kwa kuiba vya nje na ikiisha anaanza kufanya kufuru. Atawaibia ndugu zake, atawaibia wazazi wake, atamwibia mkewe, atawaibia watoto wake na mwisho ataanza kujiibia yeye mwenyewe.

Naam ndivyo walivyo na mimi binafsi nasita sana kuwa na mnakasha na watu wanaojiita wenye akili hizo huku wakitetea mambo ya kipuuzi na ya kijinga. Hizo si akili ni ugonjwa unaosababishwa na vitu vingi lakini viwili vikubwa ni tamaa na ulafi...tamaa na ulafi ni kama pete na kidole!
 
Wanabodi

Kama kawaida yangu kila nipatapo fursa, huja na kwa Maslahi ya Taifa, kila Jumatano kwenye gazeti la Mwananchi na Jumapili kwenye gazeti la Nipashe na kwenye kipindi cha KMT on Channel Ten TV, kila siku za Jumapili saa 3:00 usiku na marudio Jumatano saa 9:30 alasiri.

Hoja ya leo ni hoja za Utanganyika na Uzanzibari ambazo ni hoja muflis zinazosababishwa watu wanaitwa vitimbakwiri kujivunia uraia ambao haupo kutokana na ujinga tuu wa ukosefu wa elimu ya uraia kuhusu uraia wa Tanzania. Kwenye uraia, hakuna Mtanganyika wala Mzanzibari, tuna uraia mmoja tuu, Mtanzania. Swali ni jee tuwatoe ujinga hawa vitimbakwiri muflis wanaotaka kutubagua kwa Utanganyika na Uzanzibari kwa kuwaelimisha elimu ya uraia, au tuwaache tuu na ujinga wao kujisikia sifa kujinasibisha na kujivunia Utanganyika na Uzanzibari?.

Hili ni Nipashe la Leo.
View attachment 2994081

Ukosefu wa Elimu ya Uraia Kuhusu Katiba, Sheria, Haki na Wajibu, ndio umesababisha, huu ubaguzi wa Utanganyika, na Uzanzibari, watu wakielimishwa kuhusu uraia, hawa vitimbakwiri muflis wanaoleta ujinga wa ubaguzi wa kunyoosheana vidole vya Utanganyika na Uzanzibari, ujinga huu utawatoka, wataerevuka na tutakuwa na Utanzania pekee!.

Hivi karibuni, kumeibuka hoja za kibaguzi za baadhi ya wanasiasa, kutoa kauli za kibaguzi za kuwanyooshea watu vidole na kuwaita “Wao Wazanzibari”, “Sisi Watanganyika”. Miongozi mwa watu wanaotoa kauli hizo ni baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani, waliofilisika kisiasa, na baadhi ya wanaolaani kauli hizo, ni baadhi ya viongozi wa chama tawala, ambapo nimemsikia mmoja wa viongozi hao, akilaani vikali kauli hizo bungeni kwa maneno makali kabisa!, huko pia ni kufilisika kisiasa.

NB. Aliyesema wanasiasa wanaojinasibisha na Utanganyika na Uzanzibari, dini zao, kanda zao, au kabila zao, ni watu muflis, waliofilisika kisiasa, sio mimi ni Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, na akaiandikia kitabu kinaitwa “Nyufa”. Mwalimu alisema dhambi ya ubaguzi ni mbaya sana, ni kama kula nyama ya mtu, ukiishakula huwezi kuacha!.

Uraia ni hoja ya kikatiba na kisheria. Kabla ya Muungano, tulikuwa na nchi mbili za Tanganyika na Zanzibar, hivyo tulikuwa na uraia wa Tanganyika, na uraia wa Zanzibar. Baada ya muungano, tukaungana kuwa nchi moja ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, na kuwa na uraia mmoja tuu, uraia wa Tanzania.

Baada ya Muungano, majina ya nchi hizi zote mbili, nchi ya Tanganyika, na nchi ya Zanzibar, yalibadilika na kuwa Tanzania Bara na Tanzania Visiwani, hivyo jina la Tanganyika likafutwa, ila jina la Zanzibar, liliendelea kuwepo, kutokana na uadimu na uadhimu wa huu muungano wetu.

Uadimu wa Muungano
Miungano ya nchi zote duniani ni miungano ya aina mbili kuu,

1. Muungano wa Union, ambapo nchi mbili zinaungana na kuunda nchi moja. Zile nchi zote mbili zilizoungana , zote zinakufa na kuunda nchi moja mpya. Hivyo ndivyo ulivyo muungano wetu kimataifa, ni muungano wa Unioni, ile nchi ya Tanganyika imekufa, ile nchi ya Zanzibar imekufa, imezaliwa nchi moja mpya ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, yenye urais mmoja tuu, uraia wa Tanzania. Hakuna tena uraia wa Tanganyika, wala uraia wa Zanzibar, kuna uraia mmoja wa Tanzania. Tanganyika haipo nafasi yake imechukuliwa na Tanzania Bara, na Zanzibar japo ipo, ila sio nchi ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, yenye utawala wake wa ndani, lakini hakuna uraia wa Zanzibar, uraia ni mmoja tuu wa Tanzania.

2. Muungano wa Federation, ni nchi mbili au zaidi, zinaungano kuwa nchi moja, lakini zile nchi zote mbili zinaendelea kuwa utawala wake wa ndani, na serikali zao, chini ya utawala mkuu wan chi ya federal state, kama Marekani. Vivyo hivyo muungano wetu kwa ndani ya muungano ni muungano wa federation yenye nchi mbili, Tanzania na Zanzibar, yenye marais wawili, Rais wa JMT “mwenye R kubwa, na rais wa Zanzibar mwenye r ndogo, zenye serikali mbili, serikali ya JMT na serikali ya SMZ, mabunge mawili, Bunge la JMT na BLW, na zenye mahakama mbili, Mahakama ya JMT na Mahakama ya Zanzibar, ila kwenye uraia, bado ni uraia mmoja tuu wa JMT, ila kwa Zanziar, wana ukaazi, ule ukaazi sio uraia ni utambulisho tuu wa wakaazi wa Zanzibar lakini wote ni Watanzania.

Hivyo muungano wa Tanzania ni muungano adimu pekee duniani ambao kwa upande mmoja ni muungano wa union na upande wa pili ni muungano wa federation, hakuna muungano wa aina hii popote duniani.

Uadhimu wa Muungano.
Muungano wetu licha ya kuwa ni muungano adimu, pia ni muungano adhimu, wenye dhima ya kuungana milele!. Miungano yote duniani unaundwa kwa mikataba ya kisheria ya muungano. Mikataba hiyo inakuwa na kipengele cha jinsi ya kuivunja miungano hiyo. Kwenye zile Articles of Union za Muungano wetu, hakuna kipengele cha jinsi ya kuuvunja, muungano, hivyo zile Hati za Muungano sio mkataba wa muungano, ni makubaliano ya muungano, (not a contract, but an agreement) yenye dhima ya muungano wa milele, na ndio maana tunasema “muungano tutaulinda kwa gharama yoyote”.

Tangu tumeungana, na mimi tangu nimezaliwa na kupata akili, sikumbuki hata mara moja, kusikia vipindi vya elimu ya uraia kuhuhusu huu muungano wetu adimu na adhimu, hali inayopelekea Baadhi ya Watanzania kuanza kujinasibisha na Utanganyika wao, na Uzanzibari wao.

Kwa vile Tanganyika ilifutwa na jina la Tanganyika kufutwa, utanganyika nao ukafutika, Watanganyika tunajisabisha kwa Utanzania wetu, lakini kwa vile kwa vile jina la Zanzibar, halikufutwa, na kuna Uzanzibari ukaazi, hivyo baadhi ya Wanzanzibari, wanajinasibisha kwa Uzanzibari wao kama uraia wa Zanzibar, badala ya kujinasibisha na Utanzania wao, kungekuwa na vipindi vya elimu ya uraia kuhusu katiba, sheria, haki na wajibu, kusingekuwepo, vitimbakwiri wowote, wanaojinasibisha kwa Utanganyika wao, au Uzanzibari wao kwasababu, uraia wa JMT ni uraia mmoja tuu, hakuna uraia wa Tanganyika, wala hakuna urais wa Zanzibar, kuna uraia mmoja tuu, uraia wa JMT.

Wiki ijayo, nitaendelea na kuwaletea hizi chokochoko za kuuchokoa muungano na kuanza kunyoosheasha vidole vya ubaguzi wa “Utanganyika na Uzanzibari” zilianzia wapi, dawa yake ni nini na tiba ya kudumu ya kuitibu sumu hii na kuiangamiza kabisa.

View: https://youtu.be/ZJIKhnZCf04?si=fPhb1_0doZmgD7T4
Wakati huo huo, naendelea na darasa langu la elimu ya uraia kuhusu katiba, sheria na haki on Channel Ten kila Jumapili saa 3:00 usiku.
Karibuni.

Paskali

Unajua ndugu Pascal Mayalla mzee kama wewe ikifikia mahali mtu akakuita "mjinga" na Kitambakwiri" labda itakuwa ni kukukosea heshima na adabu...

Lakini inakuwaje kama wewe mwenyewe umejipa hiyo sifa ya UJINGA na UPUMBAVU?

Bila shaka atakeyeitikia na kukufukuzia kwa tabia yako hiyo hatakuwa amekuvunjia heshima yoyote..

Mpaka hatua hii, bila shaka yoyote ni kuwa WEWE Pascal Mayalla ndiye hasa uliye MJINGA na KITIMBAKWIRI unayestahili kuelimishwa na kufundishwa kusikiliza na kuelewa mawazo ya watu wengine..

Tunautaka muungano. Tunataka ushirikiano na watu au nchi zingine. Lakini muungano huo ni lazima uwe wenye usawa na kuheshimiana kwa pande zote zilizokubali kuunga/kushirikiana..

Huu Muungano wa nchi za Tanganyika na Zanzibar ni wa kihuni na ni wa kilaghai kutoka kwa watu ambao toka mwanzo hawakuwa na nia njema (pengine) au walikuwa na nia njema lakini nia njema hiyo ikatekelezwa ktk namna ya hovyo na matokeo yake ndiyo haya..

KWA HIYO: Sio UJINGA wala u - TIMBAKWIRI watu kuzisema kasoro hizi kwa malengo ya kurekebisha. Ujinga na u - timbakwiri ni kule kung'ang'ania kuishi ktk makosa au kasoro. Na huyo mtu ni wewe na wenzako wote huko CCM...

Swali ni moja tu: Mataweza kuwafanya Watanganyika kuishi ktk ujinga wenu hadi lini?

Hilo halikubaliki na ni LAZIMA TUCHUKUE HATUA KUREKEBISHA..[/QUOTE]
 
Mimi matumaini yangu ni kwamba hata tukiwa na raisi mtanganyika dai la kutaka marekebisho ya muundo wa muungano liendelee.

Nasema hivi kwa sababu tumekuwa tunabadili walalamikaji kutegemea nani mtawala.
 
Kwamba hiyo elimu ya uraia uliipata wewe peke yako kutoka mbinguni na ukaielewa kwelikweli?Unazeeka vibaya aisee!Unaiishi dunia ya medieval ages.Unawachagulia watu kitu wasichokitaka au mfanane mawazo kivipi?Jikite kwenye kueleza faida zake.Labda,labda visokorokwinyo na vizabizabina wako watakuelewa.Kwani wewe unakufaidisha nini huo muungano?Au upate sifa tu kwamba.."tumemuona Pascal Njaa anautetea muungano hasa"...!🤣🤣🤣

Ningeongeza kwamba Paskali yeye hatoki sehemu ye yote katika nchi hii.
Nataka ajue ukiwa nje ya Tanzania kila mmoja anajitambulsiha Mtanzania; lakini ukiwa ndani ya Tanzania unajitambulisha unatoka wapi. Hiyo ni kawaida po pote duniani, mtu akiwa ndani ya Kenya anauliza unatokea wapi. Kwahiyo Zanzibar na Tanganyika inapaswa iwepo. Uko ndiko kujitambulisha vizuri. Wewe ndiyo mufilisi mkubwa kwa kuwa hujui utambulisho wako. CCM imetupumbaza kwa kuiua Tanganyika. Hii ni kosa kubwa sana kisheria na kiutamaduni/ kidesturi.
Hata ukiwa Dar unaulizwa unatoka wapi. Naomba serikali ielewe Tanganyika haitakufa kwa nguvu ya CCM.
 
Kwa wakati ule Nyerere alikuwa na haki zote za kuishikilia Zanzibar, ilikuwa ni dunia ya vita baridi kati ya magharibi na mashariki. Wakubwa wa magharibi wakampa darasa lililomuingia juu ya suala la ulinzi wa Tanganyika na wepesi wa mashariki kuivamia nch hii kupitia hivyo visiwa viwili.

Leo tunampigia kelele RIP Nyerere kwa kutazama vigezo vya dunia ya leo wakati yeye alitazama vigezo vya wakati ule. Alikuwa na uhalali wa kuja na maamuzi yale kama tulivyo na uhalali wa kuhoji kilichofanyika wakati ule.
Uhalali wa kuhoji ni haki yetu ya msingi, lakini kuna wanaccm waliojimilikisha nchi kuwa mali yao hawataki tukajadiliana wanataka tufuate wanachotaka wao.
 
Unafiki wetu ni kwamba kuhoji kunakuja kipindi cha rais muislam akiwa mkristo hakuna anayejisumbua kuhoji.

Kuna chembechembe za ubaguzi na chuki kwa wengi wa hawa wanaohoji.
 
Kwahiyo watu walihoji wakati wa Mwinyi, Kikwete na Samia! Weka ushahidi. Ni vyama gani vilivyo na wakiristu tu ambavyo ndivyo vinahoji!
 
Wanabodi

Kama kawaida yangu kila nipatapo fursa, huja na kwa Maslahi ya Taifa, kila Jumatano kwenye gazeti la Mwananchi na Jumapili kwenye gazeti la Nipashe na kwenye kipindi cha KMT on Channel Ten TV, kila siku za Jumapili saa 3:00 usiku na marudio Jumatano saa 9:30 alasiri.

Hoja ya leo ni hoja za Utanganyika na Uzanzibari ambazo ni hoja muflis zinazosababishwa watu wanaitwa vitimbakwiri kujivunia uraia ambao haupo kutokana na ujinga tuu wa ukosefu wa elimu ya uraia kuhusu uraia wa Tanzania. Kwenye uraia, hakuna Mtanganyika wala Mzanzibari, tuna uraia mmoja tuu, Mtanzania. Swali ni jee tuwatoe ujinga hawa vitimbakwiri muflis wanaotaka kutubagua kwa Utanganyika na Uzanzibari kwa kuwaelimisha elimu ya uraia, au tuwaache tuu na ujinga wao kujisikia sifa kujinasibisha na kujivunia Utanganyika na Uzanzibari?.

Hili ni Nipashe la Leo.
View attachment 2994081

Ukosefu wa Elimu ya Uraia Kuhusu Katiba, Sheria, Haki na Wajibu, ndio umesababisha, huu ubaguzi wa Utanganyika, na Uzanzibari, watu wakielimishwa kuhusu uraia, hawa vitimbakwiri muflis wanaoleta ujinga wa ubaguzi wa kunyoosheana vidole vya Utanganyika na Uzanzibari, ujinga huu utawatoka, wataerevuka na tutakuwa na Utanzania pekee!.

Hivi karibuni, kumeibuka hoja za kibaguzi za baadhi ya wanasiasa, kutoa kauli za kibaguzi za kuwanyooshea watu vidole na kuwaita “Wao Wazanzibari”, “Sisi Watanganyika”. Miongozi mwa watu wanaotoa kauli hizo ni baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani, waliofilisika kisiasa, na baadhi ya wanaolaani kauli hizo, ni baadhi ya viongozi wa chama tawala, ambapo nimemsikia mmoja wa viongozi hao, akilaani vikali kauli hizo bungeni kwa maneno makali kabisa!, huko pia ni kufilisika kisiasa.

NB. Aliyesema wanasiasa wanaojinasibisha na Utanganyika na Uzanzibari, dini zao, kanda zao, au kabila zao, ni watu muflis, waliofilisika kisiasa, sio mimi ni Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, na akaiandikia kitabu kinaitwa “Nyufa”. Mwalimu alisema dhambi ya ubaguzi ni mbaya sana, ni kama kula nyama ya mtu, ukiishakula huwezi kuacha!.

Uraia ni hoja ya kikatiba na kisheria. Kabla ya Muungano, tulikuwa na nchi mbili za Tanganyika na Zanzibar, hivyo tulikuwa na uraia wa Tanganyika, na uraia wa Zanzibar. Baada ya muungano, tukaungana kuwa nchi moja ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, na kuwa na uraia mmoja tuu, uraia wa Tanzania.

Baada ya Muungano, majina ya nchi hizi zote mbili, nchi ya Tanganyika, na nchi ya Zanzibar, yalibadilika na kuwa Tanzania Bara na Tanzania Visiwani, hivyo jina la Tanganyika likafutwa, ila jina la Zanzibar, liliendelea kuwepo, kutokana na uadimu na uadhimu wa huu muungano wetu.

Uadimu wa Muungano
Miungano ya nchi zote duniani ni miungano ya aina mbili kuu,

1. Muungano wa Union, ambapo nchi mbili zinaungana na kuunda nchi moja. Zile nchi zote mbili zilizoungana , zote zinakufa na kuunda nchi moja mpya. Hivyo ndivyo ulivyo muungano wetu kimataifa, ni muungano wa Unioni, ile nchi ya Tanganyika imekufa, ile nchi ya Zanzibar imekufa, imezaliwa nchi moja mpya ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, yenye urais mmoja tuu, uraia wa Tanzania. Hakuna tena uraia wa Tanganyika, wala uraia wa Zanzibar, kuna uraia mmoja wa Tanzania. Tanganyika haipo nafasi yake imechukuliwa na Tanzania Bara, na Zanzibar japo ipo, ila sio nchi ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, yenye utawala wake wa ndani, lakini hakuna uraia wa Zanzibar, uraia ni mmoja tuu wa Tanzania.

2. Muungano wa Federation, ni nchi mbili au zaidi, zinaungano kuwa nchi moja, lakini zile nchi zote mbili zinaendelea kuwa utawala wake wa ndani, na serikali zao, chini ya utawala mkuu wan chi ya federal state, kama Marekani. Vivyo hivyo muungano wetu kwa ndani ya muungano ni muungano wa federation yenye nchi mbili, Tanzania na Zanzibar, yenye marais wawili, Rais wa JMT “mwenye R kubwa, na rais wa Zanzibar mwenye r ndogo, zenye serikali mbili, serikali ya JMT na serikali ya SMZ, mabunge mawili, Bunge la JMT na BLW, na zenye mahakama mbili, Mahakama ya JMT na Mahakama ya Zanzibar, ila kwenye uraia, bado ni uraia mmoja tuu wa JMT, ila kwa Zanziar, wana ukaazi, ule ukaazi sio uraia ni utambulisho tuu wa wakaazi wa Zanzibar lakini wote ni Watanzania.

Hivyo muungano wa Tanzania ni muungano adimu pekee duniani ambao kwa upande mmoja ni muungano wa union na upande wa pili ni muungano wa federation, hakuna muungano wa aina hii popote duniani.

Uadhimu wa Muungano.
Muungano wetu licha ya kuwa ni muungano adimu, pia ni muungano adhimu, wenye dhima ya kuungana milele!. Miungano yote duniani unaundwa kwa mikataba ya kisheria ya muungano. Mikataba hiyo inakuwa na kipengele cha jinsi ya kuivunja miungano hiyo. Kwenye zile Articles of Union za Muungano wetu, hakuna kipengele cha jinsi ya kuuvunja, muungano, hivyo zile Hati za Muungano sio mkataba wa muungano, ni makubaliano ya muungano, (not a contract, but an agreement) yenye dhima ya muungano wa milele, na ndio maana tunasema “muungano tutaulinda kwa gharama yoyote”.

Tangu tumeungana, na mimi tangu nimezaliwa na kupata akili, sikumbuki hata mara moja, kusikia vipindi vya elimu ya uraia kuhuhusu huu muungano wetu adimu na adhimu, hali inayopelekea Baadhi ya Watanzania kuanza kujinasibisha na Utanganyika wao, na Uzanzibari wao.

Kwa vile Tanganyika ilifutwa na jina la Tanganyika kufutwa, utanganyika nao ukafutika, Watanganyika tunajisabisha kwa Utanzania wetu, lakini kwa vile kwa vile jina la Zanzibar, halikufutwa, na kuna Uzanzibari ukaazi, hivyo baadhi ya Wanzanzibari, wanajinasibisha kwa Uzanzibari wao kama uraia wa Zanzibar, badala ya kujinasibisha na Utanzania wao, kungekuwa na vipindi vya elimu ya uraia kuhusu katiba, sheria, haki na wajibu, kusingekuwepo, vitimbakwiri wowote, wanaojinasibisha kwa Utanganyika wao, au Uzanzibari wao kwasababu, uraia wa JMT ni uraia mmoja tuu, hakuna uraia wa Tanganyika, wala hakuna urais wa Zanzibar, kuna uraia mmoja tuu, uraia wa JMT.

Wiki ijayo, nitaendelea na kuwaletea hizi chokochoko za kuuchokoa muungano na kuanza kunyoosheasha vidole vya ubaguzi wa “Utanganyika na Uzanzibari” zilianzia wapi, dawa yake ni nini na tiba ya kudumu ya kuitibu sumu hii na kuiangamiza kabisa.

View: https://youtu.be/ZJIKhnZCf04?si=fPhb1_0doZmgD7T4
Wakati huo huo, naendelea na darasa langu la elimu ya uraia kuhusu katiba, sheria na haki on Channel Ten kila Jumapili saa 3:00 usiku.
Karibuni.

Paskali

ni watu wasio na akili tu au wanafiki, ndio wanaweza kuona muungano upo sawa.
 
Back
Top Bottom