Ertugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 14,705
- 30,041
Huu uzi nimeandika nikiwa kwenye dala dala,kwahiyo kwa wale ambao mnasema ni vigumu kuona mtu akifungua JF akiwa public,basi mimi sio kwamba nafungua tu bali hata kuandika uzi naandika pia.
Wazo la kuandika limenijia baada ya kuona mdada amebandika kucha zilizo nakishiwa na gold,nikajikuta algorithm ya kichwa changu inaniletea data mbali mbali kuhusiana na dada zetu
Kama mwanamke amepewa kucha na Mungu na bado akaongeza nyingine je wewe mtoto wa kiume utampa nini mwanamke aridhike? Kama amepewa nywele na bado akaongeza nyingine juu yake,Je wewe mtoto wa kiume utampa nini aridhike?
Kama alipewa matiti na bado akaenda kufanya operation yaongezeke ukubwa ,je wewe mtoto wa kiume kuna kipi utafanya kumridhisha mwanamke
Home boys fanyeni kile ambacho ni muhimu kwa mwanamke,kama kuhakikisha ana sehemu ya kulala, anapata chakula kizuri,anapata mavazi na anapoumwa anapata matibabu
Mambo mengine yafanye kama uwezo unaruhusu,lau uwezo hauna basi usijitese bure au kufanya mambo ambayo yatahatarisha uhai wako na mustakabali wa maisha yako usiibe kazini kisa kutaka kumridhisha mke,usi dhulumu wenzako kisa unataka kumridhisha mwanamke,hauta weza kufanya hivyo.
Mwanamke hapo juu pichani anaitwa Jada Pinkett Smith, mke wa Will Smith ambaye amewahi kuwa mwanamuziki,mchekeshaji na sasa muigizaji maarufu wa filamu duniani,amemwambia mumewe hata afanye nini bado hataridhishwa na mume wake huyo
Mume anajitahidi sana kumpa mkewe dunia lkn she is in love na home boy mwingine,,je wewe home boy wa buza,bonyokwa,nanjilinji na chanika utaweza kumridhisha mwanamke?
Lau ungempa mwanamke dunia yote ipo siku moja angetaka apate na ulimwengu mzima,mpende,mthamini mwanamke kadri ya uwezo wako,lakini usivuke mipaka na kuingia kwenye mitihani ya maisha
Ni hayo tu!