Hongera Baba Askofu Shao wa Kanisa Katoliki Zanzibar

semtawa

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2012
Posts
1,129
Reaction score
1,175
Kiongozi wa dini ni kiungo cha jamii. Hapaswi kuwa mrengo wa kulia au kushoto (katika kujenga jamii moja). Hivyo ni muhimu mno kwa kiongozi wa dini atumie vema ulimi wake ili mwisho wa siku utoe matunda ya umoja, amani, utulivu, usalama na upendo katika jamii.

Ndivyo alivyofanya Baba Askofu Augustine shao. Ameitumia Christmas kukumbuka kuzaliwa Bwana Yesu Kristo, kwa kukumbusha wanasiasa umuhimu wa kupenda meza za mazungumzo kama ambavyo Mkuu wa nchi, Rais na Amiri Jeshi Mkuu Samia Suluhu Hassan, alivyoonyesha pale alipokutana na viongozi wa Baraza la Vyama Vya Siasa. Mahubiri bora kabisa ya Christmas 2021. # Kiongozi wa dini hapaswi kurusha sumu mithili ya nyoka DRAGON bali kuunganisha jamii.

Screenshot_20211225-201743_WPS Office.jpg
 
Hii toilet paper ulioileta hapa nalo ni gazeti hili?

Bishop Desmond Tutu alisema, usipokemea maovu na kujifanya upo neutral wewe tayari umeshachaguwa kuwa upande madhalimu kama haya maccm.
na (Desmond Tutu) akaendelea kusema ...

If an elephant has its foot on the tail of a mouse and you say that you are neutral, the mouse will not appreciate your neutrality
 
Hii toilet paper ulioileta hapa nalo ni gazeti hili?

Bishop Desmond Tutu alisema, usipokemea maovu na kujifanya upo neutral wewe tayari umeshachaguwa kuwa upande madhalimu kama haya maccm.
Kiongozi makini siku zote anapaswa kuongoza jamii yenye kupenda kuzungumza. Mazungumzo huleta umoja, amani na utulivu.
 
Matola, halafu tujenge utaratibu wa kujadili hoja. Hilo gazeti ukijadili heshima yake na mchango wake ktk nchi hii na ukombozi wa Afrika, huwezi kulitaja kirahisi hivyo. Unless knowledge yako iko Limited ktk historia ya hilo gazeti.
 
Kiongozi makini siku zote anapaswa kuongoza jamii yenye kupenda kuzungumza. Mazungumzo huleta umoja, amani na utulivu.
Ni mazungumzo gani hayo wakati unaendelea kuumiza wengine?Acha uwanja huru,waite wote muongee.Na si kuongeaongea.Ni kuongea kwa dhamira haswa ya kuleta maelewano.
 
Matola, halafu tujenge utaratibu wa kujadili hoja. Hilo gazeti ukijadili heshima yake na mchango wake ktk nchi hii na ukombozi wa Aftika, huwezi kulitaja kirahisi hivyo. Unless knowledge yako iko Limited ktk historia ya hilo gazeti.
Lilikuwa.Na si tena.Hata bibi alikuwa binti.
 
Kiongozi wa dini ni kiungo cha jamii. Hapaswi kuwa mrengo wa kulia au kushoto (katika kujenga jamii moja). Hivyo ni muhimu mno kwa kiongozi wa dini atumie vema ulimi wake ili mwisho wa siku utoe matunda ya umoja, amani, utulivu, usalama na upendo katika jamii.

Ndivyo alivyofanya Baba Askofu Augustine shao. Ameitumia Christmas kukumbuka kuzaliwa Bwana Yesu Kristo, kwa kukumbusha wanasiasa umuhimu wa kupenda meza za mazungumzo kama ambavyo Mkuu wa nchi, Rais na Amiri Jeshi Mkuu Samia Suluhu Hassan, alivyoonyesha pale alipokutana na viongozi wa Baraza la Vyama Vya Siasa. Mahubiri bora kabisa ya Christmas 2021. # Kiongozi wa dini hapaswi kurusha sumu mithili ya nyoka DRAGON bali kuunganisha jamii.

View attachment 2058274

..aliyeligawa taifa ni nani, kiasi kwamba imembidi Rais Ssh kuliunganisha?

..nini mahusiano ya Ssh na uongozi ulioligawa taifa?
 
Sehemu yoyote ambako kuna makundi yenye maslahi tofauti na mwingiliano, conflict ipo. Ila conflict haipaswi kuwa sehemu ya maisha ya jamii.

Hata tunavyosema kuunganisha Taifa na meza ya mazungumzo haina maana Taifa letu lina matatizo yoyote makubwa bali ni kuendeleza utamaduni wa kuzungumza. Kushirikisha makundi tofauti ya uongozi ndiyo utamaduni wa Serikali zetu nchini.
 
Lilikuwa.Na si tena.Hata bibi alikuwa binti.
Credibility yake ipo kubwa tu. Kilichobadilika ni maslahi ya itikadi za wasomaji. Watu wa upinzani wasio jadili na kupenda kuangalia issues wao wanaamini kila kinachoandikwa ni kui favor Chama tawala CCM. Ni Uhuru wao kufikiri tofauti ila muhimu wawe wanapenda kufikiri na kuchambua issues kama iliyopo front apo.
 
Credibility?Waachwe kupewa ruzuku(riziki) tuone wataishia wapi!
 
Sehemu yoyote ambako kuna makundi yenye maslahi tofauti na mwingiliano, conflict ipo. Ila conflict haipaswi kuwa sehemu ya maisha ya jamii.

Hata tunavyosema kuunganisha Taifa na meza ya mazungumzo haina maana Taifa letu lina matatizo yoyote makubwa bali ni kuendeleza utamaduni wa kuzungumza. Kushirikisha makundi tofauti ya uongozi ndiyo utamaduni wa Serikali zetu nchini.

..kama unayoeleza ni kweli, basi Askofu ametoa sifa za UONGO kwa Rais Ssh.
 
Ni mazungumzo gani hayo wakati unaendelea kuumiza wengine?Acha uwanja huru,waite wote muongee.Na si kuongeaongea.Ni kuongea kwa dhamira haswa ya kuleta maelewano.
Mwaka 1958 wakati wa mjadala mzito ndani ya TANU kuhusu kama Chama kishiriki uchaguzi wa Kura Tatu au isishiriki, Mwalimu Nyerere aliwaambia wajumbe; " Hatuwezi kupinga uchaguzi wa Kura Tatu nje ya uchaguzi wa Kura Tatu." TANU ilitikiswa lakini ikashiriki uchaguzi...

# UAMUZI WA BUSARA WA TABORA.
 
Hii toilet paper ulioileta hapa nalo ni gazeti hili?

Bishop Desmond Tutu alisema, usipokemea maovu na kujifanya upo neutral wewe tayari umeshachaguwa kuwa upande madhalimu kama haya maccm.
Kumbuka Askofu Tutu ndiyo aliongoza Tume ya Maridhiano Afrika Kusini licha ya ukatili wa utawala wa makaburu. Hapa kwetu tunazungumzia meza za mazungumzo kuendeleza utamaduni wetu misingi ya umoja, upendo na mshikamano wa kitaifa si vinginevyo.
 
Hapana. Yuko sahihi.
..kama unayoeleza ni kweli, basi Askofu ametoa sifa za UONGO kwa Rais Ssh.
Hapana yuko sahihi Baba Askofu. Mazungumzo ni muhimu uwe kama utamaduni. Si vinginevyo.
 
Hapana. Yuko sahihi.
Hapana yuko sahihi Baba Askofu. Mazungumzo ni muhimu uwe kama utamaduni. Si vinginevyo.

..kwamba nchi imegawanyika.

..Rais SSH anafanya juhudi kubwa kuiunganisha.

..lakini pia Ssh alikuwa sehemu ya utawala uliotugawa.

..pia huko nyuma Ssh aliwahi kutoa kauli za kebehi za kuwagawa wananchi haswa kipindi cha KAMPENI.
 
..kwamba nchi imegawanyika.

..Rais SSH anafanya juhudi kubwa kuiunganisha.

..lakini pia Ssh alikuwa sehemu ya utawala uliotugawa.

..pia huko nyuma Ssh aliwahi kutoa kauli za kebehi za kuwagawa wananchi haswa kipindi cha

Nasubiria siku akanushe au kufuta zile kauli za kampeni....nasubiria
 
CCM ndio chanzo kikuu cha kuligawa taifa
Siyo kweli. CCM ni Chama Tawala malengo yake ni kuendelea kukamata dola. Wapinzani nao wanataka dola. Hapo katika maslahi tofauti kunaweza kutokea tofauti kila upande ukitaka hili. Hizi ni siasa. Siasa si uadui ndiyo maana watu wanasisitiza kuwa tofauti za kisasa zinamalizwa kisiasa ktk meza ya mazungumzo.
 
..ccm kwa muda mrefu imekuwa ikitumia mapolisi, mahakama, na tume ya uchaguzi, kuvikandamiza vyama mbadala vya siasa.

..ukandamizaji huo ndio unaosababisha mgawanyiko unaozungumziwa, na kauli za msisitizo kwamba tofauti za kisiasa zimalizwe kwa mazungumzo.
 
Back
Top Bottom