Hongera Dkt. Dorothy Gwajima, The Primary HealthCare Iron Lady

Hongera Dkt. Dorothy Gwajima, The Primary HealthCare Iron Lady

jingalao

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2011
Posts
36,197
Reaction score
29,717
Napenda kumtia moyo Mama Dorothy Gwajima kwani wachache wa namna hii ni adimu kuwapata.

Mungu ampe nguvu Dkt. John Pombe Magufuli ili kuendelea kuibua na kuzilinda hizi hazina ambazo kutokana na ufisadi kutamalaki hazikuwahi kuonekana.

Tanzania inaweza kusimama katika afya bila kutegemea misaada ya kondomu,pedi na vidonge vya uzazi wa mpango.

Awamu ya Tano imesimika miundombinu ya huduma za Afya (HARDWARE)Awamu hii ni kuiweka sawa "SOFTWARE " ya kuhudumia yaani uadilifu na kurejea kwenye misingi ya maadili ya watoa huduma za afya.

Miaka kadhaa baada ya sekta ya afya kuwa ina urahisi wa kupata ajira pameibuka makanjanja wengi walioikimbilia sekta hii wakija na nia ya kupiga hela tu.

Hawa ni vichomi na kamwe hawawezi kumpenda "MD RUSSIA" ambaye amepanda kutoka ngazi ya usimamizi wa wodi hadi wizara(step by step....SIJUI UNAMDANGANYIA WAPI.

Anajua shida wanayopata wananchi,watumishi,viongozi wa afya,n.k

Anajua pa kuwachapa IMAGINE Kila siku tunasikia muuguzi kamfinya na kumdhihaki mjamzito lakini mwisho wa mwaka leseni yake anaipata kama kawa.

BARAZA LA WAUGUZI/ MADAKTARI Kazi kupiga hela za leseni tu. Mkiguswa hoo mama hajakaa kihaiba ya Gov Official.

SONGA MBELE UKAIFUFUE SEKTA YA AFYA NGAZI YA MSINGI.

SONGA MBELE GWAJIMA SONGA MBELE GWAJIMA SONGA MBELE GWAJIMA .

Ni miaka mitano tena ya MABADILIKO YA KWELI.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!!
 
Hivi inakuaje Kuna baraza la wafamasia halafu halijawahi kuja na resolution ya kutengeneza Maji ya IV FLUIDS (NaCL,Dextrose 10%)badala yake tunaimport kutoka UGANDA?

How come P.O.P(CaCO3) (chokaa) tunaimport kutoka nje??

Iweje hadi nguo za kuvaa madaktari/manesi zitoke nje??
 
Huyu mama anatrend sana, na mm ngoja nianze kumfatilia
 
Sekta ngumu sana hii. Kutokana na unyeti wake na wingi wa wasomi waliopo kwenye sekta, watumishi wake aliona wao ni untouchable. Ilifikia hatua hata kujiona ni bora kuliko wengine na kuamua kugomea kutoa huduma kwa kufanya migomo.

Madaktari ni watumishi kama walivyo walimu, maafisa nk. Watekeleze wajibu wao kama walivyokubaliana na muajiri wao. Palikuwa na haja ya kuwa na waziri wa aina hii ili kuweka sawa hii sekta. Wajipange upya kuwa na mwanzo mpya sasa
 
Kuna wizi mkubwa sana ndani ya sekta ya afya. Ila kwa anavyokurupuka na kuropoka hata fanya chochote zaidi ya kufoka foka tu kama Baba yao.
 
Aifufue Sekta ya Afya kuna wakati ilikufa?
 
Hivi kwanini hawa watu wanaovaa bendera za taifa uongozi wao huwa ni wa kutumia nguvu badala ya akili?
Wala hatumii nguvu huyu mama...anafanya data trangulation tu halafu anakupeleka kwenye red corner halafu anakupa option ya kuinua mkono msonge mbele au ubishe akutemeshe nyongo.
 
Field Marshall, mshika kiuno Dr. Gwajima. Hongera sana.
 
Mama Gwajima noma sana wezi wote na matapeli wa afya watakimbia
kuanzia wizarani hadi zahanati ....FIELD MARSHAL ANA MISSION MOJA TU KUFUMUA HII SEKTA ILI IJITEGEMEE NA SIO KUWA CHAKA LA HISANI YA WATU WA MAREKANI.

amechallange kuwa kama unaitaka nafasi yake fanya vizuri uonekane usimletee majungu wewe piga mzigo tu halafu onesha uhodari wako atajiuzulu na kukuachia kijiti kiroho safi tu.
 
Namuunga mkono Mheshimiwa Waziri ila arekebishe style ya uongeaji ili kuendana na hadhi ya cheo chake japo hii isimrudishe nyuma katika kushughulikia hawa wehu wanaoiba madawa yetu.

Kazi nzuri Mh. Waziri tuchape kazi.
 
Back
Top Bottom