Hongera Dkt. Dorothy Gwajima, The Primary HealthCare Iron Lady

Hongera Dkt. Dorothy Gwajima, The Primary HealthCare Iron Lady

Tatizo ni mifumo mibovu tu, hana jipya huyo, business as usual, ccm mmefeli sana kwenye mambo mengi zimebaki kelele nyingi tu.

Hii wizara alivyoingia Hamisi K mkasema sasa basi akaja mama wa Korona mkasema sasa afya imepata tiba eti "muharubaini ".

Sasa kaja msema hovyo gwajima mnasema wizara ilikuwa haifai mara wapiga dili nk, miaka yote mitano mlikuwa mnafanya nini? Kazi kutupigia kelele tu, amini nawaambi gwajima atapita kero za afya zitabaki pale pale mpaka mtakapo fanya utafiti wa kina kuhusu mambo mbalimbali yanayolisibu Taifa.
 
Napenda kumtia moyo Mama Dorothy Gwajima kwani wachache wa namna hii ni adimu kuwapata....
Unajua maana ya CCHP? Unajua maana ya busket fund wewe? Je unajua kwamba 60% ya bajet ya afya inategemea wazungu?
 
Dr Gwajima anasifika kwa kuchapa kazi.

Hata hivyo Kuwaita watumishi wezi, waongo, wazushi, matapeli, wasio wazalendo kisha hachukui hatua za kinidhamu dhidi yao inatia doa utendaji wake.
Watanzania wengi wanapenda "Show ya Kibabe" kuliko hiyo kazi yenyewe.

Yani, ukiwa mwanasiasa mwenye maneno 10% na kazi 90%, watakuona zoba.

Ukiwaa maneno 90% na kazi 10%, watakusifia sana.

Anachofanya huyu Waziri ni mchezo mbaya wa kuigiza unaotia watu uoga, unaovunja morale ya kazi kwa kuwalundika wafanyakazi wote kundi moja, wakati alitakiwa ku target kundi la wahalifu, kuwakamata na kuwafanya mfano.

Aseme hawa wezi tumewashika, tunawashitaki. Akijaribu mwingine kuiba, tutamshitaki hivihivi.

Wakati Magufuli aanaanza urais, nilikuwa nazungumza na rafiki yangu mmoja. Nikawa nasema tumepata rais mkaripiaji sana, anakaripi bila comprehensive strategy. Serikali ya kuvamiavamia na kutishatisha itachoka tu. Kutisha si policy.

Akaniambia, hujaona kitu bado. Vitaibuka vi-Magufuli vingine vidogo vidogo vingi tu. Vitamgeza.

Sasa naona maneno yale ya utabiri yanatimia.

Watu watarudi nyumbani halafu waulizwe na watoto wao wa kizazi cha kuhoji "Baba, kwani wewe ni mwizi? Mbona tumeona Waziri anasema Wafanyakazi wa Wizara yenu ni wezi?
 
Unajua maana ya CCHP? Unajua maana ya busket fund wewe? Je unajua kwamba 60% ya bajet ya afya inategemea wazungu?
Mjomba Naijua HSBF ....for how long sekta ya Afya imepokea HSBF kwa nini hatujaenda kujitegemea kwa kipindi kirefu??
JIBU ANAKUJA NALO GWAJIMA AND THE REAL DREAM TEAM BEHIND HER!!
 
Napenda kumtia moyo Mama Dorothy Gwajima kwani wachache wa namna hii ni adimu kuwapata...
Hakuna lolote.

Wanamchi wanataka bima za afya.Wahudumu wa afya wanataka ajira na mishahara mizuri.

Ashughulikie hayo kwanza sio mbwe mbwe kama za Dkt.Kangi Lugola
 
Watanzania wengi wanapenda "Show ya Kibabe" kuliko hiyo kazi yenyewe.

Yani, ukiwa mwanasiasa mwenye maneno 10% na kazi 90%, watakuona zoba...
Mbona kuna walioshikwa na wameanza kuwa wa mfano?Uzuri wake anawajua vibaka na anajua kuwachambua na hatimaye best way ya kuwashughulikia.

Kumbuka Tz ilifika mahali kibaka hafungiki.
 
Hakuna lolote.

Wanamchi wanataka bima za afya.Wahudumu wa afya wanataka ajira na mishahara mizuri.
Ashughulikie hayo kwanza sio mbwe mbwe kama za Dkt.Kangi Lugola
Bima ya Afya ndio wimbo wake....unajua historia yake katika kuonesha kuwa bima ya afya ni suluhisho la matatizo ya healthcare financing???
She did it Singida/Iramba...go fetch the details.

MWAKA HUU MACHAKA YOTE YAMECHOMWA
 
Bima ya Afya ndio wimbo wake....unajua historia yake katika kuonesha kuwa bima ya afya ni suluhisho la matatizo ya healthcare financing???
She did it Singida/Iramba...go fetch the details.

MWAKA HUU MACHAKA YOTE YAMECHOMWA
Sasa hivi ni waziri.Na sio RMO.Ajikite na sera na sio kusuta.

Asilimia 80 ya watanzania hawana bima nahawana uwezo wa kugharamia tiba.

Tiba za afya bado ni hafifu sababu ya uhaba wa watumishi na mishahara duni.
 
Atengeneze mfumo wa kudhibiti wizara na mahospitali sio kubweka na kudhalilisha watu wenye taaluma zao
 
Sasa hivi ni waziri.Na sio RMO.Ajikite na sera na sio kusuta....
Anahamasisha Bima sana tu.

Anahamasisha uwajibikaji.

Anaelekeza usimamizi thabiti wa mapato ili dawa zipatikane,vituo viajiri watumishi unaweza kuhisi ni ndoto lakini these are the kind of leaders who will make it happen.

STAY TUNE.
 
Atengeneze mfumo wa kudhibiti wizara na mahospitali sio kubweka na kudhalilisha watu wenye taaluma zao
Mifumo ipo na mingine aliwahi kuiweka ila walikuwa wanambania tu....now its the time.
 
Anahamasisha Bima sana tu.
Anahamasisha uwajibikaji
Anaelekeza usimamizi thabiti wa mapato ili dawa zipatikane,vituo viajiri watumishi ....unaweza kuhisi ni ndoto lakini these are the kind of leaders who will make it happen....STAY TUNE.
Anahamasisha kusutana tu mkuu.Uwajibikaji lazima uende sambamba na marupurupu.Huwez kukamua ng'ombe bila kumlisha majani.

Stay TUNED.
 
Back
Top Bottom