Hongera Dkt. Dorothy Gwajima, The Primary HealthCare Iron Lady

Hongera Dkt. Dorothy Gwajima, The Primary HealthCare Iron Lady

aAnahamasisha kusutana tu mkuu.Uwajibikaji lazima uende sambamba na marupurupu.Huwez kukamua ng'ombe bila kumlisha majani.

Stay TUNED.
Mbona zipo clips za uhamasishaji wa Chf tena nyingi zilitoka miaka miwili au mitatu ....akiwa hapo TAMISEMI....?

Fursa ya kutengeneza maslahi ipo mikononi mwao watumishi ila hawakuwahi kuitumia naamini sasa wataitumia vyema.
 
Mbona zipo clips za uhamasishaji wa Chf tena nyingi zilitoka miaka miwili au mitatu ....akiwa hapo TAMISEMI....?

Fursa ya kutengeneza maslahi ipo mikononi mwao watumishi ila hawakuwahi kuitumia naamini sasa wataitumia vyema.
Mkuu naona upo nyuma sana.

Kazi ya waziri sio kuhamasisha bali kuja na mikakati ya kuwawezesha watu woote kupata bima.

Pili wananchi waweze kufaidika na bima hizo ( Ama CHF ama NHIF) kupata huduma za kibingwa.

NHIF imeanza vifurushi vipya( Mfano Najali na Timiza) ambavyo mtu hawezi kupata huduma za kibingwa kama dialysis na tiba za saratani.Na kumbuka asilimia 80 ya watanzania hawana kabisa uwezo wa kugharamia tiba.

Haya ndio mambo ya msingi.Na hakuna hata moja lilifanyika

StAY Tuned
 
Napenda kumtia moyo Mama Dorothy Gwajima kwani wachache wa namna hii ni adimu kuwapata....
Uzi mzuri ila matumizi ya:

1. Primary healthcare= una maanisha ngazi ya Dispensaries & Healthcare Centres au Kwa sababu ktk sekta ya Afya kuna Level za Primary, Secondary, Tertiary.

2. Hardware na Software sio matumizi sahii labda ungetumia Physical Infrastructures
 
Alikuwepo Kangi Lugola, na nakumbuka kada mwenzangu jingalao ulikuwa unamsifia Sana, lakini sote tunakumbuka mwisho wake. Huyu mama atulie, aweke misingi imara ya utoaji wa huduma za afya.

Pia, atambue kuwa kwa Sasa ni waziri, sio naibu Katibu Mkuu Tena. Mambo haya yalimpa umaarufu Sana Wakati akiwa naibu Katibu lakini kwa cheo Cha Uwaziri, anajishusha Sana.

Kwanza ieleweke, wezi wa dawa hawawezi kuisha. Pili, hakuna Daktari ambae hajawahi kula CCD akiwemo yeye mwenyewe enzi anapractise.

Style yake ya Uongozi itamjengea maadui wengi zaidi wizarani, inashusha morali ya wafanyakaz wa wizara na Idara zake, matokeo yake, wizara itaonekana inazingua mwisho atatumbuliwa.

Akae chini, ajenge team work nzuri. Ataacha legacy nzuri.
 
Mbona kuna walioshikwa na wameanza kuwa wa mfano?Uzuri wake anawajua vibaka na anajua kuwachambua na hatimaye best way ya kuwashughulikia.
Kumbuka Tz ilifika mahali kibaka hafungiki.
Waziri anaweza na anatakiwa kuwasema wahalifu bila kuwavunjq moyo wafanyakazi wasio wahalifu.

Huyu anavyobwata ni kama vile kila mfanyakazi ni mwizi.

Si kitu kigumu sana kufanya.

Anavyokaripia ni kama headmistress wa shule ya sekondari anawakaripia wanafunzi watundu, si Waziri anayeongea na wafanyakazi watu wazima wenye watoto na wajukuu.

Vitu kama hivi ndivyo vinafanya watu wengine wenye kujiheshimu kuapa kwamba hatuwezi kufanya kazi serikali ya Tanzania.

Kwa sababu, mtu kama mimi natekeleza wajibu wangu vizuri ukianza kunikaripia kama mimi mwizi nitakujibu majibu yanayokufaa na kukuambia mimi nafanya kazi yangu vizuri, tafadhali sana usinilundike na kundi la wezi kijumlajumla tu.

Halafu itaonekana Kiranga hana nidhamu, kamjibu Waziri.
 
Uzi mzuri ila matumizi ya:
1. Primary healthcare= una maanisha ngazi ya Dispensaries & Healthcare Centres au
Kwa sababu ktk sekta ya Afya kuna Level za Primary, Secondary, Tertiary
2. Hardware na Software sio matumizi sahii labda ungetumia Physical Infrastructures
Soft ware inayohitajika ni kuajiri wahudumu wengi zaidi wa afya na kuboresha marupurupu yao.Watu wana miaka 6 hawana nyongeza.
 
Watanzania wengi wanapenda "Show ya Kibabe" kuliko hiyo kazi yenyewe.

Yani, ukiwa mwanasiasa mwenye maneno 10% na kazi 90%, watakuona zoba...
Well said mkuu.

I can't agree more!
 
Kuna wizi mkubwa sana ndani ya sekta ya afya. Ila kwa anavyokurupuka na kuropoka hata fanya chochote zaidi ya kufoka foka tu kama Baba yao.
Tatizo linakuja pale wanapomdanganya kisha anawashtukia..inabaki aibu tu.
 
Mjomba Naijua HSBF ....for how long sekta ya Afya imepokea HSBF kwa nini hatujaenda kujitegemea kwa kipindi kirefu??
JIBU ANAKUJA NALO GWAJIMA AND THE REAL DREAM TEAM BEHIND HER!!
Shida yako unajilaumu mwenyewe. Tulipata uhuru 1961 nchi haijawahi wakiwa na mpinzani ni walewale kina MAGUFULI.

Waliouzia nyumba hawala zao kina kabula wa kebys.

Wao wenyewe alinunua nyumba za umma, mfno MAGUFULI alinunua magorofa mawili ya NIC kule dodoma kwa laki 6 tena kwa mkopo? Akiwa wazir wa nyumba huyo ni mzalendo? Anaichukia rushes?

Acha kuabudu vikaragosi
 
Ulishawahi kumuona Mwl Nyerere na Mzee Kawawa wamevaa hayo ma Skafu na ma tai ya bendera ya Taifa?
Hivi kwanini hawa watu wanaovaa bendera za taifa uongozi wao huwa ni wa kutumia nguvu badala ya akili?
 
Wapigaji sekta ya afya wanalia sahv
Kazaaa mama kazaaaa

Ova
 
Mkuu naona upo nyuma sana.

Kazi ya waziri sio kuhamasisha bali kuja na mikakati ya kuwawezesha watu woote kupata bima...
Ameshakwambia kuwa ni muhimu kuanza na hamasa then sekta ijiweke tayari kuwahudumia halafu Sera.

I think she knows what is needed and how to approach it.

BIG ACHIEVMENT :
JAFO AMEANZA KUISEMEA CHF,PM NA YEYE Bado tamko la Na.1 shughuli iishe.sasa wakati Sera ikitegemewa kuingia bungeni ni dhambi sana kuwa na challange ya wizi wa dawa vituoni/huduma mbovu vituoni...hivyo inahitajika show ya kibabe ndani ya muda mfupi ili sekta ya afya iwe tayari kuwapa huduma watakaojiunga.

Ni wachache watakaomuelewa kwa sasa ila muda mfupi tutampigia makofi.
 
Ameshakwambia kuwa ni muhimu kuanza na hamasa then sekta ijiweke tayari kuwahudumia halafu Sera...
Ok...

Basi mimi nipo huku Ifakara nasubiri maboresho ya bima za afya.Hayo mambo ya kusutana kwenye media hayana faina kwangu na familia yangu huku kijijini.
 
Ok...

Basi mimi nipo huku Ifakara nasubiri maboresho ya bima za afya.Hayo mambo ya kusutana kwenye media hayana faina kwangu na familia yangu huku kijijini.
nitakuja kukutembelea hapo IFOZA...!
Umewahi kujiuliza kwa nini hatuna hospitali ya wilaya hapo?
 
Naona ule uzi wa vidonge vyake umewauma, sasa umekuja na rangi ya kumpaka ili avutie. Ni hivi, afanye kazi yake, siasa za kiki zenyewe zimeshindwa kumtoa jiwe hadi kaishia kuiba kura.
lini mnaenda ICC?
 
Hivi inakuaje Kuna baraza la wafamasia halafu halijawahi kuja na resolution ya kutengeneza Maji ya IV FLUIDS (NaCL,Dextrose 10%)badala yake tunaimport kutoka UGANDA?
How come P.O.P(CaCO3) (chokaa) tunaimport kutoka nje??

Iweje hadi nguo za kuvaa madaktari/manesi zitoke nje??
Nimewahi kuhudumu Hospitali Teule ya Wilaya ya Muleba Rubya (sijuhi kama bado ni hospitali ya wilaya) Masista Wafamasia walikuwa wanatengeneza Iv fluids aina zote kuanzia Dextrose 50%, 10% na 5%, RL, NS syrups za watoto pale kabla MSD na upigaji wa 10% hawajaingilia kati.

Wizara ya Afya inaweza kuwa inashikilia rekodi ya kuwa pango la wapigaji dili kuliko hata Bandari ya enzi zile. Go! go! go! Dkt. Gwajima....fitina, upendeleo, wizi, nk vilitufanya sisi wenye mapenzi mema na wagonjwa tuache hii kazi na kuwa wakulima!
 
nitakuja kukutembelea hapo IFOZA...!
Umewahi kujiuliza kwa nini hatuna hospitali ya wilaya hapo?
Kuna hospitali ya DDH ( St Francis) ndio inatoa huduma zote.
Kuhusu hospitali ya wilaya ni kweli hospitali kubwa ilijengwa.Lengo ni iwe ya wilaya.

Sasa jimbo lilivyoenda kwa Lijuakali (CHADEMA)basi waka stop shughuli zote za maendeleo pamoja na uzinduzi wa hiyo hospitali ya wilaya kana kwamba wana ifakara hawalipi kodi.

Na hii yote ilitokea sababu "Maendeleo hayana chama".

Stay Tuned
 
Nimewahi kuhudumu Hospitali Teule ya Wilaya ya Muleba Rubya (sijuhi kama bado ni hospitali ya wilaya) Masista Wafamasia walikuwa wanatengeneza Iv fluids aina zote kuanzia Dextrose 50%, 10% na 5%, RL, NS syrups za watoto pale kabla MSD na upigaji wa 10% hawajaingilia kati.
Wizara ya Afya inaweza kuwa inashikilia rekodi ya kuwa pango la wapigaji dili kuliko hata Bandari ya enzi zile.
Go! go! go! Dkt. Gwajima....fitina, upendeleo, wizi, nk vilitufanya sisi wenye mapenzi mema na wagonjwa tuache hii kazi na kuwa wakulima!
zipo hospitali kama K.C.MC zina uwezo wa kutengeneza jiulize kwa nini Muhimbili anunue maji*WATER FOR INJECTION kutoka UGANDA ??
C'MON FIELD MARSHALL MOVE ON AND QUICKLY!!
 
Back
Top Bottom