Hata JPM akimteua tena kwa nafasi nyingine hata kuwa full Minister Dr Faustine Ndugulile hawezi kulamba viatu kama Mwigulu Nchemba.
Dr Faustine ni professional na hapo ndipo anaposimamia na watu wamuelewe hivyo, hapindishi. Kwenye siasa habebwi na mtu bali anakwenda kwa uwezo wake na CV yake. Alipambana kutetea wananchi kwenye kivuko mwaka Ile JPM aliposema wapige mbizi. Aliweza kushinda jimbo DSM kupitia CCM mwaka 2015 bila kuwa tegemezi, huyu siyo mtu wa kubezwa. Nakumbuka ni yeye na Mussa Azzan Zungu ndiyo walilinda heshima ya CCM Dar, mengine yote yalikwenda opposition mpaka mipango ya kuyanunua ambapo kina Abdulla Mtulia na Mtolea ilipofanywa.
Akiwa Mbunge 2010-15 aliweza kutetea wana Kigamboni dhidi ya dhuluma ambayo ilikuwa inapangwa kupitia Prof Tibaijuka na akamshinda.
Ni Msomi bingwa wa virology na micro biology ambaye amekwisha fanya kazi za kimataifa mpaka kuisaidia South Africa katika kujenga mifumo ya Blood Transfusion kupitia USAID.
Ni mmoja kati ya wasomi wa ku jivunia. KAMWE HALAMBI VIATU VYA MTEUZI