Umekuja kusifu boss wako haya tayari umeshinda hongera vipi wamepona wangapi kwenye kujifukiza
Sent using
Jamii Forums mobile app
KUJIFUKIZA (STEAM INHALATION OR AROMATHERAPY)
Kujifukiza (steam inhalation) sio tiba ya corona bali ni njia nzuri sana na sahihi yenye gharama nafuu ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya COVID 19
Kuna hatua mbalimbali ambazo ni lazima zipitiwe kabla havijachimba na kuingia kwenye kuta za njia ya hewa (Respiratory tract)
Hatua ya kwanza kabisa ni CONTAMINATION
Contamination ya virusi vya COVID 19 inaweza kuanzia kwenye mikono pale mtu anapoguana moja kwa moja na virusi au inaweza kuwa kwenye njia za hewa pale mtu anapovuta hewa iliyochangamana na virusi vya COVID !9
Lengo la kunawa mikono kwa sabuni na maji yanayotiririka na matumizi ya sanitizer ni kuondoa physical contamination na vijidudu mbalimbali visivyonekana kwa macho kama vile virusi vya korona
Lengo la kuvaa barakoa ni kupunguza uwezekano wa contamination kwa njia ya hewa ambapo vijidudu vinaweza kutoka kwa mgonjwa wakati wa kukohoa au kupiga chafya na kumwingia mtu mwingine.
Ili kuondoa contamination ndani ya njia za hewa kabla wadudu hawajachimba na kuingia ndani ya chembe hai ni kujifukiza
Kuna malengo mengi sana ya kujifukiza na hapa mimi nazungumzia kujifukiza kwa lengo la kuondoa contamination katika njia ya hewa
Unapojifukiza kwa lengo la kuondoa contamination ya virusi ndani ya njia za hewa tunatumia maji na mafuta mvuke yajulikanayo kama ESSENTIAL OILS. Essential oil ni mafuta yaliyo na viasili dawa vyepesi (volatile plant compounds)
Mfano mzuri viasili hivyo yaani volatile Compounds ni majimaji makali yanayoruka tunapomenya matunda jamii ya citrus kama chungwa limao ndimu chenza na hata tunapokata vitunguu haya ndiyo maji yanayofanya tutote machozi.
Mafuta haya mepesi huchujwa kutoka kwenye majani magome na maganda ya matunda mbalimbali kwa kutumia njia ijulikanayo kama DISTILLATION amayo ndiyo pia kuandaa pombe Kali (liquor) na yana uwezo wa kuharibu maendeleo ya virusi kabla havijachimba na kuingia ndani ya chembe hai na kusababisha maambukizi yaani infection
Kuna miti mingi sana inayoweza kutumika kutengeneza hizi essential oil Mimea hiyo ni kama
Eucalyptus globulus, Camphor, Thymus Vulgaris, Foeniculum Vulgaris, cinnamomum Zeylanicum, Mentha Piperita, Syzigium Aromaticum, Cymopogon Citrutus na mingineyo.
Eucalyptus Globulus mmea ujulikanao hapa Tanzania kwa jina la MKARATUSI DAWA una wingi wa volatile components ambazo zimonyesha uwezo mkubwa wa kuvuruga maendeleo ya virusi nje ya chembe hai na hata ndani ya chembe hai (in vitro and vivo)
Kwa mfano mkaratusi dawa umethibitika kuwa na components zifuatazo ambazo hazina madhara yoyote katika mapafu ya mwanadamu na zenye uwezo wa kukatisha maisha ya virusi na bakteria. volatile component hizo ni kama
-CINEOLE
-PINENES
-SESQUITERPENE ALCOHOLS
-AROMADENDRENE
-CUMINALDEHYDE
Hizi zote ni dawa zenye thamani kubwa sana lakini zinapatikana kwenye mikaratusi miti ambayo inapatikana kwa wingi sana mafinga na mkoani njombe. Miti hii mara nyingi hutumika kutengenezea nguzo za umeme na majani yake hutupwa ambapo yangetumika kutengeneza essential oil na ikauzwa ndani na nje ya nchi na nchi ikapata pesa nyingi za kigeni.
Nadhani wasomi katika kitengo cha FOOD AND BIOCHEMICAL ENGINEERING wananielewa vizuri ninapozungumzia utajiri huu. Wateja wakubwa wa essential oil ni makampuni ya kutengeneza dawa za binadamu na viwanda vya perfume
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa mwaka 2009 na kuonyesha uwezo wa cineole itokanayo na mkaratusi dawa(Eucalyptus Globulus) katika kutika kupunguza maambukizi ya virusi na bakteria katika njia za hewa.
https://onlinelibrary.wiley.com/doi/abs/10.1097/00005537-200404000-00027
Hatua ya pili ni INFECTION
Katika hatua hii virusi tayari vinakuwa vimefanikiwa kuchimba na kuingia ndani ya chembe hai. Katika hatua hii virusi tayari vinakuwa vimeanza kutoa amri kwa chembe hai kuzalisha virusi zaidi
Katika hatua hii njia za kujifukiza haiwezi kuondoa maambukizi na hapo kinga ya mwili wa mtu husika (immune response) katika kuhakikisha virusi haviongezeki na kuleta madhara yoyote mwilini.
Bahati mbaya sana inaweza kutokea kwamba kinga ya mtu haiwezi kurespond vizuri kukabiliana na virusi kwa sabababu mbalimbali. Ni vema tukafahamu kwamaba ziko protocol mbalimbali zinazoweza kuongeza kinga ya mwilli
Tafiti zimeonesha kwamba mimea kama
-ECHINACEA ANGUSTIFOLIO MAJANI
-MZIZI ASTRAGALUS MEMBRACEOUS
inaweza kuongeza kinga ya mwili na kuupa mwili nguvu ya kukabiliana na virusi vya aina mbalimbali.
IKUMBUKWE
Kujifukiza kutakukinga na maambukizi ya korona iwapo bado virusi hivi havijachimba na kuingia ndani ya chembe hai zinazounda kuta za njia za hewa
Kwa hiyo tuendelee kunawa mikono, kutumia sanitizer, kuvaa barakoa na kujifukiza mafuta ya mkaratusi yaliyochanganywa na maji hii itauepusha na maambukizi dhidi ya Corona..