Salaam Wana jamvi.
Napenda kumpongeza Naibu Waziri wa Afya kwa majibu na maelezo yake kuhusu suala la Covid-19. Dkt. Ndugulile amekuwa akitoa majibu na maelezo ya kitabibu zaidi kama ilivyo taaluma yake.
Kuhusu maelezo ya baadhi ya viongozi wa dini na wanasiasa kupinga matumizi ya barakoa, Dkt. Ndungulile amesisitiza matumizi ya barakoa. Kuhusu kujifukiza alitahdharisha madhara yanayoweza kutokea kwenye mfumo wa hewa kutokana na kujifukiza. Kwa kweli huyu msomi amekataa kuwa kasuku, amesimamia taaluma yake kuliko cheo chake.
Hongera Dkt Faustine Ndungulile maana katika hili la Covid-19 ukweli ndio utakaotusaidia badala ya siasa za kujikomba.
Nawasilisha.