Hongera Haji Manara kwa kupewa kazi ya usemaji wa kampuni ya Tigo

Hongera Haji Manara kwa kupewa kazi ya usemaji wa kampuni ya Tigo

LIKUD

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
18,037
Reaction score
33,681
Hongera sana Haji Manara kwa nafasi hiyo adhwimu.God bless!!!

Aliyepewa kapewa.

Itoshe kusema kwamba Mganga wa Haji sio tapeli.
---
Kupitia Ukurasa wake rasmi wa Instagram HajiManara anathibitisha kupata usemaji wa Kampuni ya Mawasiliano ya tigo. Katika kulieleza hili Haji Manara anaandika:

Alhamdulillah 🙏🏻🙏🏻

Unadhani mimi ni hodari sana kiasi cha kuendelea kupata hizi deals za Makampuni? Hapana ni Mungu tu anaeniangazia na pengine kuuvaa uhusika nnapokabidhiwa jukumu na wao au Taasisi nnazofanya nao kazi.

Kuisemea Kampuni kubwa kama hii hususan katika kipindi hiki cha Holiday na kwa namna walivyojipanga na hizi Zawadi kubwa kubwa ni zaidi ya Mipango ya Mungu, na ni heshma kwetu ndugu zangu.

Sisi tumetoka Uswahilini huko kuja kupewa fursa kama hizi ni ushindi kwa Mahaslers wote.

@tigo_tanzania mmepata Semaji, Mmepata Mwanamme hasa anaejua kazi yake, Mtaenjoy mwaka huu.
 
Kiingilishi kinapanda?...

Elimu ya Telecom ipo? Ok.
Exposure je?......

Anewei.. hongera kwake.

Wasemaji au maafisa habari wa makampuni au mashirika huwa hawana nasaba na taaluma inayohusiana na biashara kuu ya kampuni au shirika...

Mara nyingi huwa ni watu wenye taaluma ya habari...

Hizo mambo za kitaalamu huwa wanapigwa msasa wakiwa kazini...
 
Unajua kuitwa MSEMAJI ujue ni jina zito sana.

Lazima Biashara uijue haswa, ujue mambo ya kiteknolojia ujue taasisi mipango yake yaan Strategic plans..

Huyu jamaa kule kwenye Mpira palimfaa kwa kuwa anafaham Mpira maana amezaliwa na kukulia ktk Mpira.

Ila huku kwenye maswala ya 5G mara 4G na unaenda ktk midahalo ya kimataifa kuzungumzia kampuni yako. Una content..?
 
Pamoja na madhaifu yake yote, matusi na lugha chafu ila ukweli Manara ana karama ya umashuhuri.

Kila anachogusa na kufanya ni habari. Sijajua usemaji huo utakuwa wa aina gani hasa kwenye mtandao wa simu ila sina mashaka na utekelezaji wake.

Manara alizaliwa kufanya anachokifanya.
 
100%
Akitoka Tigo anaenda kuwa msemaji wa Rais Ikulu
 
Back
Top Bottom