Hongera ITV kumhoji Tundu Lissu. Hongera sana Tundu Lissu kuzungumza kistaarabu kwa lugha za staha. Ruksa kuhisi chochote, sio fair kutaja majina!

Hongera ITV kumhoji Tundu Lissu. Hongera sana Tundu Lissu kuzungumza kistaarabu kwa lugha za staha. Ruksa kuhisi chochote, sio fair kutaja majina!

Pascal tokea ufahamike (ujipambanue) kuwa kada wa kuchonga wa CCM ile credibility yako iliyokuwepo hapa JF imepotea kabisa na kufikia mahali watu wanakuita majina mabaya.

Hujachelewa, hata katika wokovu tunafundishwa kuwa ili uokolewe na kurudishwa kundini ina kupasa UMKANE SHETANI NA KAZI ZAKE ZOTE.

Ni wakati muafaka sasa upate wokovu kwa kumkana shetani (CCM) na kazi zake zote uokolewe na kurudi kundini (JF) ambapo naamini unapathamini sana ndio maana hata mbele ya Rais (2016) ulitamka wazi kuwa wewe na JF ni damu damu
 
Mwenzangu katika kugombea uteuzi usiwe kinyonga huku na kule,kuwa consistent. Sio kwa vile Magufuli hayupo madarakani,wala Lissu, ndio uwatupie vijembe, hawatakukumbuka ng'o!....endelea tu kama ulivyokuwa unam praise Magu..

Mgombea mwenza wa uteuzi!,,lol
 
Kwa hakika mimi nawapa pongezi wote wawili. - Yaani Bi, Farhiya na mh. Lissu. Katika miaka iliopita tuliona akina Tido Muhando wanauliza masuali kwa wapinzani kama mbogo.

Mwana dada anauliza masuala kistaarabu kabisa. Tido muhando hafiki hata chembe licha ya umaarufu na uzoefu wake, Hongera.
 
Sisi Chadema tunatuma Maombi Maalum kwa Mgombea Urais wa CCM Mzee Daktari bingwa wa kemia duniani Bwana Magufuli Kukubali Kuwa na MDAHALO na Mgombea Urais Wa Chadema Kamanda Tundu Lissu ili Kushindanisha SERA na Mitazamo Yao kwa Nchi Yetu Live kwenye TV na Redio Zote za Duniani na Wananchi Wote Watasikiliza!:
🙂 🙂🙂😀😛😆😅😂🤣
 
nchi hii Lissu anaongozs kwa IQ kubwa.
Nchi yetu inawahitaji akina Lissu wa upande ule, akina Zitto wa upande mwingine ila sioni kama CCM imeaandaa watu wanaoweza kusimama wao wenyewe kihoja bila favor za kuwa chama dola.

Hoja hujibiwa kwa hoja, hoja zote za Lissu zinajibika, sema zinahitaji mjibu hoja aliyeshiba kifalsafa, kiakili na kimawasiliano (communicator). Tatizo la CCM wanapalilia wachumia tumbo waimba sifa but watupu kumkichwa badala ya kuvutia free-thinkers, walioiva kimaarifa lakini wanaoamini katika falsafa ya Magufuli.

Mi binafsi naamini katika falsafa ya Magufuli kiuchumi lakini nachelea kusema kuwa huyo mzee amezungukwa na watu wanaomuogopa wanaomfuata si kwa sababu ya itikadi bali kutetea mkate wao. Na hawatamsaidia kujibu hoja za Lissu.
 
huyo mzee amezungukwa na watu wanaomuogopa wanaomfuata si kwa sababu ya itikadi bali kutetea mkate wao. Na hawatamsaidia kujibu hoja za Lissu.
CCM wote hawana uhuru wa kufikiri tena, wamekuwa brainwashed na jiwe kwamba kama hausifii kaa kimya au utashughulikiwa, ukisifia kuna vizawadi vidogo vidogo utapata, so wanashindana kumsifia jiwe kwa lolote badala ya kuthink otside the box nini watu wanataka.

hoja za kumjibu Lissu hawawezi kuwa nazo watataja tu tumenunua mandege cash bila kujua wameipa nchi hasara.

uhuru anaouongelea Lissu ni pamoja na uhuru wa kufikiri na kukosoa kama aliokuwanao Membe alipokuwa ccm.

Ilibaki kidogo jiwe atuaminishe watanzania wote upinzani nchi hii umekufa bahati nzuri kaja Lissu katufumbua macho na akili.

cc. mataga, praise team.
 
Lissu kazungumza ukweli mtupu, uzuri wa lissu ni mkweli sana na mzalendo wa nchi yetu. Tatizo la mtoa mada ni mnafiki sana.asemacho sicho anachokiamini kiamini. Anasema rais hawezi mtengua CAG ilihali aliyepita aliondolewa kwa nguvu
 
Yapo mambo kadhaa aliyoyazungumza Lissu ambayo, in theory, ndivyo yanavyopaswa yawe. Lakini, in practice, hasa katika mchi yetu, ukiyatekeleza ni kama kufungulia shimo la choo.

Uhuru wa kiuchumi. Kweli siasa za ujamaa zilitushinda. Alipokuja mzee Ruksa na uhuru wake wa kiuchumi wafanyakazi waliishi kama mashetani. Alipokuja mzee Mkapa na uhuru wake wa kiuchumi Lissu huyu huyu alikuwa akigombana naye takribani kila siku. Alipokuja Kikwete na uhuru wake wa kiuchumi nchi ikawa kama shimo la panya. Magufuli katight mambo kiaina kama ujamaa fulani but mambo yote yanakwenda. Not perfect lakini inaonekana uhuru wa kiuchumi kwa nchi yetu haiendi kama theory inavyosema.

So kwa kumjibu Lissu, nchi yetu inahitaji bado top-down control ya serikali.
Kumwelewa lissu unahitaji kuwa na IQ kubwa sana
 
Back
Top Bottom