Hongera ITV kumhoji Tundu Lissu. Hongera sana Tundu Lissu kuzungumza kistaarabu kwa lugha za staha. Ruksa kuhisi chochote, sio fair kutaja majina!

Hongera ITV kumhoji Tundu Lissu. Hongera sana Tundu Lissu kuzungumza kistaarabu kwa lugha za staha. Ruksa kuhisi chochote, sio fair kutaja majina!

Lissu kazungumza ukweli mtupu, uzuri wa lissu ni mkweli sana na mzalendo wa nchi yetu.Tatizo la mtoa mada ni mnafiki sana.asemacho sicho anachokiamini kiamini. Anasema rais hawezi mtengua CAG ilihali aliyepita aliondolewa kwa nguvu
Mamlaka ya uteuzi ikifanya mabadiliko ni kumuondoa kiongozi kwa nguvu?
 
Kumhisi mtu yoyote au kumshuku mtu yoyote is your right, lakini kumtaja hadharani kwa majina huyo unayemhisi, is not right unless una ushahidi usiotia shaka, na ukiitwa kuthibitisha, utathibitisha pasipo kubabaika wala kujiuma umma.

Wewe unajuaje kama akiitwa athibitishe atashindwa?

Usimsemee mtu, juu ya yote Tundu Lissu is a guru in law anajua kile anachosema and what would be its consequences hivyo huna haja ya kumfundisha.
 
Sijui kama siku ya kesho itaisha salama kwa ITV. Mwenendo wa Campaign unaonyesha JPM kachoka na anaongea ongea tu, nimeanza kuelewa kwanini JPM anamuhofia sana Lissu
Jamaa hajui mpaka muda huu ashike kipi aache kipi akiangalia Nyuso za watu wake anao waomba kura ndo anachoka mwili na akili.
 
Kama vile humpendi LISSU hivi then nafsi inakataa unaweka pongezi kwa itv. ITV wamefanya yao na sisi hatuwezi kuwawekea midomoni maneno yapi wahojiwa waongee. Hatupaswi tuwachagulie nini waongee na watu gani wadiwataje. Tume bila kunyoshewa vidole hawatajirekebisha. Wanaonyesha udhaifu mkubwa sana lazima watajwe majina
 
Hakika, Tume inasema wamejiandikisha watu m29, maana yake nusu ya watanzania wamejiandikisha kupiga kura, tunakaribia kufikia m60.
Sijui hili linawezekaje!!!!!
Hebu tujifikirishe, hakuna nchi duniani ambayo wapigakura waliojiandikisha ikafika nusu ya idadi ya watu? Vinginevyo tume imeandaa kura za maruhani kwa aliyewateua.
 
Back
Top Bottom