Hongera JamiiForums, Sauti yenu Imefika Wizara ya Elimu kuhusu Watoto kutokufunga Shule Likizo

Determinantor

Platinum Member
Joined
Mar 17, 2008
Posts
59,045
Reaction score
94,974
Nimefurahi sana baada ya malalamiko yaliyotolewa hapa kuhusu Wanafunzi kutokufunga shule wakati wa Likizo.

Nimeona barua ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kitengo cha Udhibiti Ubora wakizataka shule hizo kutoa maelezo kwa nini hawakufunga shule.

Nikiwa kama Mwalimu kitaaluma naungana na wizara ya Elimu na niwapongeze sana kwa kutupia jicho na wawachukulie hatua

Wanafunzi sio empty Jars waliondaa mitaala wana akili na walijua kuwa mwanafunzi sio masomo tu.

Shukrani sana kwa JF na kwa Wizara ya Elimu. Naweka na barua hapa

Screenshot_20210611-190804.png
 
Mchango shs 15,000 kwa mtoto mmoja ni extra fees wakati huu wa likizo wakiwa wanajiandaa na mtihani wa mwisho wa kidato cha nne na standard seven.

Kwa kuondoa mshikemshike na serikali viambatanisho hivyo watavipata, maana vikao na wazazi walikaa na makubaliano yakafikiwa.
 
Ni sahihi ila Walioweka likizo sio Wajinga, watoto wanahitaji mapumziko ujue. Kuna extra curricular activities. Sasa kuwashindilia tu masomo mwanzo mwisho ni kuwakaririsha, which is not health at all
 
Nimefurahi sana baada ya malalamiko yaliyotolewa hapa kuhusu Wanafunzi kutokufunga shule wakati wa Likizo.

Nimeona barua ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kitengo cha Udhibiti Ubora wakizataka shule hizo kutoa maelezo kwa nini hawakufunga shule.

Nikiwa kama Mwalimu kitaaluma naungana na wizara ya Elimu na niwapongeze sana kwa kutupia jicho na wawachukulie hatua.

Wanafunzi sio empty Jars waliondaa mitaala wana akili na walijua kuwa mwanafunzi sio masomo tu.

Shukrani sana kwa JF na kwa Wizara ya Elimu. Naweza na barua hapa

View attachment 1815525
Lilipaswa kutoka agizo la moja Kwa moja, shule nyingi za binafsi zitaangushia makubaliano Kati ya shule na WAZAZI, uzoefu unaonyesha shule nyingi za private zinakuwa na kundi la mamuliki wanaojifanya WAZAZI na wao siku zote huunga mkono maamuzi ya shule
 
Hahahahaha nimecheka sana maana kuna Wazazi mahali wanatokwa povu bila kujua kuwa wanatetewa wao wenyewe na future ya Watoto wao
 
Huo ndo ukweli Mimi hata Yale magroup ya wazazi wa watoto mashuleni sijiungagi kabisa, make humo kwenye magroup kuna wazazi mpaka kero endapo utaenda kunyume na mipango ya shule wao ndo matajiri, wanaojua maana ya elimu, wanaojua malezi, kero tupu, Kwa sasa imekuwa kawaida drs la 4, 6 na 7 kupewa maprogram ya ajabu ajabu Kwa kisingizio cha kujiandaa na mitihani na mwisho siku matokeo hayatimofautiani saana na shule za serikali. Zaidi tunaambulia kiingereza Tu. Watoto waruhusiwe kufunga shule wajifunze mambo mengine ya nyumbani, Mtoto ajufunze hata kufuga kuku, siyo kila siku homework akiachana na issue za shule kidogo ni remote ya TV, big noo
 
You nailed it pale pale! Kuna wazazi hawajui hizi mambo ndio Maana nikaweka kabisa na hio theory hapo ya Piaget, nilimsoma nikamuelewa zaidi ya 16yrs ago.
Maisha ni zaidi ya kukariri
 
Tunakosa hata muda wa kuwafundisha mambo mengine ya muhimu zaidi ya kukaririshwa huko mashuleni.

Kwa kweli Tz kungekuwa na homeschooling ningemfundisha mwanangu mwenyewe nyumbani huko shule aende kufanya mitihani tu.. shule za siku hizi hazina activities za kuwachangamsha watoto ni kutizama madaftari kuanzia saa 2 mpaka 9 hawainui hata migongo, enzi zetu shule haikuwa about vitabu pekee
Shule ilikua sehemu nzuri sana ya socialization na skill building na sio kukaririshwa.
Tulikua na nyakati za kucheza, kufurahi, kusali na kusoma!

Elimu ya Tanzania inajenga kaburi kubwa sana kwa future ya Watoto wetu

Inaua creativity, kwa mfano, kwanini shule zinunue mboga za majani wakati wangeweza kuwa na bustani za mchicha, tembele etc? Huyu mtoto hajui hata spinach kama inapandwa au inachimbwa.

What a shame?
 
Kwamba madogo wengine wanajua spinachi inachimbwa kama viazi😁😁😁😁😁
 
Nimefurahi sana baada ya malalamiko yaliyotolewa hapa kuhusu Wanafunzi kutokufunga shule wakati wa Likizo.

Nimeona barua ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kitengo cha Udhibiti Ubora wakizataka shule hizo kutoa maelezo kwa nini hawakufunga shule.

Nikiwa kama Mwalimu kitaaluma naungana na wizara ya Elimu na niwapongeze sana kwa kutupia jicho na wawachukulie hatua.

Wanafunzi sio empty Jars waliondaa mitaala wana akili na walijua kuwa mwanafunzi sio masomo tu.

Shukrani sana kwa JF na kwa Wizara ya Elimu. Naweza na barua hapa

View attachment 1815525
Halafu usisahau kuleta mrejesho wa hatua zitakazochukuliwa.
 
Kwamba madogo wengine wanajua spinachi inachimbwa kama viazi😁😁😁😁😁
Siyo utani nakumbuka mara ya Kwanza wakati naamia Dar toka Arusha, Mimi nilitangulia nikawa nimenunua Shamba, na nilikuwa na kijana ambaye kipindi hicho alikuwa form one mzumbe sekondari akiwa ametokea hizi shule zetu pendwa, nilishangaa kwenda naye Shamba Mtoto hajui hata mti wa mnazi hajui kiazi kinapatikanaje, tangu siku hiyo mwisho kabisa kusoma shule binafsi, alipomaliza mzumbe katupwa huko mbeya Kataka kuleta ngonjera nikamwambia huko huko. Kamaliza six kapangiwa jkt Kanembwa kaleta ngonjera hoo kambi za kigoma ziko harsh ni kamwambia huko huko, mwisho siku kaenda kujisalimisha Ruvu sijui aliwaeleza nini naona wamempokea. Kwangu naona ninhatua kama ameweza kwenda na kujibadilishia kambi mwenyewe naona kuna mabadiliko kutoka Ile mentality ya st
 
Back
Top Bottom