Hongera JF kwa Whistleblow, JF tubadilike, tusichafue majina ya Watu kwa tuhuma za Hearsay zisizo na Uthibitisho, Ukituhumu, Weka Uthibitisho

Huyo jpm unaye muota tayari Mungu kesha mtwaa kitambo ndugu .

Geuza macho tazama aliyepo maana ndiyo katiba imetupatia .

Japokuwa JKN alishatangulia bado mtu anaweza kumu quote na asilazimishwe kutomtaja. Sijui umefikiria nini kuona shida kwangu kumtaja JPM, ni dhahiri he was a man, it is unfortunately that only sensible people will second this. Siwezi kulazimishwa hata siku moja kumkubali unayetaka kunilazimisha nimkubali na mimi pia simlazimishi mtu akubali kuwa JPM alikuwa a “Man”. Reasoning capacity ya mtu ndo itamfanya aamue, ila kama mtu akitanguliza mapenzi ya ukabila na Udini hapo ndo utaona watu wanatoa mapovu.
 

Paskali una angalizo zuri, lakini watu wanaona bora waweke hizo hearsay humu mitandaoni, maana taasisi za uchunguzi na kutoa haki nazo zinafanya kazi nje ya weledi kabisa. Mifano mirahisi kabisa, kuna nyumba ilikamatwa ikiwa imejiunganishia bomba la mafuta hapa Dar, waziri mkuu na IGP wakasema ndani ya siku 7 watatoa ripoti ya jambo lile, lakini mpaka leo kimya.

Hata watu wakiamua kwenda mahakamani, bado mahakamani kwa sasa sio sehemu ya uhakika ya kwenda kupata haki, mfano hii kesi ya Mbowe kama kuna documents zimewafikia mashahidi kinyume na utaratibu na bado jaji anakoroga unategemea nini? Kuna mashahidi unaona kabisa wanatoa ushahidi wenye kutia shaka lakini wanaachwa.

Kwa mifano hiyo ya wazi wa taasisi za kufanyia kazi tuhuma ziko chini ya weledi, unategemea watu waache kuja kuanika huku mitandaoni. Fuatilia vizuri hicho unachosema ni kuchafuana, utakuta zaidi ya nusu ni kweli kwani ni watu wanaojuana na machafu yao. Watu waliopo madarakani kwa uchaguzi wa kishenzi vile watakuwaje wasafi?
 
Sukuma Gang Mlishangilia Sana Ubaguzi
Qmme Zenu sasa Kibao kimewageukia, tulieni Dawa iwaingie
Pascal ameamua kumchoma mkanda mwenzake. Kaaumua ku-frame kabisa namna uchunguzi unatakiwa kufanywa dhidi ya Biteko.
 
Huyo ngungenge ni kama sio january basi ni chawa wa january post zake nyingi humj zinekaa kimajungu majungu sana
 
Kiukweli mtu anayemchafua mtu kama Prof. Mkenda, ni anajichumia tuu dhambi za bure. Kuna watu uadilifu wao, unaonekana wazi kabisa machoni, wala huhitaji microscope.
P
Ukiona hivyo jua vijana wako kazini kumuundia genge. Yaleyale ya Kalemahindi juu ya magenerator ya kigoma kisa tu wamwondoe mtu. Kumbukizi moja ya vita vya rost ya amu kununua magazeti yote ya rai ili apenyeze propoganda chafu kumwondoa PM Sumuye asigombee urais ili mzee wa msoga apite kilaini enzi za denjaman mkaapo akimaliza muda wake
 
Umkubali usimkubali mama Samia ndiye mwenyekiti wenu wa ccm na hilo ni lazima wala hakuna kubembelezana.
 
Acheni hizo tuhuma zifangiwe uchunguzi na sio kumnanga aliyeleta habari, ni swala la mda ukweli utajulikana na huyo Doto tuhuma za kuhusu madini ziko tangu enzi za Magufuli na hata Uraia wake alipewa kinguvu na Magufuli.
So lisemwalo lipo ka halipo basi laja
 
Nakuunga mkono huyo whistle blower kaanzisha hyo mada then kazi kwa Takukuru kuchunguza hizo tuhuma na sio kusema eti aweke yeye ushahidi hapa
 
Hii nchi kuna utofauti mdogo sana kati ya mtu fisadi na mtu safi...

Mimi nikisikia kuwa mtu fulani ni fisadi, jambo la kwanza huwa naamini hiyo taarifa hata kama haina ushahidi...
Kwa hiyo tukiambiwa Watu8 ni fisadi jambo la kwanza ni kuamini uambiwaji / maelezo huo/hayo bila hata ushahidi.

Kama msimamo ndiyo huo kama taifa, basi tufute dhana ya ushahidi.
 
Tunaomba ushahidi wa kupewa uraia kinguvu.
====
Ndugu Pascal Mayalla harakisha utekelezaji wa ombi langu la kutufundisha namna bora ya kuleta habari "as whistleblow".

Wateja tupo wengi.
 
Wanataka kumtoa kwa hiyo wanajaribu kutengeneza tuhuma feki. Kuna mtu wao wanataka kuwekwa pale.
 
Tunaomba ushahidi wa kupewa uraia kinguvu.
====
Ndugu Pascal Mayalla harakisha utekelezaji wa ombi langu la kutufundisha namna bora ya kuleta habari "as whistleblow".

Wateja tupo wengi.
Ndio Sasa kapewa unataka nitoe ushahidi mpaka niende migration huko na hyo kutoweka ushahidi haimaanishi jambo halipo na halijatendeka
 
Tumtetee msukuma mwenzetu kwa nguvu zote

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Ndio Sasa kapewa unataka nitoe ushahidi mpaka niende migration huko na hyo kutoweka ushahidi haimaanishi jambo halipo na halijatendeka
Habari hizi ulizipataje? Yaani uliahack system ya immigration, uliambiwa na mtu, ulishiriki kuwasilisha maelekezo ya kinguvu idara ya uhamiaji ili mtu apewe uraia, yaani ni namna gani ulipata habari hizi?
 
Habari hizi ulizipataje? Yaani uliahack system ya immigration, uliambiwa na mtu, ulishiriki kuwasilisha maelekezo ya kinguvu idara ya uhamiaji ili mtu apewe uraia, yaani ni namna gani ulipata habari hizi?
Wewe huko dunia gani mbona hayo mambo yamezungumzika tangu enzi za jiwe inajulikana maana vetting yake ilionyesha sio raia wa nchi hii hata ya madini kuibiwa Iko tangu mwendazake hajaondoka duniani.
N. B haya yangu tu hayahusiki na sukuma gang au interest ya cheo chochote Mimi ni Raia wa kawaida tu, so msije sema na chuki yoyote.
 
Naounga mkono hoja. Moyo wa mtu ni kichaka, hata siku moja usimsemehe mtu. Hivi Kuna kiongozi tz akikaa sehemu nyeti yenye mavumba asifanye ubadhilifu?? Tatizo bongo hakuna system inayowashughulikia wabadhirifu ipasavyo, watu wanaanza kwa kuteuliwa na wanaishia kutenguliwa

Yahani adhabu kubwa wanayopata ni kutumbuliwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…