Hongera JF kwa Whistleblow, JF tubadilike, tusichafue majina ya Watu kwa tuhuma za Hearsay zisizo na Uthibitisho, Ukituhumu, Weka Uthibitisho

Msukuma mwenzako huyo, una njaa hivyo kumkingia kifua ili angalau akupooze hiyo njaa siyo mbaya!
Wasukuma mmeamka sasa baada ya kuamshwa na mwendazake....
Ni kawaida binadamu kuelimishana na kuamshana.Mwendazake alikuwa na haki ya kuamsha watu wake kwa sababu moja tu.Charity starts at home.Hata akina Mramba marehemu walihusika kuwaamsha wachaga
 
Lazma atoke, Kwani nani alisema hii nchi ni ya WASUKUMA tu, mjomba wenu keshaondoka washenzi ninyi, mlidhani atatawala milele kaweka wasukuma wenzake sehemu zote zenye upigaji ili ajigaie mfyuuu zenu
Matusi hayatakusaidia wasukuma watabaki juu mawinguni, sehemu kubwa ya uchumi wa madini uko usukumani hakuna mbadala inabidi ukubaliane na hali.Kwa taarifa yako jamaa wameamka na hawatalala so usitegemee mteremko.By the way sidhani kama una haki ya kumtukana wasukuma unajitakia shida bure
 
Ni dotto huyuhuyu alikuwa kajigeuza mungu mtu aliyelibia taifa aliyetesa upinzani wakati wa mwendazake au ni dotto mwingine?
kuna watu wa upinzani wanaunga hoja ya P humu inashangaza

Lisemwalo lipo kama halipo linakuja.....

Huyu mnayesema mzalendo si mzalendo tuwe wakweli. P anasafisha wa kwao
P anatisha msiandike tetesi humu eti whistle naniliii
Let people talk write usiwatishe watu vile upo kwenye utawala
Kama kasingiziwa afungue kesi
Wakiumizwa watu alikuwa miongoni mwao watesi

JF ni zamani sio siku hizi hakuna cha whistle blower wala blawa wanafuta meeeeengi na kunanilii pia

P acha watu waseme tuna wezi na watesi wengi ktk Taifa wewe endelea kula keki ya Taifa mmebahatika mweh... hizi zingine ni porojo tu

Taifa lina mark time lipo pale pale tangu miaka 36 iliyopita. Pale Mwl alipokabidhi nchi kwa majambazi...
 
Jamani huyu mtu namfahamu. Nawafahamu ndugu zake zaidi ya 15. Nina uhakika wa 100% siyo Mtanzania, na siyo msukuma, japo anaongea kisukuma fluently.
Mbaguzi mbaguzi tu sasa umeshindwa kuthibitisha wizi wa Biteko umegeukia kabila lake.Mtateseka sana na wasukuma lakini wao wako buzzy wanasaka fursa.Sasa hivi wameingia Msumbiji na kule wameoa na kuzaa watoto wao mtasema siyo wasukuma.Mna shida nyie viumbe
 
Mnafiki tu huyu, mbona Kesi ya Mbowe kakaa kimya? Mbowe katukanwa matusi yote! Mayala acha unafiki, na Mimi nakutuhumu sasa " Mayala amepewa pesa kumsafisha Biteko" vimba upasuke
 
Kaka mkubwa upo sahihi lkn hizo tuhuma hazikuanza kwake km ckosei kuna wazir.wa mambo yandan wa fetha wa umeme upo kimya lkn umeshituka alipotajwa huyo wa madini na kutuaminisha kuwa msafi vip nawe unamaslai hapo.

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Jambo ambalo nimekuwa nikijiuliza, na hata wakati mwingine kuogopa, hivi ni kwa namna gani watu huwa wanapata ujasiri wa kutoa tuhuma dhidi ya mtu kwa kutumia hisia tu, au kwa kutumia vyanzo visivyo rasmi... God Forbid!

Na ujinga wa haya mambo, mtu ukiwa ni wa kushabikia haraka haraka unaweza kujikuta unatumika bila kujijua!! Yaani watu wana tofauti zao huko, ama za kisiasa au vinginevyo. Kutokana na hilo, mtu anaamua kutunga jambo kwa sababu anafahamu likishafika mitandaoni, fasta atapata watu wa kupigana vita yake bila wenyewe kufahamu kwamba wanatumika!!
 

Udhibitisho utafanywa na taasisi husika, mtoa taarifa kamaliza eneo lake.

Mahakama zipi za kutegemea katika mazingira haya?

Hiyo kesi ya Mbowe ni chain gani of custody imefuatwa, huyo jaji anajizungusha nini kama hiyo chain imefuatwa?
 
Bora mpush mwenzio anapigwa maneno tuu,
Simtetei kwasababu ni homeboy wangu, namtetea kwasababu namfahamu ni mtu muadilifu na mchapa kazi, asipigiwe majungu ya uongo, wivu, fitna na chuki binafsi.
ndugu mwandishi mkongwe nakukumbusha;
Wapo waloitwa magaidi wakawekwa na ndani muda mrefu kwa kusingiziwa!.
Masheikh wa Uamsho, tuliwasemea sana, tena sio humu tuu kwenye social media, sisi wengine tuna access hadi kwenye mainstream media za TV, Redio na Magazeti, na huwezi jua, usikute labda DPP aliamua kuwaachia huru masheikh baada ya kusoma mfululizo wa makala hizi humu jf na kwenye magazeti.
Rejea za Mfululizo huu wa makala za DPP
View attachment 1825142
View attachment 1825139
View attachment 1825143

Wapo walopigwa risasi kisa kusingiziwa wanaihujumu nchi!!
Hawa pia tuliwatetea, ila kwanza kile tuu kitendo cha mtu kupigwa risasi, japo ni ukatili na unyama, ila pia usikute tukio lile ni karma payback ya matendo ya mhusika, anaweza kuwa na yeye aliwapiga watu wengi sana risasi za maneno makali na tuhuma za uongo na uzushi, kwa kutoa risasi za maneno makali na hivyo karma ikamjibu kwa risasi za moto. Akina sisi tuliwapa angalizo kabla
Ila pia baada ya kupigwa risasi, kuna watu walidhani ni naniliu ndie anahusika, Mama akawaeleza wazi sio askari wetu, askari wetu akikosa kulenga target kwa risasi 3, ataandika Maelezo!. Hivyo ni uthibitisho wahusika ni watu wasiojulikana.
hili la wasiojulikana tumelipigia kelele sana humu na kwa vile serikali ilikosa pa kuanzia, akina sisi tulishauri
Wapo walosingiziwa mafisadi wakafungwa wakalipishwa mihela huku kiukweli hawajaiba
Hawa pia tuliwapigania sana, rejea zile makala za DPP.
Wapo walopoteza mamazao kwa mshtuko kufuatia kifungo chao kwakusingiziwa makosa hawakufanya....
Pia hawa tuliwapigania sana,
Ajabu mwandishi mkongwe katika wooote wewe umeumizwa na mpush mwenzio mpaka umeona umsemee huku kwanguvuuu unahisi jinalake linastahili usafi wahali yajuu...
Naamini nimeeleweka vya kutosha. Mimi ni mtetezi huru wa haki na nimetetea wengi akiwemo huyu gaidi kwa kueleza sio gaidi ni mhalifu tuu wa kawaida.
P
 
Ukimsikiliza Biteko, utakubaliana na mimi, huyu ni mzalendo wa kweli wa nchi hii, kumtuhumu kwa tuhuma lukiki bila ushahidi wowote au uthibitisho wowote, sio kumtendea haki.
Kusema hata Jiwe alikuwa anasema lkn anaiba pesa za umma anajenga chato kwao, kwa upendeleo bila ruhusa ya bunge! Usiyakubali maneno ya mtu...... kila mmoja can pretend!
Ila nakubaliana na wewe tuhuma lazima ziwe na ushahidi..
 
Ni kawaida binadamu kuelimishana na kuamshana.Mwendazake alikuwa na haki ya kuamsha watu wake kwa sababu moja tu.Charity starts at home.Hata akina Mramba marehemu walihusika kuwaamsha wachaga

Mramba aliamsha vipi wachaga? Mramba yeye ndiye aliyeamshwa na waliomtangulia..
 
Mkuu sblandes , asante sana kwa mchango huu. Viongozi wetu wote ni binadamu, hakuna malaika, hata JPM hakuwa malaika, wala Mama sio malaika, they are all human beings and can make mistakes au kuwa mafisadi, ila kwenye tuhuma ziwe ni tuhuma za kweli sio uongo, uzushi, fitna na majungu.
P
 
Udhibitisho utafanywa na taasisi husika, mtoa taarifa kamaliza eneo lake.

Mahakama zipi za kutegemea katika mazingira haya?

Hiyo kesi ya Mbowe ni chain gani of custody imefuatwa, huyo jaji anajizungusha nini kama hiyo chain imefuatwa?
Ni cardinal rule kuwa ukitoa tuhuma lazima uthibitishe.

Kesi ya Mbowe bado inaendelea hivyo basi kama chain of custody haikufuatwa basi tutajua.
 
Ni cardinal rule kuwa ukitoa tuhuma lazima uthibitishe.

Kesi ya Mbowe bado inaendelea hivyo basi kama chain of custody haikufuatwa basi tutajua.

Sio juu ya whistle blower kudhibitisha. Kwani ni hatua gani wamechukuliwa waliokutwa wamejiunganishia bomba la mafuta hata baada ya kudhibitika wizi huo?

Hiyo kesi ya Mbowe mpaka sasa jaji ameshaonyesha kaandikiwa hukumu, hivyo anajitahidi kutokuiangusha jamuhuri.
 
Kwa hiyo unatakiwa kupiga mbiu huku huna uthibitisho? Piga mbiu huku ukiwa na ushahidi. Hata wikileaks walipiga mbiu wakiwa na ushahhidi.

Sakata la Kigamboni watuhiwa walikamatwa, je hawakufikishwa mahakamani?

Kesi ya Mbowe bado inaendelea acha prejudice.
 

Umewahi kuwaona mahakama gani? Waziri mkuu na IGP walisema watatoa taarifa ndani ya siku 7. Umewasikia wakisema lolote? Sasa unataka whistle blower atoe ushahidi, wakati huo wa wako wazi mamlaka zimeufyata?

Hamna kesi yoyote ya Mbowe inayoendelea zaidi ya siasa chafu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…