Hongera Kenya(Kenyatta na Odinga) kwa kuuona mwanga na kufungua ukurasa mpya!

Hongera Kenya(Kenyatta na Odinga) kwa kuuona mwanga na kufungua ukurasa mpya!

Wengi wenu hamjui siasa za Kenya. Siasa za kenya ziko hivi hivi tangu wapate uhuru. Leo huyu anafanya ushirika na yule, Kesho wamekosana, keshokutwa aliyekuwa adui wa fulani ndiye mpiga debe wake mkubwa! Kwa kifupi wanajali matumbo yao na kila kitu wanachofanya wanakuwa wameweka maslahi ya matumbo yao mbele! Hivi nikikumbia kabla Uhuru hajachaguliwa kuna siku alienda nyumbani kwa Odinga wakiwa na familia yake na wakashinda wote huku wakila na kunywa utaamini? Siasa za Kenya siyo za kupigiwa mfano hata siku moja.
....Za kupigiwa mfano ni hizi za kuokota watu kwenye kiroba siyo?
 
I
"Nikiwa rais watalimia meno"," atakayenipinga nitampoteza ndani ya dk.5". Mtu hunena yaliyoujaza moyo wake,roho iliyojaa visasi ikeshayo ikijiapiza kufanya uovu inaanzaje kuandaa makongamano ya upatanisho?

Hiiiiiiii!!! Yaya ghete.
Inashangaza mtu anakuwa na moyo Mbaya hivi sijawahi ona katika awamu zote nne
 
Kuna rais mmoja wa huko nchi ya mbali anafikiri kufanya hivi ni udhaifu.

Hiki alichofanya UK itakuwa hajakielewa kabisa,maana yeye akiangalia huku na kule anaona kama anamiliki kila kitu,kujishusha hivyo ni udhaifu kwake.
 
Bavicha mnashangaza!
Lowassa alikwenda ikulu mkamporomoshea matusi,bakini na siasa zenu za kususa
 
Tanzania haina cha kujifunza Kenya ila Kenya wana cha kujifunza Tanzania

Kwa kuwa umasikini wa lugha umekuganda kama shati lililoloa, nakupa tafsiri ya kilichofanyika nchini Kenya...


Alhamisi tarehe 31/5/2018: Mapema leo asubuhi wakati wa Sara ya Kitaifa jijini Nairobi, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amemuomba msamaha muhasimu wake Raila Odinga na kutaka tofauti zao za kisiasa walizokuwa nazo kipindi cha Uchaguzi Mkuu wa Kenya ziweze kuisha na waijenge nchi yao. Naye Makamu wa Rais wa Kenya William Ruto amefanya hivyo hivyo kwa Kalonzo Musyoka.

Sisi hapa Tanzania tumefuzu katika kuupa msogo ustaarabu, tunawindana kama wanyama wa mwituni...
 
Kusema kweli kwa kitendo alichofanya Uhuru Kenyatta bila kujali nini kitaendelea baada ya hapo katika uwanja wa siasa Kenya kinahitaji pongezi na labda kujifunza.....
Wewe Dunyua vipi? Sisi haikuwa hand shake tu. Sisi Magufuli na Lowassa walikaa pamoja ikulu masaa kibao waki chat, kufurahi na kupata lunch. Wakatoka wawili na kutoa maneno matamu kwa waandishi wa habari. Kitendo hicho kikawauma sana chadema, wakafura na kuitisha mkutano wa dharura wa NEC kwa madhumuni ya kumwadabisha Lowassa. Sasa hapa anayepaswa kujifunza ni nani kama si chadema?
 
Hii ni kwale ambao lugha imewapiga chenga, haya ndio yaliyojiri kwenye hiyo video...

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amewataka radhi wote aliowakosea na kumtaka naibu rais William Ruto pia kufanya hivyo ambapo Ruto alikumbatiana na Kalonzo Musyoka pamoja na Raila Odinga.

Naye kinara wa chama kikuu cha Upinzani, ODM, Raila Odinga amewaomba radhi rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto kufuatia kutoelewana haswa wakati wa siasa za uchaguzi uliopita.

Kwa upande mwingine naibu rais William na Kalonzo Musyoka nao wameombana msamaha na kuahidi kuweka tofauti zao kando. Haya yamejiri kwenye maombi ya 16 ya kuliombea taifa yalio andaliwa jijini Nairobi.

Viongozi wote hao wanne wameahidi kuweka kando tofauti zao za kisiasa na kushikana katika kuendeleza taifa lao na kuwaunganisha Wakenya. Hongereni sana Wakenya kwa kuona mwanga na kufungua ukurasa mpya!

NB: Ni wazi habari kama hii ni mbaya sana kwa serikali ya Tanzania na wengi walioikumbatia hii serikali ya CCM watajitokeza wengi sana kwenye hii thread wakibeza na kuponda hatua hii ya ukomavu wa kisiasa uliooneshwa na jirani zetu.

Lakini huko kubeza na kuponda tunazidi tu kuonesha tulivyozama katika giza totoro kiasi kwamba hata tukikaza macho kiasi gani hatuoni kitu na hivyo kutojua faida ya mwanga.

Ukosefu wa mwanga umetufanya tusijue tunatoka wapi wala tunaelekea wapi na huu mwanga uliojipenyeza kutoka kwa majirani zetu huenda ukatuzindua na hivyo tukajitambua.

Uzuri na kinacholeta tumaini ni kwamba mwanga na giza hazikai pamoja, mwanga ukipiga hodi tu, giza hilooo linatokomea. And now there's already flicker of light at the end of this dark tunnel, thanks to the KENYANS!
 
Angeomba huo msamaha ile awamu yake ya kwanza alipopelekwa the hegue ndio ningemuona kamaanisha ila kaomba awamu ya pili anamalizia gwe yake , hiyo ni siasa na biashara ndani yake tu
Una mawazo ya Kiafrika,Muhimu kuwa kaomba msamaha,yeye ni raisi hana umuhimu wa kuomba msamaha hasa kwa vile hii ni awamu yake ya mwisho

Msamamaha aliouomba Kenyatta kaiweka kenya sehemu nzuri kaika kuwatika ramani ya dunia,kwa wawekezaji,kwa wafadhili,kwa fanya biashara nk
 
Uhuru mjuzi jana nimemuangalia vizuri kwanye maazimisho yao yaani anavyoongea utapenda,,kitu tunacho sie.
 
Wewe Dunyua vipi? Sisi haikuwa hand shake tu. Sisi Magufuli na Lowassa walikaa pamoja ikulu masaa kibao waki chat, kufurahi na kupata lunch. Wakatoka wawili na kutoa maneno matamu kwa waandishi wa habari. Kitendo hicho kikawauma sana chadema, wakafura na kuitisha mkutano wa dharura wa NEC kwa madhumuni ya kumwadabisha Lowassa. Sasa hapa anayepaswa kujifunza ni nani kama si chadema?
Dr Akili, mkutano wa Magufuli na Lowassa ajenda yake haikuwa uzuluhishi au maridhiano (reconciliation) ndio maana baada ya mkutano huo tukawa tunasikia minongono kuwa Lowassa alikwenda Ikulu kujaribu kuomba ghorofa lake la Ubungo Tanesco lisibomolewe, na minongono mingine Zaidi. Haukuwa mkutano wa kurudisha Umoja baada ya uhasama wa uchaguzi. Lowassa hakwenda kukutana na Magufuli katika nafasi yake ya kiongozi wa upinzani kwa baraka zote za Chama chake. Dr Akili kuna tofauti kubwa sana na walichokifanya Wakenya. Wakenya wamekutana katika mkutano maalumu wa kuliombea Taifa, kuweka sawa tofauti zao hadharani mbele ya wananchi hakuna ajenda zilizofichika. Chama cha upinzani na chama tawala vimekutana kuweka sawa tofauti zao. Dr kuna tofauti sana hapa.
 
Ni kweli wamefanya vizuri lakini pia ni kitendo kinachoonyesha kuwa siasa ni mchezo mchafu sana, wakenya wengi wamepoteza maisha kwa vuguvugu hizi, lakini leo kiurahisi tu watu wanashikana mikono eti wanasameheana, vipi kuhusu waliopoteza maisha? Ni siasa za maji taka hizo.
Ujinga wao kwani walitumwa, wanasiasa siku zote mtaji wao ni wajinga na wapumbavu wa kufikiri....ova.
 
....Za kupigiwa mfano ni hizi za kuokota watu kwenye kiroba siyo?
Hili ndilo tatizo la forum nyingi za Bongo. Ukiwa kinyuma na wanaoilaumu serikali basi wewe uko upande wa serikali. Tuanafanya ule ushabiki uliopitwa na wakati wa Simba na Yanga. Kuua vile vile siyo kuzuri. Sifu pale panapostahili na kosoa pale panapostahili. Siasa za Kenya huzijui wewe. Omba Mungu uzima ufike wakati wa uchaguzi ndiyo utashangaa (kama utakuwa na kumbukumbu kwani wabongo wengi hawana) jinsi watakavyogeukana na kuchochea mauaji!
 


Kusema kweli kwa kitendo alichofanya Uhuru Kenyatta bila kujali nini kitaendelea baada ya hapo katika uwanja wa siasa Kenya kinahitaji pongezi na labda kujifunza. Haya ndio mambo ambayo nchi yetu ilikuwa inasifika sana. Tanzania ilikuwa ndio nchi ya Africa iliyokuwa kimbilio kwa wale wenye magomvi na kutokuelewana wakaja Tanzania kupatanishwa. Vyama vya wapigania Uhuru kama ZANU na ZAPU viliweza unganishwa kwa juhudi za Mwalimu Nyerere ikatoka Patriotic Front nakumbuka Mwalimu pia alijaribu sana kuweza kuunganisha ANC na PAC vyama vya ukombozi wa Afrika kusini kipindi kile lakini naona pale hakufanikiwa lakini juhudi zilifanyika. Na najua wako wengine wengi wanaweza kuja na mifano mingi ya kuonyesha jinsi gani nchi yetiu ndio ilikuwa muubiri na mtekelezaji wa dhana ya Umoja ni Nguvu na utengano ni udhaifu. Tuliimba hizi nyimbo shule za msingi na kweli tulifanikiwa sana kujenga nchi moja yenye mshikamano usiojali dini, ukabila au rangi. Nafikiri hili tunahitaji kuliweka kama ndio msingi Mama kadri tunavyozidi kwenda mbele katika mapambano ya kujenga Tanzania yetu. Leo Kenya wamegundua kuwa utengano ni udhaifu. Watanzania tufungue macho na masikio tunayaone na kuyasikia haya na bila kuyapuuzia, kwa sababu ukweli hata siku moja haupuuzwi kama una nia ya kweli ya kuboresha na kujifunza.

Huku kwetu Lowassa akikutana na Magufuli, chadema wanafura hatari.
 
Nakuelewa sana Mkuu na hicho ndio kiini cha siasa bahati mbaya, UWONGO, UNAFIKI na FITINA kwa kiwango kikubwa. Ila tunachosema msingi iwe uzalendo kuweka maslahi ya Taifa mbele hivyo kujenga mazingira chanya (Amani na mshikamano) kuweza kujenga nchi. Hali halisi za siasa zetu za dunia ya tatu tunazijua. Lakini kitendo cha mwanasiasa kuweza kusema nimekosea naomba kusamehewa hata kama ni katika kulitumikia tumbo, lakini linaleta mshikamo kwa wananchi na kupunguza uhasama kwa wafuasi wao.
Nimekuelewa mkuu. Ila kuna umuhimu gani wa kufanya usanii wa kuomba kusahemehewa wakati ukifika uchaguzi unageuka na kuhamasisha mauaji? Mkuu hakuna viongozi wenye ubinafsi kuliko viongozi wa Kenya. Sisi Mwalim Nyerere alifanikiwa kuondoa hili tatizo kidogo ila sasa linarudi kwa kasi. Na nikisema hivi simaanishi kuwa Tanzania tuko vizuri ila tu natahadharisha kuwa Kenya siyo nchi ya kusifia kuhusu uongozi.
 
Back
Top Bottom